17 MACHI 2026 episode artwork

EPISODE · Mar 17, 2026 · 9 MIN

17 MACHI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha CSW70. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka DRC.Nelly ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaeleza kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka, mathalan huko Lebanon watu 816,000 sawa na asilimia 14 ya watu wote wamekimbia makazi yao. Na huko Iran watu milioni 3.2 wanakadiriwa kukimbilia maeneo ya Kaskazini mwa taifa hilo na vijijini wakikimbia machafuko. Namba ya dharura ya msaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UHCHR inapokea zaidi ya simu 1,000 kwa siku za watu wakiomba msaada.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya kuwa njaa duniani inaweza kufikia viwango vya juu mwaka huu iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea na bei ya mafuta itabaki kuwa juu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Carl Skau amesema “Ongezeko la gharama za chakula na mafuta duniani zinaweza kuacha mamilioni ya familia zikiwa nje ya uwezo wa kununua vyakula, hasa katika nchi zinazotegemea uagizaji bidhaa kama vile Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia. Kwa hakika, uchambuzi wetu unakadiria kwamba, kama mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea hadi mwezi Juni, watu zaidi ya milioni 45 wanaweza kuingizwa kwenye njaa kali kutokana na bei kuwa juu na hii itaweka rekodi ya juu ya njaa duniani kote. Na haya ni matarajio mabaya.".Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo moja ya matukio ya kando ya Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 ni Kushughulikia vikwazo vya haki ya kijinsia kupitia mfumo wa Mahakama ya Mtandao nchini Tanzania kwa lengo la kufanikisha haki kwa wanawake na wasichana. Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania anasema mashinani mfumo unatumia simu zisizo janja na akisema mobile app ni apu ya kwenye simu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Mar 17, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

17 MACHI 2026

0:00 9:59

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on March 17, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!