EPISODE · Mar 13, 2026 · 9 MIN
13 MACHI 2026
from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ujumbe wa kijana kutoka Uganda anayehudhuria mkutano wa CSW70, na mradi wa intaneti kwa wanafunzi nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mateso yanayowakabili wananchi wa taifa hilo la Mashariki ya Kati lililotumbukizwa kwenye vita isiyowahusu.Mikutano hii inayokutanisha Umoja wa Mataifa watetezi wa haki za wanawake dunia inawapa ujasiri vijana wa kuona kuwa nao wana uwezo na fursa ya kusaka majawabu katika jamii zao. Ni kauli ya kijana wa kike kutoka nchini Uganda anayeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani (CSW70 ) unaoendelea hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Maelfu ya wanafunzi katika eneo la Kajiado nchini Kenya wameanza kunufaika na mradi wa kusambaza intaneti shuleni uitwao ‘Last Mile Connectivity’. Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa kidijitali na matokeo ya masomo kwa wanafunzi ili kuwaandaa na maisha ya baadaye, huku shule 1,000 zikitarajiwa kufikiwa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
What this episode covers

NOW PLAYING
13 MACHI 2026
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.