Ep. 19 - Salama Na Monalisa | MASHHURA episode artwork

EPISODE · Jun 4, 2020 · 1H

Ep. 19 - Salama Na Monalisa | MASHHURA

from Salama Na · host Salama Na

Kabla sijasema jinsi ambavyo nampenda na kumheshimu mgeni wetu wa wiki hii napenda kusema cha kwanza ambacho nilikipenda kwake kwanza ilikua jina lake, Ms Yvonne Cherrie kisha Monalisa. Rafiki mzuri, mstaarabu na mtu mwema sana. Mona pia ana bahati sana, bahati ya kuwa na Mama ambaye ni hodari na mcheshi ambaye nae alifanya kazi yake ya kuhakikisha bintiye kwanza anafanya yote anayostahili kufanya kama mtoto kabla haja mshika mwanaye mkono na kumtambulisha kwenye dunia ya sanaa ambayo ilitufanya tumtambue na kumpenda pia na pia kuwakubali zaidi kama Mama na mtoto ambao ni mahodari sana. Kwenye kikao chetu hiki ambacho kilifanyika wakati Corona imependa moto na ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan Mona hakutusumbua kabisa, alitaka tu kupata uhakika wa usalama eneo la tukio na alikua pale on time kabisa, na pengine sisi inawezekana tulimsumbua kwa kutopokea simu kwa wakati. Mimi na Monalisa tunajuana kitambo kiasi so mazungumzo yetu yalianzia siku zile tulipokua tunaonana karibia kila siku, enzi za utoto wetu. Yeye alikua msanii hodari lakini pia alikua mmoja ya watangazaji mahiri kabisa wa Radio One na hata ITV. Enzi za kuwa ukurasa wa mbele wa magazeti ya udaku karibia kila Ijumaa na Jumatatu. Tulianzia hapo. Sote tunajua alipitia mambo meeeengi sana maskini ya Mungu, kuanzia maisha hayo ya umaarufu wa kuuza gazeti, mahusiano yake na Marehemu Meddy Mpakanjia na Amina Chifupa. Sanaa yake ya awali, ndoa yake na Marehemu George Tyson. Watoto wake, mahusiano yake na Mama yake, elimu, kazi na Sanaa kwa ujumla. Nilikua na wakati mzuri sana wakati tunarekodi hii na yangu matumaini pia uta enjoy. Love, Salama. Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jun 4, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 19 - Salama Na Monalisa | MASHHURA

0:00 1:00:48

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 0 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on June 4, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!