PODCAST · news
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
by United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
-
100
25 AGOSTI 2026
UN na ICRC watoa wito mpya wa kanuni kuhusu silaha zinazojiendesha zenyewe.Mageuzi ya Kilimo ya Malawi: Mwanzo mpya kwa wakulima wadogo.Vijana wa Yambio Sudan Kusini wataka elimu, usalama na nafasi zaidi katika uamuzi.
-
99
24 AGOSTI 2026
Siku 100 tangu Ebola kutangazwa nchini DRC hali inazidi kuwa mbaya.Pamoja na kuchukua hatua WHO yaonya kuhusu kuongezeka kwa wagonjwa wa mpox Guinea-Bissau. Ufadhili mpya wa dola milioni 22 za marekani kwa elimu ya watoto walioathiriwa na mgogoro Sudan.
-
98
21 AGOSTI 2026
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nduha anakuletea-Julien Harneis, Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Ebola amesema nchini DRC “Katika miezi mitatu iliyopita watu 2,500 wamekufa na nusu yao wamekufa katika kipindi cha siku tatu zilizopita na mlipuko unaendelea kusambaa zaidi, hivi sasa umesambaa katika eneo lenye ukubwa sawa na nchi ya Ufaransa.”-Hali ya ukosefu wa fedha ni mbaya pia nchini Somalia ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema kuwa kupunguzwa kwa ufadhili wa kibinadamu nchini Somalia kumesababisha kufungwa kwa vituo 205 vya afya na lishe, huku watoto wanaougua utapiamlo mkali wakisafiri umbali mrefu kutafuta matibabu wakati mwingine wakifika hospitalini wakiwa katika hali mahututi.-Leo ni ni siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Waathirika wa Ugaidi Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amezungumzia kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Uponyaji kupitia Kumbukumbu,” akasisitiza kuwa kuwakumbuka waathirika kunaweza kuwa njia ya kuelekea uponyaji na kuanza upya.-Na katika mada kwa kina leo tuko Uganda kwake manusura wa ugaidi Hassan Ndugwa akisimulia kilichomsibu 2010 na hatua alizochukua katka kupambana na itikadi kali na fikra potofu kuhusu ugaidi na kuudhibiti
-
97
20 Agosti 2026
Tume ya UN: Uchaguzi Sudan Kusini usigeuke kuwa uwanja mwingine wa mapiganoWFP yaongeza operesheni za msaada kwa manusra wa teteko la ardhi ColombiaUmoja wa Mataifa na Sudan Kusini waimarisha maandalizi dhidi ya Ebola
-
96
19 AGOSTI 2026
Leo katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataofa Flora Nducha anakuletea --Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wahudumu wa Kibinadamu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kuwalinda wahudumu wa kibinadamu wanaotoa msaada wa kuokoa maisha katika maeneo yenye migogoro-Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura (OCHA) iliyotolewa leo katika kuadhimisha hii imeonya kwamba wahudumu 907 wa kibinadamu walikumbwa na vitendo vya ukatili mwaka jana, wakati wakitekeleza kazi zao za kuokoa maisha katika maeneo ya migogoro yanayozidi kuwa ya hatari.-Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, amesema ana wasiwasi kuhusu taarifa za kukamatwa na kuzuiliwa kwa wanachama wa vyama vya upinzani nchini Zambia kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 13 katika ncho hiyo ya barani Afrika.-Na katika mada kwa kina hii leo tunaye Muhudumu wa Kibinadamu Cedric Lusimba muuguzi aliyehudumu katika maeneo mbalimbali yenye mizozo
-
95
JIFUNZE KISWAHILI - NENO KARAKARA
Sasa umewadia wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KARAKARA"
-
94
18 AGOSTI 2026
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Leo WHO imefanya mkutano wa pili wa kamati ya dharura ya kanuni za afya za Kimataifa mjini Geneva Uswisi kutathmini kuhusu mlipuko wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.-WHO pia imezungumza na waandshi wa habari DRC katika jitihada za kupambana na Ebola na pia kuhakikisha jamii inashirikishwa ipasavyo ikiwemo waendesha pikipiki au boda boda-Ripoti mpya iliyotolewa leo na WHO na UNICEF, imeonesha kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana katika muongo mmoja uliopita, vituo vingi vya afya duniani bado havina huduma za kutosha za maji, vyoo na usafi.-Katika mada kwa kina leo utamsikia Emmanuel Madragule muhudumu wa kibinadamu Bunia DRC anayefanya kazi na OCHA akieleza kinachumsukuma kuendelea kutoa huduma ya kibinadamu-Na katika jifunze Kiswahili utasikia maana ya neno "KARAKARA"
-
93
Sudan Kusini : Wakimbizi wako hatarini kukosa chakula yasema UN
Zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi 650,000 nchini Sudan Kusini wako katika hatari ya kupoteza msaada muhimu wa chakula na lishe kutokana na ukosefu mkubwa wa fedha, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, na lile linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR zimeonya. Kupunguzwa kwa msaada kunaweza kuwaathiri wakimbizi 240,000 ndani ya wiki chache, wakati nchi hiyo yenyewe ikikabiliwa na ongezeko la tatizo la njaa. Feissal Kirwa na taariifa zaidi(TAARIFA YA FEISSAL KIRWA)Nattss…..Katika makazi ya wakimbizi ya Wedweil nchini Sudan Kusini, akina mama na watoto wanasubiri msaada wa chakula na lishe ambao wengi wanategemea ili kuendelea kuishi.Zaidi ya watu milioni 7.8 nchini Sudan Kusini ambani zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, huku watoto milioni 2.2 wakikabiliwa na unyafuzi.Sasa, mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa wakimbizi wanaofika nchini humo wakiwa tayari na utapiamlo mkubwa wanaweza kukabiliwa na hali mbaya zaidi iwapo ufadhili utaisha.Katika vituo vya lishe, watoto hupimwa uzito na urefu huku wahudumu wa afya wakifuatilia hali yao, wakati akina mama wakipewa chakula cha ziada kwa ajili ya watoto wao. Naibu Mkuruengenzi wa WFP nchini Sudan Kusini ni Adham Effendi,(SAUTI YA ADHAM EFFENDI- RASHID)“Bila ufadhili wa haraka, msaada kwa zaidi ya wakimbizi 650,000 utapunguzwa, na hivyo kuweka maisha na mustakabali wao hatarini. Hii