03 MACHI 2026 episode artwork

EPISODE · Mar 3, 2026 · 9 MIN

03 MACHI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Leah Mushi

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Mashariki ya Kati ambako Leo ni siku ya nne ya mzozo mabomu yameripotiwa kuendelea kulipuka. Makombora yanarindima katika ukanda huo huku ndege zisizo na rubani au droni zikisababisha maafa sasa katika nchi 12. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Mgogoro wa Iran ukiendelea kupamba moto, Umoja wa Mataifa na mashirika yake wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu kuhusu hali hiyo tete huku wakiendelea kuhamasisha amani kupitia diplomasia kwani tayari madhara ya moja kwa moja kwa wanadamu yameshaonekana. Mathalani leo Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, OHCHR, Ravina Shamdasani akirejelea  tukio moja baya la kusikitisha ambapo inaripotiwa wasichana kadhaa waliuawa na kujeruhiwa wakati shule yao ya msingi huko Minab, kusini mwa Iran, iliposhambuliwa wakati wa saa za masomo, amesema, “watoto, wasichana wadogo katikati ya siku ya shule, mwanzoni mwa siku ya masomo, wanauawa kwa namna hii, mabegi yao ya shule yakiwa na, unajua, madoa ya damu juu yake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA leo limeeleza kwamba kulingana na picha mpya za satelaiti, sasa linaweza kuthibitisha baadhi ya uharibifu wa hivi karibuni kwenye majengo ya milango ya Kiwanda cha Kuchakata Mafuta cha FEP kilichojengewa chini ya ardhi huko Natanz, Iran. Ujumbe wa IAEA umefafanua kuwa hakuna athari zozote za mionzi zinazotegemewa na hakuna athari za ziada zilizobainika kwenye Kiwanda cha FEP chenyewe, ambacho tayari kilikuwa kimeharibiwa vibaya katika mzozo wa mwezi Juni.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wanyamapori mwaka huu kaulimbiu ya siku ikilenga “Mimea ya Dawa na Harufu nzuri inaangazia nafasi muhimu ya mimea hii katika kudumisha afya ya binadamu, urithi wa kitamaduni, na kipato cha jamii za wenyeji. Katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akionesha wasiwasi wake kuhusu kutoweka kwa miea asili ya dawa ametoa wito akisema,ninazihimiza nchi zote ziwe watunza bustani wa rasilimali za pamoja za dunia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Mar 3, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

03 MACHI 2026

0:00 9:58

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on March 3, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!