Uaminifu, Wakwe, na Siri za Ndoa | Émo Talk Show episode artwork

EPISODE · Jun 12, 2026 · 1H 2M

Uaminifu, Wakwe, na Siri za Ndoa | Émo Talk Show

from Émo Talk Show · host Tulia Mulemba

Je, ni kweli ku-cheat ni "asili" ya mwanaume na wanawake wanapaswa kuvumilia? Je, ndoa za kisasa zinashindwa kwa sababu tumeshindwa kuweka mipaka na wazazi au wakwe zetu? Katika kipindi hiki cha kusisimua, Tulia anakaa chini na wanandoa Furaha na Annick kujadili mambo mazito na magumu yanayoikabili jamii yetu ya Afrika Mashariki na Kati, hasa wale wanaoishi Diaspora.Tunaanza kwa kuvunja ule msemo wa sumu wa kwamba "wanaume ndo jinsi wanakuwaga" na kuzungumzia ukweli kuhusu uaminifu (fidelity). Furaha anafunguka na kueleza kwa nini mwanaume anaye-cheat ni mtu ambaye hajakomaa na "amevamia ndoa". Pia, Annick anashiriki kwa uwazi kwa nini anakataa kuhalalisha mateso kwenye ndoa na kwanini hachunguzi simu ya mume wake!Lakini mazungumzo hayaishii hapo. Tunaingia ndani zaidi kujadili shinikizo la kiutamaduni kutoka kwa wakwe na kile kinachoitwa "Black Tax". Unawazuiaje wazazi wasiendeshe ndoa yako? Inakuwaje pale maumivu ya kihisia kutokana na mahusiano yenye sumu yanaposababisha magonjwa ya kimwili kama presha na heart attack? Na kwa nini tunawafundisha watoto wetu wa kiume jinsi ya kutafuta pesa, lakini tunashindwa kuwafundisha jinsi ya kuwa waelewa kihisia (emotional intelligence)?Iwe wewe ni mwanandoa mpya, hujaoa/hujaolewa, au unapitia changamoto za mahusiano kwenye maisha ya ughaibuni, kipindi hiki kimejaa uponyaji, vicheko, na ukweli mchungu unaopaswa kusemwa.🔔 USISAHAU KU-SUBSCRIBE, KU-LIKE, NA KU-SHARE!Ungana na familia ya Émo tunapoendelea kuvunja miiko, kuponya jamii zetu, na kujifunza maana halisi ya upendo wenye afya. Tuambie kwenye comments: Je, unakubaliana na Furaha kwamba wanaocheat walivamia ndoa? Je, huwa unakagua simu ya mwenzako? Tuongee!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jun 12, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

Uaminifu, Wakwe, na Siri za Ndoa | Émo Talk Show

0:00 1:02:14

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Émo Talk Show?

This episode is 1 hour and 2 minutes long.

When was this Émo Talk Show episode published?

This episode was published on June 12, 2026.

Can I download this Émo Talk Show episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!