25 JUNI 2026 episode artwork

EPISODE · Jun 25, 2026 · 9 MIN

25 JUNI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Feissal Kirwa

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunaelekea nchini DRC, kwa Lydie Mwenge, Mwanaharakati wa kupigania haki hususan za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 walioathirika na vita inayoendelea nchini humo ukiwemo ukatili wa kingono.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea na harakati za kutoa msaada wa dharura kwa Venezuela kufuatia matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyolikumba taifa hilo jana Jumatano Juni 24, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 164 pamoja na uharibifu mkubwa katika mji mkuu, Caracas, na maeneo ya jirani. Matetemeko hayo mawili yenye ukubwa wa 7.2 na 7.5 katika kipimo cha Richter yametokea ndani ya muda wa chini ya dakika moja, yakiharibu nyumba, hospitali, barabara na miundombinu mingine muhimu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa kuimarishwa kwa ulinzi wa mabaharia duniani, akionya kuwa ongezeko la migogoro na mivutano ya kisiasa linaweka maelfu ya wafanyakazi wa baharini katika hatari wakati wakiendelea kuhakikisha biashara na usafirishaji wa bidhaa duniani vinaendelea. Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mabaharia, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Juni, Katibu Mkuu amesema karibu asilimia 90 ya bidhaa na mahitaji muhimu duniani, ikiwemo chakula, dawa na nishati, husafirishwa kwa njia ya bahari.Na maandalizi ya Mkutano wa 15 wa Afrika Kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, AfIGF utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Ghana yameanza ambapo maoni ya wadau yatakusanywa ili kuweka mazingira salama ya matumizi ya intaneti barani Afrika na hatimaye duniani. Vijana na watoto kutoka nchi mbalimbali wamekutana jijini Nairobi Kenya kuandaa mawazo yao na mmoja wao ni Sheryl Christine Adhiambo kutoka taasisi ya Legal Sisters ya nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

NOW PLAYING

25 JUNI 2026

0:00 9:58

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Et Merdre ! Martin Poirot Et Merdre ! Votre émission vivante consacrée aux spectacles du même genre !Découverte des coulisses de toute les formes de créations artistiques du spectacle vivant : mise en scène, scénographie, jeu, écriture, expositions... Dans chaque émission retrouvez un artiste, un spectacle, un lieu, ou un festival. Aussi disponible en vidéo sur YouTubeUne émission animée par Martin PoirotRéalisée par Zachary GuerenneurIllustrée par Carole MarietHébergé par Ausha. Visitez ausha.co/fr/politique-de-confidentialite pour plus d'informations. Zero Așteptări Paul Puscas Podcastul nostru, este un refugiu de pace și introspecție în tumultul cotidian și în mijlocul așteptărilor adesea nerealiste ale societății. Ne-am dedicat acest spațiu digital pentru a oferi o platformă celor care doresc să exploreze diverse perspective și să participe la discuții deschise, autentice, fără prejudecăți sau anticipații predeterminate. Fiecare episod pe care îl lansăm este o invitație la reflecție și explorare personală, acoperind o gamă largă de subiecte, de la dezvoltare personală și spiritualitate, la cultură, artă și știință, prezentate întotdeauna într-o manieră acc Temps de Dol Temps de Dol Soy 1 de 4. Lo he sido dos veces. Aquí te traigo mi tiempo de duelo para que, si también estás transitando un proceso de duelo gestacional sepas que no estás sola. Hablemos. Escuchemos. Visibilicemos. Y, sobretodo, acompañemos. Podcast de Leyendo Ciencia Ficción Leyendo Ciencia Ficción Un podcast sobre literatura de ciencia ficción de cualquier época.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on June 25, 2026.

What is this episode about?

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunaelekea nchini DRC, kwa Lydie Mwenge, Mwanaharakati wa kupigania haki hususan za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 walioathirika na vita inayoendelea nchini humo ukiwemo ukatili wa...

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes, you can download this episode by clicking the download button on the episode player, or subscribe to the podcast in your preferred podcast app for automatic downloads.
URL copied to clipboard!