06 JULAI 2026 episode artwork

EPISODE · Jul 6, 2026 · 9 MIN

06 JULAI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendelo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo limeendesha midahalo ya amani na utatuzi wa migogoro kwa vijana, lengo, ni kuimarisha amani kwa Maendeleo Endelevu.Siku nne tu baada ya shambulio kubwa la Urusi dhidi ya Ukraine, usiku wa kuamkia leo kwa saa za Ukraine wakazi wa Mji Mkuu, Kyiv kwa mara nyingine tena wamekumbana  mashambulizi yaliyofanywa na Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Matthias Schmale, amesisitiza akisema, "haiwezi kurudiwa mara nyingi vya kutosha kwamba sheria za kimataifa za kibinadamu zinataka hatua zote zinazowezekana zichukuliwe ili kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia." Mbali na mji mkuu, mwishoni mwa wiki mashambulizi ya mabomu katika mji wa Sumy yaliwaua raia kadhaa na kuwajeruhi makumi ya wengine, wakiwemo watoto. Miji mingine kama Dnipro, Kherson, Kyiv, Zaporizhzhia na mingine pia ilikumbwa na vifo na majeruhi wengi miongoni mwa raia pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia, hali iliyokatiza upatikanaji wa huduma za msingiHakuna dawa au mwanasesere anayefikia mtoto bila kufanyiwa kwanza uchunguzi au majaribio ya kina kuthibitishwa ni salama, lakini akili mnemba au AI imefikia watoto kupitia kusoma, urafiki au maswali binafsi ya msingi bila hata mtu mmoja kujiuliza athari mbaya za mfumo huo kwa watoto, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa siku mbili kuhusu usimamizi wa akili mnemba ulioanza leo huko Geneva, Uswisi. Hivyo amesema, “hakuna mtoto anayepaswa kugeuzwa majaribio ya akili mnemba isiyodhibitiwa. Kwa kuendeleza kazi inayofanywa na Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na wadau wengine, leo ninatoa wito wa kupitishwa kwa Ahadi ya Usalama wa Watoto katika Matumizi ya akili mnemba, yenye kanuni tatu rahisi kwa mfumo wowote wa AI unaoweza kufikiwa na watoto.”.Na taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) iliyotolewa leo jijini London nchini Uingereza imemnukuu Katibu Mkuu wa shirika hilo, Arsenio Dominguez, akitoa wito wa hatua za haraka za kimataifa kuhakikisha mabaharia hao wanaachiliwa haraka na wakiwa salama. Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) iliyotolewa leo jijini London nchini Uingereza imemnukuu Katibu Mkuu wa shirika hilo, Arsenio Dominguez, akitoa wito wa hatua za haraka za kimataifa kuhakikisha mabaharia hao wanaachiliwa haraka na wakiwa salamaMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jul 6, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

06 JULAI 2026

0:00 9:58

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on July 6, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!