inaweza kumaanisha mgao mdogo wa chakula na kupunguzwa kwa msaada wa lishe kwa watoto na akina mama.”Kwa wakimbizi wengi wapya, msaada huanza mara tu wanapowasili Sudan Kusini. Biskuti zenye virutubisho na za kutia nguvu hutolewa kwa watu ambao huenda hawana sehemu za kupikia au maji safi.Lakini wimbi la watu wanaokimbia migogoro linaendelea kuongezeka.Idadi ya wakimbizi na watu wanaorejea nchini humo takrivab 3,000 wanafika Sudan Kusini kutoka Sudan kila wiki, na kuongeza shinikizo kwa jamii na huduma ambazo tayari zimeelemewa. Adham anaongeza(SAUTI YA ADHAM EFFENDI 2- RASHID)“Msaada wa chakula mara nyingi ndio tofauti kati ya kukabiliana na hali ngumu na janga. Pamoja na washirika wetu UNHCR na wengine, WFP inawasaidia wakimbizi na jamii zinazowapokea. Lakini mahitaji yanaongezeka kwa kasi zaidi kuliko rasilimali zilizopo.”Baadhi ya familia sasa zimejikuta zikilala chini ya miti baada ya kukimbia Sudan.Miongoni mwao ni Saleh, anayepika chakula cha mchana huku mke wake akimtunza mtoto wao wa miezi sita.Wengine, kama Esraa, wameishi katika makazi hayo ya wakimbizi kwa miaka kadhaa. Msaada wa fedha kutoka WFP umemsaidia kununulia familia yake chakula na kuendesha biashara yake ndogo.Lakini msaada huo muhimu sasa uko hatarini kutoweka.WFP na UNHCR zinasema uhaba wa fedha unaweza kulazimisha kupunguzwa kwa mipango ya chakula na lishe kwa mamia ya maelfu ya wakimbizi na waomba hifadhi.Mashirika hayo yanaonya kuwa kupungua kwa msaada kunaweza kusababisha ongezeko la utapiamlo miongoni mwa watoto, huku wanawake na watoto wakikabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kukatili na kudhulumiwa.Huku njaa ikiwa tayari imeenea nchini Sudan Kusini na wakimbizi wapya wakiwasili kila wiki, mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanatoa wito wa ufadhili wa haraka ili kuzuia hali kuzorota zaidi na kulinda familia zilizo katika mazingira hatarishi dhidi ya njaa kali na utapiamlo.
-
92
FAO yawezesha wanawake na vijana katika sekta ya mwani Zanzibar
Nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) tangu mwaka 2019, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaimarisha sekta ya mwani, kwa kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuongeza uzalishaji, tija na kipato. Miongoni mwa walionufaika zaidi ni vikundi vya wanawake, ambavyo vimejengewa uwezo kuhusu mbinu bora za uzalishaji, uanikaji na uhifadhi wa mwani, pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi anatuletea taarifa inayomhusu mnufaika mmoja wa mafunzo hayo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Jumla ya vikundi 33 vya wanawake vimewezeshwa kwa chanja bora za kuanikia mwani na maturubai maalum ya kuufunika wakati wa mvua.Aidha, wanawake wamejengewa uwezo kuhusu teknolojia ya kilimo mchanganyiko inayowawezesha kulima mwani sambamba na kufuga majongoo bahari.Teknolojia hii inalenga kuongeza tija, kuboresha matumizi ya rasilimali za bahari na kuwawezesha wanawake kupata vyanzo mbalimbali vya kipato.FAO pia imewawezesha vijana kupitia Zanzibar Technology and Business Incubator (ZTBI), kwa kuwapatia mafunzo kuhusu usindikaji, ubunifu na uongezaji thamani wa bidhaa za mwani. Mafunzo hayo yamejikita pia katika uboreshaji wa ubora, upatikanaji wa ithibati na masoko, huku vijana wakipatiwa vifaa vya kuendeleza uzalishaji na ujasiriamali katika sekta ya mwani.
-
91
Licha ya changamoto mijini, Somalia yafanikisha kampeni ya chanjo ya polio
Zoezi la siku tano la utoaji chanjo dhidi ya polio limekamilika katika mkoa wa Banadir nchini Somalia, likiwafikia watoto zaidi ya 122,000 walio chini ya umri wa miaka mitano. Kampeni hiyo imeendeshwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Flora Nducha.(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Kampeni hiyo imetekelezwa katika wilaya za Daynile, Garasbaley na Kahda, ambako kuna familia nyingi zilizolazimika kuyakimbia makazi yao na ambazo imekuwa vigumu kuwafikia watoto wao katika kampeni zilizopita.Kwa muda wa miezi mitatu, Wizara ya Afya ya Somalia, utawala wa mkoa wa Banadir, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na wadau wengine walifanya maandalizi ya kina ili kuwafikia watoto walio hatarini zaidi.Katika utekelezaji wake, timu 178 zilitumwa kutoa chanjo ya matone dhidi ya polio nyumba kwa nyumba, katika vituo maalumu, maeneo ya vituo vya mpito na kupitia timu zinazohamahama.Timu hizo zilitumia takwimu za idadi ya watu, ramani za kijiografia na taarifa kutoka maeneo husika kutambua makazi na watoto ambao hawajapata chanjo.CHANGAMOTO MIJINIKatika taarifa yake kutoka Mogadishu nchini Somalia, WHO imeeleza kuwa kufikia kila mtoto katika maeneo ya mijini bado ni changamoto.Mkoa wa Banadir unapokea watu wengi wanaokimbia maeneo mengine kutokana na ukosefu wa usalama nchini Somalia. Baadhi yao huishi katika makazi yasiyo rasmi na kuhama mara kwa mara, hali inayofanya iwe vigumu kuwatambua na kuwafuatilia watoto ambao hawajapatiwa chanjo.Licha ya changamoto hizo, watoto 122,067 walipatiwa chanjo, sawa na asilimia 94 ya lengo la awali. Juhudi zinaendelea, watoto waliokosa chanjo watatafutwa na kupatiwa huduma hiyo haraka.Mwakilishi wa WHO nchini Somalia, Dkt. Mohamed Ali Kamil, amesema “Kumfikia kila mtoto kunahitaji uongozi imara wa serikali, ushiriki wa jamii na ushirikiano madhubuti wa wadau wote. Kampeni hii ni fursa muhimu ya kujaribu mbinu inayolenga zaidi mahitaji na kuimarisha uwajibikaji katika utoaji chanjo mijini.”KWA NINI CHANJO YA POLIO?Chanjo hiyo ni muhimu kwa sababu polio inaweza kusababisha ulemavu wa kudumu, lakini pia inaweza kuzuilika kwa chanjo.Somalia imekuwa ikikabiliana na mlipuko wa polio tangu mwaka 2017, hivyo kumfikia kila mtoto ni hatua muhimu katika kuziba pengo la kinga, kukomesha maambukizi na kulinda kizazi kijacho.
