Wednesday 25 2020 Daily Mass episode artwork

EPISODE · Mar 25, 2020 · 34 MIN

Wednesday 25 2020 Daily Mass

from St. Joseph Cafasso King'ong'o Parish · host St Joseph Cafasso King'ong'o Parish

MASOMO YA MISA, MACHI 25, 2020 JUMATANO, JUMA LA 3 LA KWARESIMA SHEREHE YA KUPASHWA HABARI YA KUZALIWA BWANA SOMO 1 Isa. 7:10 – 14 Bwana alisema na Ahazi akinena,  Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini  sana, au katika mahali palipo juu sana. Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka,  wala sitamjaribu Bwana. Naye akasema, Sikilizeni sana, enyi nyumba ya  Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka  kumchosha Mungu wangu pia? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.  Tazama, Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita  jina lake Imanueli. Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu. WIMBO WA KATIKATI Zab. 40:6 – 10 (K) 7 , 8 (K) Tazama, nimekuja, Ee Bwana, kuyafanya mapenzi yako. Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja. (K) Katika gombo la chuo nimeandikiwa Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu. (K) Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa, Sikuizuia midomo yangu; Ee Bwana, unajua. (K) Sikusitiri haki yako moyoni mwangu; Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha fadhili zako wala kweli yako Katika kusanyiko kubwa. (K) SOMO 2 Ebr. 10:4 – 10 Haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo ajapo  ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea  tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;  Ndipo niliposema, Tazama nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa)  niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo  na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa  nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo aliposema, Tazama,  nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi  alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa  mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu. SHANGILIO Yn. 1:14 Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukaona utukufu wake. INJILI Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa  Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa  na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni  Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema.  Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake,  akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia,  Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua  mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa  mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye ju, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi  cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme  wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno  hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu  atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;  kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa  Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto  mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa  tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema,  Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha  malaika akaondoka akaenda zake. Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

NOW PLAYING

Wednesday 25 2020 Daily Mass

0:00 34:24

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

Zero Așteptări Paul Puscas Podcastul nostru, este un refugiu de pace și introspecție în tumultul cotidian și în mijlocul așteptărilor adesea nerealiste ale societății. Ne-am dedicat acest spațiu digital pentru a oferi o platformă celor care doresc să exploreze diverse perspective și să participe la discuții deschise, autentice, fără prejudecăți sau anticipații predeterminate. Fiecare episod pe care îl lansăm este o invitație la reflecție și explorare personală, acoperind o gamă largă de subiecte, de la dezvoltare personală și spiritualitate, la cultură, artă și știință, prezentate întotdeauna într-o manieră acc MomDocs St. Louis Childrens Hospital - MomDocs A monthly podcast from Washington University pediatric specialists at St. Louis Children’s HospitalThe MomDocs are pediatricians at St. Louis Children’s Hospital. They work in a variety of specialties and share their advice and expertise on the questions we all face as parents. Cztery pory roku Polskie Radio S.A. Codziennie w podcaście „Cztery Pory Roku” opowiadamy o ważnych sprawach. Prowadzący i reporterzy są tam, gdzie dzieją się interesujące rzeczy. Przenosimy do podcastu tradycję audycji i nowe spojrzenie na świat, to właśnie są cztery pory roku. Alcatraz Radio2 "Fratello, la cosa assurda non è che sono un italiano nel braccio della morte di un carcere di massima sicurezza degli Stati Uniti. La cosa assurda è che tu stai fuori. Che tutti lì fuori siete liberi e state di schifo. Dov'è la tua libertà, tesoro? Nei lager dei quartieri di merda in cui vi hanno ficcato come bestiame, che cosa vi aspettate di diventare, onorevoli? Vi tengono in vita solo perché dovete comprare. Consigli per gli acquisti? Fanculo. Chi di noi due è nel braccio della morte? lo o te? Benvenuto ad Alcatraz, tesoro.”

Frequently Asked Questions

How long is this episode of St. Joseph Cafasso King'ong'o Parish?

This episode is 34 minutes long.

When was this St. Joseph Cafasso King'ong'o Parish episode published?

This episode was published on March 25, 2020.

What is this episode about?

MASOMO YA MISA, MACHI 25, 2020 JUMATANO, JUMA LA 3 LA KWARESIMA SHEREHE YA KUPASHWA HABARI YA KUZALIWA BWANA SOMO 1 Isa. 7:10 – 14 Bwana alisema na Ahazi akinena,  Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini  sana, au...

Can I download this St. Joseph Cafasso King'ong'o Parish episode?

Yes, you can download this episode by clicking the download button on the episode player, or subscribe to the podcast in your preferred podcast app for automatic downloads.
URL copied to clipboard!