-
90
17 AGOSTI 2026
Karibu usikilize jarida la habari za UN ambalo leo habari zake zote zimetoka barani Afrika. Utasikia kuhusu juhudi za kutoa chanjo wa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 huko nchini Somalia.Utasikia namna FAO inavyowasaidia wananchi huko Zanzibar kuongeza ubora wa zao la Mwani.Na mwisho utasikia ufinyu wa bajeti unavyoathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini.
-
89
14 agosti 2026
Karibu kusikiliza jarida ambapo leo utasikia mahojiano na kijana kutoka nchini Kenya Feisal Kirwa aliyekuwa akishiriki mafunzo kwa Vitendo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa muda wa miezi sita na sasa amehitimu mafunzo hayo. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari.
-
88
13 AGOSTI 2026
Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Harakati za kutokomeza Ebola ya virusi vya Bundibugyo huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, zinakumbwa na mkwamo kwani wananchi wamesema wanahitaji sio tu matibabu dhidi ya ugonjwa huo, bali pia maji, chakula, matibabu ya malaria, chanjo na huduma za afya uzazi, mama na mtoto.-hirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mpya kuhusu ubora wa maji ya kunywa, likizitaka nchi kuimarisha kanuni, ufuatiliaji na usimamizi wa hatari zozote zinazoweza kujitokeza . Licha ya maendeleo yaliyopatikana, watu bilioni 2.1 bado hawana huduma ya maji ya kunywa inayosimamiwa kwa usalama-kingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, OHCHR, imezisihi mamlaka za Israel kusaidia familia za Wapalestina ambazo zimezingirwa na walowezi ndani ya nyumba zao kwa siku kadhaa, huku kampeni ya kuwapokonya ardhi yao ikizidi kushika kasi.-Na katika mada kwa kina leo tunajikita na Akili Mnemba (AI) na kilimo na kilimo biashara Afrika utamsikia Afisa wa FAO Meshack Malo
-
87
12 AGOSTI 2026
Katika Jarida la habari hii leo Flora Nducha anakuletea-Leo ni Siku ya vijana Duniani Umoja wa Mataifa wasisitiza umuhimu wa kuwasikiliza, kuwapa fursa na kuwasaidia vijana kuchangia na kushamiri katika jamii-Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kuhusu ajira kwa kundi la vijana inasema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana duniani umeongezeka, huku ukuaji dhaifu wa uchumi na upungufu wa nafasi mpya za kazi ukiwaweka vijana katika mazingira magumu ya kuingia katika soko la ajira.-Katika mada kwa kina utamsikia kijana kutoka Tanzania Zephania Opiyo aliyepata fursa ya mafunzo kwa vitendo Umoja wa Mataifa sasa amehitimisha na anatanabaisha safari yake na wito kwa vijana wenzie
-
86
-
85
-
84
-
83
11 AGOSTI 2016
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Feissal Kirwa anakuletea-Idadi ya vifo na majeruhi kufuatia tetemeko la ardhi nchini Colombia inaongezeka huku Umoja wa Mataifa ukianza kuwasilisha msaada muhimu kwa waathirika na kuwa tayari kusaidia kwa kila hali-Nchini Tanzania serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF inahakikisha kila mtoto anasajiliwa pindi anapozaliwa -Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana itakayoadhimishwa kesho Agosti 12 leo utasikia sauti za vijana mbalimbali wakigusia ajira, elimu na maisha kwa ujumla.
-
82
10 AGOSTI 2026
Mada kwa kina leo inamulika ubunifu wa aina yake wa kugeuza mabaki ya nywele za binadamu kuwa mbolea asilia, hatua ambayo inatekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Je nani anafanya? Na inafanyika wapi? Ungana na Assumpta Massoi kwenye mada hii kwa kina inayoanza na utambulisho wa muhusika kutoka Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, barani Afrika.
-
81
JIFUNZE KISWAHILI - NENO MADHILA
Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MADHILA"
-
80
07 AGOSTI 2026
Miaka 20 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) Tanzania inasema inajivunia mafanikio makubwa ya ujumuishwaji , je ni mafanikio gani hayo na ni katika nyanja gani? Kupata undani ungana na Maryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum nchini Tanzania akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
-
79
06 AGOSTI 2026
Leo tunaangazia hatua kubwa katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi, VVU, ambapo Zimbabwe imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza duniani kuanza kutoa Lenacapavir, sindano ya kinga inayotolewa mara mbili tu kwa mwaka na yenye ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Hatua hiyo inaimarisha juhudi za nchi hiyo yenye kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.2, ikilenga zaidimakundi yaliyo hatarini, hususan wasichana balehe na wanawake vijana ambao wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa maambukizi. Hata hivyo, pamoja na matumaini hayo, changamoto za upatikanaji wa dawa hiyo, gharama, unyanyapaa pamoja na ufikiaji wa huduma katika maeneo ya vijijini bado zinaendelea kuathiri kasi ya mafanikio. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI, UNAIDS, Feissal Kirwa wa idhaa hii amefuatilia kwa kina.
-
78
JIFUNZE KISWAHILI - NENO MZIO
Sasa umewadia wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MZIO"
-
77
05 AGOSTI 2026
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Feissal Kirwa akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya amani na usalama, usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama, haki za binadamu na hali ya hewa.MUHTASARI1. Wimbi jipya la mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya raia na majeruhi wengi, limelaaniwa vikali na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, akisisitiza kuwa raia lazima walindwe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.Mashambulizi hayo ya usiku yaliyoanza mwezi huu wa Agosti yamekuja baada ya mwezi Julai kuwa mwezi ulioshuhudia idadi kubwa zaidi ya vifo vya raia nchini Ukraine tangu Aprili mwaka 2022. 2. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake Jeremy Laurence, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa utekelezaji wa hukumu za kifo nchini Iran. Kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, adhabu ya kifo inaendelea kutumiwa kama njia ya kuwatia hofu wananchi na kukandamiza sauti za wanaopinga serikali.Akizungumza leo jijini Geneva, Uswisi, Jeremy Laurence amesema,“tunazihimiza mamlaka za Iran kusitisha mara moja utekelezaji wa hukumu zote za kifo na kuelekea katika kufuta kabisa adhabu ya kifo.” 3. Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaonesha kuwa uimarikaji wa mwenendo wa hali ya hewa ya El Niño unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula duniani hadi mwaka 2027. Shirika hilo linaongeza juhudi za kujiandaa na kukabiliana na athari hizo, huku El Niño ikiwa tayari imeanza kuwaathiri watu walio katika maeneo yenye hali ya njaa. MADA KWA KINAKituo kipya cha kutoa huduma kwa walioambukizwa ugonjwa wa Ebola, kinafunguliwa wiki hii huko Bunia, jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibuvyo. Kituo hiki kitakuwa kituo kikubwa zaidi nchini humo cha kutibu Ebola. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anatupitisha kwa kutumia video iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA.
-
76
04 AGOSTI 2026
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama pamoja na afya.Muhtasari wa habari:Utapiamlo mkali nchini Afghanistan umefikia viwango vya kutisha, huku majimbo 12 yakirekodi kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa cha utapiamlo miongoni mwa watoto wakati huu watu milioni 14 wakikabiliwa na njaa kali, imesema WFP.Mjumbe Maalum wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) kwa ajili ya Sudan, Derk Segaar, leo amewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kwamba wiki iliyopita alisafiri kwa njia ya Barabara nchini Sudan na kwamba ingawa macho ya dunia yameelekezwa zaidi katika maeneo ya Darfur na Kordofan, athari za vita zinaendelea kote nchini Sudan ambayo ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani, lakini pia ni miongoni mwa migogoro inayopuuzwa zaidi.Na Umoja wa Mataifa na wadau wake wanaendelea kuisaidia Rwanda kujiandaa dhidi ya Ebola. Hatua hizo zinajumuisha ufuatiliaji katika vituo vya afya, jamii na mipakani, huku zaidi ya wahudumu 100 wakipelekwa kwenye vituo vya kuingilia nchini. Pia, wahudumu karibu 400 wanapatiwa mafunzo ya utambuzi wa mapema.Mada kwa kina:Na sasa ni wasaa wa mada kwa kina inayotupeleka nchini Afrika Kusini, ambako dawa mpya ya kujikinga na Virusi Vya Ukimwi, VVU, iitwayo Lenacapavir, imeanza kutolewa kama sehemu ya jitihada dhidi ya maambukizi mapya, hasa miongoni mwa vijana walio katika hatari kubwa zaidi.Kwa mara ya kwanza, mtu anaweza kujikinga na VVU, kwa kudungwa sindano moja tu kila baada ya miezi sita, bila kumeza kidonge kila siku. Lenacapavir imeonesha ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi, na sasa imeanza kutolewa katika nchi tisa barani Afrika, ikiwemo Afrika Kusini, nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na VVU. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anakusimulia. Kwako Feissal.
-
75
JIFUNZE KISWAHILI - NENO : KUROA
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda Burundi, ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika na mchambuzi wetu ni Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUROWA”.Hiki ni kitenzi kikimaanisha kuvua samaki na nomino yake ni mroaji.Sentensi: Mroaji ameenda ziwa Tanganyika kuangalia iwapo atapata kitoweo cha samaki.Hii inamaana mroaji pia ni mvuvi, na mchambuzi wetu anasema kwa ukanda wa Maziwa Makuu, mroaji ni mvuvi.
-
74
03 AGOSTI 2026
Ili kufahamu ni kwa namna gani Chuo Kikuu cha Mount Kenya kinawasaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kifedha lakini wana uwezo wa kitaaluma ikiwa ni sehemu ya juhudi za chuo hicho kushiriki katika kuhimiza Malengo 17 ya maendeleo endelevu,SDG na kuunga mkono utekelezaji wake., Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye alikiwakilisha chuo hicho katika Kongamano la Kimataifa kuhusu Elimu ya Juu lililofanyika mwezi uliopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
-
73
31 JULAI 2026
Hii leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya, katika Kijiji cha Embulbul kilichoko Kaunti ya Kajiado, ambako Shirika lisilo la kiserikali la Tulivu Safe Haven, lililoanzishwa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa, linatekeleza hatua mbalimbali za kuwasaidia wanawake. Hii ni pamoja na kuwaokoa na kuwahifadhi manusura wa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia makazi salama, ushauri nasaha, msaada wa kisheria na uwezeshaji wa kiuchumi, sambamba na kuwarejesha shuleni wasichana walionusurika. Je, nini kinafanyika? Kupitia video iliyoandaliwa na Redio washirika wetu Domus, Feissal Kirwa amefuatilia simulizi za manusura na kutuandalia makala hii. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Maabara tembezi ya kupima virusi vya Ebola imewekwa katika mji wa mpakani wa Kasenyi ulioko kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kuna hatari kubwa ya kushamiri kwa mlipuko wa Ebola kutokana na harakati nyingi za safari. Dkt. Olga Ntumba kutoka WHO ambayo inafadhili maabara hiyo inayotoa majibu ndani ya saa moja, amesema “virusi haviheshimu mipaka. Maabara hii ina mchango muhimu kubaini mapema wagonjwa, kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa, kubadilishana taarifa na juhudi za mwitikio kwenye ukanda mzima.”Mioto ya nyika ikiendelea kutikisa maeneo ya kaskazini mwa dunia shirika la Umoja wa Matiafa la Afya duniani, WHO limekumbusha kuwa moshi utokanao na mioto hiyo ya nyika huvuka taifa, kanda na hata mabara na kuwa na madhara kwa watu hata wanaoishi mbali na moto wenyewe. Hivyo limetangaza mambo tisa ya kuzingatiwa ikiwemo kusikiliza taarifa za mamlaka kama vile viwango vya uchafuzi wa hewa, kuvaa barakoa na kusalia ndani ya nyumba na kufunga madirisha iwapo hujashauriwa kuhama.Na wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama ikianza kesho Agosti Mosi, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake, lile la afya, (WHO) na la kuhudumia watoto, (UNICEF) umetaka nchi kuimarisha mifumo ya afya ili iweze kupatia akina mama na watoto wachanga msaada wa kufanikisha unyonyeshaji bora ambao ni msingi wa ukuaji bora wa mtoto na afya ya mama anayenyonyesha. Halikadhalika utekelezaji wa kanuni ya kimataifa kuhusu matangazo ya bidhaa za mbadala wa maziwa ya mama.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, karibu!
-
72
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, “KUSOROZA.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUSOROZA.”
-
71
30 JULAI 2026
Hii leo tunakuletea mada kwa kina. Mlipuko wa sasa wa ebola ya virusi vya Bundibugyo uliotangazwa rasmi huko DRC mwezi Mei mwaka huu unazidi kuongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida, wamesema maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wakizungumza na waandishi wa habari Karl Skau, Kaimu Mkuu wa WFP, na ndio tunakupeleka nchini humo kufuatilia juhudi za kuudhibiti.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ni wakati wa dunia kuungana kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji wa watu, hususan aina mpya inayokua kwa kasi ya kulazimishwa kufanya utapeli kwa njia ya mtandao. Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Watu inayoadhimishwa kila mwaka tarehe thelathini Julai, amesema wahalifu wanawavutia watu kwa ahadi za ajira nzuri, lakini baadaye wanawafanya mateka na kuwalazimisha kuendesha utapeli mtandaoni. Guterres amezitaka nchi kuridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Uhalifu wa Mtandao uliopitishwa mwaka 2024, kushirikiana kuvunja mitandao ya uhalifu na kuwasaidia manusura kurejea katika maisha yao ya kawaida.Nchini Ukraine, mashambulizi makubwa ya usiku yaliyojumuisha makombora na mamia ya ndege zisizo na rubani yamesababisha vifo na majeruhi katika maeneo kadhaa ya makazi, yakiwemo miji ya Kryvyi Rih, Kyiv na Lviv. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, imesema nyumba na shule za awali zimeharibiwa huku watoto wakiwa miongoni mwa waliouawa na kujeruhiwa. Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema watoto watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, huku likiendelea kutoa msaada wa dharura wa kisaikolojia na usaidizi wa kifedha kwa familia zilizoathirika.Na Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, amelaani hatua za serikali ya Uganda zinazodaiwa kuendelea kubana uhuru wa msingi na kuzima sauti za wanaokosoa serikali. Amesema tangu uchaguzi mkuu wa Januari mwaka huu, viongozi wa upinzani, wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari wamekumbwa na vitendo vya kutoweshwa, kukamatwa kiholela na mateso. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Bwana Türk ni kwamba ofisi hiyo imepokea taarifa zinazoonesha kuongezeka kwa ushiriki wa jeshi katika kutekeleza majukumu ambayo kwa kawaida hufanywa na taasisi za kiraia. Aidha, baadhi ya vyombo vya habari vimelazimika kusitisha shughuli zake kwa muda.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUSOROZA. ”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
-
70
Mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuingia ng’we nyingine kesho
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na upigaji kura usio rasmi kesho Alhamisi wenye lengo la kutathmini uungwaji mkono wa wagombea saba waliojitokeza kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Antonio Guterres anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Je ni nini kinafanyika? Assumpta Massoi amekuwa anafuatilia mchakato huu na nimezungumza naye angalau atupatie kwa muhtasari.
-
69
Tunawapatia huduma na twatumai wote watapona- Dkt. wa Ebola DRC
Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo ripoti zinasema watu zaidi ya 500 wamepona Ebola ya sasa. wanajamii ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Priscilla Lecomte aliyeko kwenye timu ya Mratibu Mkuu wa Ebola wa Umoja wa Mataifa, Julien Harneis, amezungumza na mmoja wa madaktari.
-
68
29 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunaangazia mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa UN, juhudi za mashirika mbalimbali za kuhamazisha wananchi DRC kuhusu udhibiti wa Ebola, na mafunzo ya STEM viziwani Zanzibar zinazolenga kuimarisha kilimo cha mwani..Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na upigaji kura usio rasmi kesho Alhamisi wenye lengo la kutathmini uungwaji mkono wa wagombea saba waliojitokeza kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Antonio Guterres anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Je ni nini kinafanyika? Assumpta Massoi amekuwa anafuatilia mchakato huu na nimezungumza naye angalau atupatie kwa muhtasari.Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo ripoti zinasema watu zaidi ya 500 wamepona Ebola ya sasa. wanajamii ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.Je, ingekuwaje kama kila kijana kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania angeweza kugeuza zao la mwani kuwa suluhisho la kiuchumi la kesho yake? Hilo ndilo lengo mradi wa shirika la kiraia la ProjeKt Inspire kupitia programu yake ya Girls in STEM, au Wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ufadhili wa Canada. Kupitia warsha wa siku tatu ya masomo ya STEM, wanafunzi wamejifunza kutumia masomo hayo kuongeza thamani ya zao la mwani na kuendeleza Uchumi wa buluu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
-
67
Mafunzo ya STEM yawezesha vijana Zanzibar kuongeza thamani ya zao la mwani
Je, ingekuwaje kama kila kijana kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania angeweza kugeuza zao la mwani kuwa suluhisho la kiuchumi la kesho yake? Hilo ndilo lengo mradi wa shirika la kiraia la ProjeKt Inspire kupitia programu yake ya Girls in STEM, au Wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ufadhili wa Canada. Kupitia warsha wa siku tatu ya masomo ya STEM, wanafunzi wamejifunza kutumia masomo hayo kuongeza thamani ya zao la mwani na kuendeleza Uchumi wa buluu. Feissal Kirwa na taarifa zaidi.
-
66
28 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Kuna msemo wa kiswahili usemao tahadhari kabla ya hatari na hivyo ndivyo ilivyo kwa ugonjwa wa Homa ya Ini ambapo kama mtu ataenda kufanya uchunguzi mapema anaweza kupata chanjo au matibabu, lakini kama atachelewa basi anaweza kupata hata ugonjwa wa saratani. Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya kuelimisha kuhusu ugonjwa huo Leah Mushi wa Idhaa hii amezungumza na Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na ini kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, nchini Tanzania Dkt. Swaleh Kitabu Pazi, mazungumzo yaliyofanikishwa na Evarist Mapesa Afisa Uhusiano kutoka Hospitali hiyo ya Muhimbili.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Leo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuongeza kwa kiwango kikubwa upimaji na matibabu ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi, likionya kuwa ugonjwa huo unaofahamika kwa lugha ya kiingereza na kitabibu kama Hepatitis unaweza kuua watu wengi zaidi kuliko malaria, kifua kikuu na Virusi Vya Ukimwi kwa pamoja kufikia mwaka 2040 ikiwa mwenendo wa sasa wa maambukizi utaendelea..Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi zote wanachama kuhuisha dhamira yao ya kutekeleza Mkataba wa Wakimbizi wa mwaka 1951, akisema haki ya watu wanaokimbia mateso kutafuta hifadhi inazidi kutiliwa shaka, kuwekewa vikwazo au kunyimwa.Na baada ya jana ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu UNODC kuonesha jinsi biashara ya utapeli mtandaoni inavyozidi kukua duniani, leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limefafanua zaidi kuwa nyuma ya biashara hiyo kuna maelfu ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu wanaolazimishwa kufanya uhalifu kwa vitisho na ukatili.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
-
65
27 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza simulizi za wananchi kuhusu uhamazishaji wa kudhibiti Ebola. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya mitadaoni ya fursa za ajira. Zaidi ya watu 300,000 wanakadiriwa kushikiliwa katika vituo vya ulaghai Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, ambako hunyang’anywa hati za kusafiria na kulazimishwa kufanya utapeli mtandaoni.Kamanda wa Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, Luteni Jenerali Ulisses De Mesquita Gomes, amethibitisha dhamira ya ujumbe huo ya kuimarisha usalama wa vituo vya afya katika eneo la Mongbwalu, jimboni Ituri, ambalo ni kitovu cha mlipuko wa Ebola. Amesema mashambulizi ya makundi yenye silaha na watu kuyakimbia makazi yao vinaweza kuvuruga ufuatiliaji wa wagonjwa na upatikanaji wa matibabu. Walinda amani wa Nepal wanaendelea kulinda raia na miundombinu ya afya, kwa kushirikiana na jeshi la Congo na mamlaka za eneo hilo.Na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya ajira mtandaoni. Zaidi ya watu 300,000 wanakadiriwa kushikiliwa katika vituo vya ulaghai Kusini-Mashariki mwa barani Asia, ambako hunyang’anywa pasipoti na kulazimishwa kufanya utapeli mtandaoni. UNODC inasema uhalifu huo sasa unasambaa hadi Afrika na maeneo mengine duniani, na kuwataka wanaotafuta ajira nje ya nchi kuthibitisha kampuni, mikataba na mawakala kabla ya kusafiri.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
-
64
24 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani kwa Maendeleo Endelevu awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Ofisi ya Rais inayohusika na Maendeleo ya Vijana, limeendelea kutumia mafunzo ya ufundi stadi kama njia ya kudumisha amani na kuwajengea uwezo vijana kiuchumi. Hii ni katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiwemo namba moja la kuondokana na umaskini na namba 16 linalolenga pamoja na mambo mengine kujenga amani kwenye jamii.Rashid Malekela, balozi kijana wa UNDP Tanzania alihudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake, UN Women, limeonya kuwa wanawake na wasichana katika mji wa El Obeid nchini Sudan sasa wanakabiliwa na hatari mbili wanapokwenda kuchota maji ambayo ni mashambulizi ya droni mchana yanawalazimu kusubiri hadi usiku, ambako hukumbana na ubakaji na ukatili mwingine wa kingono.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 130,000 nchini Burundi, wengi wao wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRc unaweza kusitishwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu endapo halitapata ufadhili wa haraka.Na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO, umefanikiwa kurejesha utulivu katika eneo la Nyakunde jimboni Ituri, hatua iliyowezesha kurejea kwa harakati dhidi ya ugonjwa wa Ebola.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
-
63
23 JULAI 2026
Mada kwa kina hii inakupeleka Pwani ya Kenya katika Kaunti ya Kilifi ambako mradi wa ‘Tushauriane Tuimarishe Kilimo Biashara’ unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, umewezesha wakulima wa eneo hilo kubadili mtazamo na kufanya kazi kwa pamoja. Ingawa changamoto za kijinsia zimekuwepo kwa muda mrefu, sasa mradi huo umefungua njia inayoleta nuru katika uhusiano wa kijinsia, mienendo ya kaya na matokeo ya kilimo biashara. Je nini kinafanyika? Feissal Kirwa kupitia video iliyoandaliwa na FAO anakusimulia zaidi.
-
62
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”
-
61
22 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Huko DRC madini ya kimkakati mashariki mwa nchi yamekuwa kichocheo cha mizozo. Mgeni wetu leo pamoja na mambo mengine anaangazia jinsi vita imezuia wao kuendelea na uchimbaji madini. Yeye anaishi Goma, lakini Salama Machaano, wa redio washirika wetu, Adventista World Radio, Tumaini Mkuu iliyoko Bukavu, jimboni Kivu Kusini alifnga safari hadi Goma kuzungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu “Utawala wa rasilimali za asili: Msingi wa amani, usalama na ustawi” chini ya kipengele cha ajenda ya “Kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao hicho ameeleza vipaumbele vinne kuwa ni kuhakikisha manufaa ya haki yanapatikana kutokana na rasilimali za asili, kuimarisha uwazi na ushirikiano ili kukabiliana na biashara haramu, kukuza utatuzi wa amani wa migogoro inayohusiana na rasilimali, na kuzingatia masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika kuzuia migogoro na kujenga amani.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetoa wito wa kulindwa kwa raia na kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji nchini Sudan baada ya shambulio lililotekelezwa juzi tarehe 20 Julai kwa kutumia ndege zisizo na rubani likilenga soko la Ar Rahad katika jimbo la Kordofan Kaskazini na kusababisha vifo vya watoto wawili na kuwajeruhi wengine sita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kusikitishwa sana na taarifa kwamba makumi ya wahamiaji wamefariki dunia au hawajulikani walipo kufuatia kuzama kwa meli katika pwani ya Mauritania, ambapo tarehe 18 Julai manusura 38 waliokolewa na Walinzi wa Pwani wa Mauritania karibu na mji wa Nouadhibou walipokuwa wakijaribu bahati yao kuelekea nchini Hispania. IOM kupitia Mkurugenzi wake wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Sylvia Ekra, imesema watu wanaendelea kuhatarisha maisha yao kwa sababu zinazowasukuma kuondoka katika nchi zao bado zipo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
-
60
21 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Jana katika moja ya viunga vya jiji la Nairobi, wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na raia wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Kenya, ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela walikitembelea Kituo cha Kulelea Watoto ya Yatima kinachofahamika kwa jina Serah’s Vision Children’s Home na walikaa kituoni hapo kwa dakika 67.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Ikiwa ni miezi tisa tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, hali ya usalama kwa raia wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel inaendelea kuzorota. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imesema hii leo kuwa hakuna eneo linaloweza kuchukuliwa kuwa salama kwa Wapalestina, huku Wizara ya Afya ya Palestina ikiripoti kuwa zaidi ya watu 1,100 wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel tangu Oktoba mwaka 2025.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limeonya kuhusu hatari ya safari za baharini kuelekea barani Ulaya kupitia bahari ya Atlantiki baada ya watu 144 kuripotiwa kufariki au kutoweka katika pwani ya Mauritania wiki iliyopita. Katika tukio la hivi karibuni watu 387 waliokolewa katika operesheni za uokoaji.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO linasema licha ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola wa virusi aina ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuendelea kuenea kwa kasi, baadhi ya maeneo yanaanza kuonesha dalili za hali kutengamaa kutokana na hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
-
59
20 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) yanatambua kuwa kuwawezesha vijana, kulinda mazingira na kuimarisha uhakika wa kupata chakula ni miongoni mwa nguzo muhimu za kujenga jamii zenye ustahimilivu na maendeleo endelevu. Kupitia malengo kama vile la Kutokomeza umaskini, kutokomeza njaa na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , jamii zinahimizwa kuwekeza katika suluhisho zinazowawezesha wananchi kujitegemea huku zikihifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Hatua hizo zinatekelezwa katika enoe la Kajiado Kaskazini, katika kaunti ya Kajiado, kusini mwa Kenya kama anavyosimulia Kelvin Keitany wa radio washirika, Domus Radio.Hii leo Umoja wa Mataifa umekuwa na matukio mbalimbali ya kuadhimisha siku ya Mandela, Rais wa kwanza mweusi wa taifa la Afrika Kusini kwa mchango wake wa utetezi wa haki. Miongoni mwa kulikofanyika maadhimisho hayo ni Nairobi, Kenya ambako Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa alikuwa shuhuda wetu. Licha ya idadi ya magari duniani kuongezeka kwa zaidi ya bilioni moja, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limesema vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimepungua kwa asilimia 21 kati ya mwaka 2011 na 2025. Hata hivyo, ajali hizo bado zilisababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1 mwaka jana na zinaendelea kuwa chanzo kikuu cha vifo kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 29Na, Je, msikilizaji wangu, uliwahi kujiuliza kwa nini binadamu bado wanarudi kuchunguza Mwezi ulioko anga za juu , zaidi ya miaka 50 baada ya kutua huko kwa mara ya kwanza? Leo Julai 20, dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya mwezi. Umoja wa Mataifa uliitenga siku hii kuenzi tukio la kihistoria la mwaka 1969, wakati wanaanga wa safari ya Apollo 11 walipoweka nyayo za kwanza za binadamu mwezini. Lakini maadhimisho haya hayaishii kwenye historia tu bali yanasisitiza pia umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika utafiti wa anga za juu na kuhakikisha uchunguzi wa mwezi unafanyika kwa amani na kwa manufaa ya watu wote duniani.".Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
-
58
Jifunze Kiswahili: Maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."
-
57
17 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu António Guterres aliyeko ziarani nchini China amehutubia mdahalo kuhusu Tahadhari za Mapema kwa Wote katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika kwenye jukwaa la kimataifa la Akili Mnemba na Tabianchi jijini Shanghai na kutoa wito wa kuharakisha maendeleo ya mifumo ya tahadhari za mapema inayotumia akili mnemba ili kuzuia majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo amesema "tahadhari lazima zifikie kila mtu aliyeko hatarini kwa lugha wanazoelewa na mifumo ya mawasiliano wanayoweza kuiamini."Kesho Julai 18 ikiwa ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, huko Geneva, Uswisi hii leo mashindano ya 18 ya Nelson Mandela ya Mahakama ya Kimataifa ya Kuigiza yamefikia kilele kwa timu ya Chuo Kikuu cha Midlands State kutoka Zimbabwe kuibuka mshindi ilihali Chuo Kikuu cha Strathmore kutoka Kenya kimeshika nafasi ya pili.Hii leo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na marafiki wa mpira wa miguu au kabumbu, wamezindua kampeni ya mwaka mmoja ya Dunia Moja, Mchezo Mmoja, Lengo Moja kwa lengo la kutumia mpira wa miguu kama kichochea cha kuimarisha afya ya akili kwa vijana, tukio linalofanyika siku mbili kabla ya fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanaume. Akizungumza mapema kabla ya tukio hilo Sahira Al Nahari, ambaye ni Kiongozi kijana mchechemuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs amesema, "kwa hiyo, mpira wa miguu una mengi ya kutufundisha. Tunapokabiliwa na janga la kimataifa, hebu tuzielekeze fikra zetu kwenye viwanja vya mpira wa miguu. Tunapotazama kinachotokea viwanjani, tunajifunza nidhamu, ustahimilivu, na jinsi ya kuinuka tena baada ya kupoteza jambo muhimu sana."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
-
56
16 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Ukanda wa Gaza ambako sitisho la mapigano kati ya Israeli na Palestina lililotiwa Saini tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2025 limewezesha wakulima wa eneo hilo kurejea mashambani. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Mashirika mawili ya Umoja Umoja wa Mataifa lile la Uhamiaji, IOM na la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa waliyoitoa kwa pamoja jijini Gneva Uswusi na BangKok Thailand, wameeleza wasiwasi mkubwa kufuatia taarifa kwamba boti mbili zilizokuwa zimebeba zaidi ya watu 500 huenda zimezama katika pwani ya Myanmar katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa za awali, boti hizo mbili ziliondoka mwishoni mwa mwezi Juni kutoka Jimbo la Rakhine nchini Myanmar zikiwa zimewabeba zaidi ya abiria wa jamii ya Rohingya, wakiwemo baadhi waliokuwa wametoka katika kambi za wakimbizi za Cox's Bazar nchini Bangladesh.Zaidi ya watoto milioni 23 wengine zaidi ya wale ambao wako tayari kwenye umaskini duniani wanaweza kutumbukia katika umaskini wa kipato ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2025 kutokana na kuendelea kwa mzozo wa Mashariki ya Kati na athari zake kwa biashara ya kimataifa, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) jijini New York, Marekani.Na Uganda leo imeanza rasmi kuhesabu siku 42 kuelekea kutangazwa kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola baada ya mgonjwa wa mwisho aliyethibitishwa kuwa na maambukizi kupimwa mara ya pili na kubainika hana virusi hivyo, kisha kuruhusiwa kutoka hospitalini. Hatua hiyo ni mafanikio muhimu katika juhudi za nchi hiyo kudhibiti mlipuko, imesema taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO ofisi ya Uganda.Mwenyeji wako ni Feissal, karibu!
-
55
15 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana tunamulika jinsi gani vijana waliojiendeleza katika stadi ya akili mnemba au wengine wanaita akili unde, kwa kiingereza Artificial Intelligence au AI, wanarahisisha maisha ya jamii. Na tunamuangazia kijana Kalebu Gwalugano kutoka Tanzania, Muasisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Neurotech iliyoanzishwa mwaka 2022. Kijana huyu ni Mhandisi wa AI na akiwa Dar Es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki, amezungumza na mwenzetu Japhael Jambo. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Stadi za Vijana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema kuwezesha vijana kufikia uwezo wao kamili kunahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu na mafunzo jumuishi yenye ubora. Ametambua mchango wa vijana kote duniani kwamba wanaendelea kutoa mchango mkubwa kama wabunifu, viongozi na mawakala wa mabadiliko katika kujenga jamii zenye usawa, ustahimilivu na maendeleo endelevu hata hivyo mabadiliko ambayo dunia inapitia sasa yakichochewa na maendeleo ya teknolojia za kidijitali, athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika wa kiuchumi na pengo la usawa yanahitaji vijana kuwa na ujuzi mpya unaowawezesha kushindana na kunufaika na fursa zinazojitokeza.Ingawa mwaka 2025 duniani kiwango cha chanjo kwa watoto kiliongezeka kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, kiwango cha chanjo bado kiko asilimia moja chini ya kiwango cha mwaka 2019, kikiwa kimeendelea kubaki ndani ya kiwango finyu tangu mwaka 2009. Hayo ni kwa mujibu wa makadirio ya kila mwaka ya mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO na la kuhudumia watoto, UNICEF kuhusu viwango vya kitaifa vya chanjo.Na ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR inazitaka pande zinazohusika katika vita nchini Sudan, pamoja na serikali na kampuni zinazofanya biashara ya Gum Arabic, gundi inayotokana na aina fulani ya miti ya Acacia kuhakikisha shughuli zao zinaendana na sheria za kimataifa na hazichangii kuendeleza mzozo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
-
54
14 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu ya UN kumsikia Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake. Baada ya ziara yake mjini Bunia, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO anayehusika na Programu ya Dharura za Afya, Dkt. Chikwe Ihekweazu, amewambia waandishi wa habari Geneva, Uswisi kwamba mlipuko wa sasa ni moto ambao kinachouchochea kiko katikati, huku ukiendelea kusambaa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari (IMO) limesema lina wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulizi ya jana usiku yaliyolenga meli kwenye mlango wa bahari wa Hormuz na viunga vyake na kusababisha vifo vya takribani mabaharia wawili na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kupitia taarifa yake iliyotolewa London, Uingereza, IMO imesema inafanya kazi kwa haraka na mamlaka husika ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo.Na uungwaji mkono wa umma kwa wakimbizi unaendelea kuwa imara licha ya kuwepo kwa changamoto na kutokuweko kwa uhakika wa mustakabali duniani, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa pamoja uliofanywa na kampuni ya IPSOS na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Utafiti umebaini kuwa asilimia 66 ya washiriki katika nchi 29 wanakubaliana kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kuruhusiwa kusaka hifadhi katika nchi nyingine, ikiwa ni punguzo la asilimia moja tu ikilinganishwa na mwaka 2025.Utafiti huu umefanywa ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa Mkatab awa Kimataifa wa kulinda wakimbizi.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
-
53
Uhaba wa maji watishia mafanikio ya SDGs – Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
-
52
IMO yatetea uhuru wa usafiri wa majini, sheria za kimataifa na usalama wa mabaharia
Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Anold Kayanda ameifuatilia taarifa hiyo.
-
51
13 JULAI 2026
Hii leo jaridani tunaangazia malengo ya maendeleo endelevu, uhuru wa usafiri katika maji, na shughuli za Redio Miraya za kutumia redio kujenga amani na kutoa tahadhari za mapema za hali ya hewa nchini Sudan Kusini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi.Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Nchini Sudan Kusini, Redio ndiyo chanzo kikuu cha taarifa kwa takribani asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ndiyo maana kuendelea kwa matangazo ya Radio Miraya ambayo yamedumu kwa miaka ishiriki katika redio hii inayomilikiwa na UNMISS yaani Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani Sudan Kusini ni kipaumbele cha juu katika juhudi zake za kuzuia migogoro na kujenga amani.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
No topics indexed yet for this podcast.
Loading reviews...
Loading similar podcasts...