Ep. 2 - Salama Na Marco Chali | DOKTA episode artwork

EPISODE · Feb 9, 2020 · 1H 3M

Ep. 2 - Salama Na Marco Chali | DOKTA

from Salama Na · host Salama Na

DOKTA Marco na mimi tumekua marafiki wa miaka mingi na moja kati ya vitu vimetufanya tuwe marafiki ni kufanana kwetu kwa kupenda vitu vya aina moja. Kuanzia teknolojia mpaka muziki, nakumbuka siku ya kwanza kukutana naye, ilikua ni uzinduzi wa kipindi cha Bongo Star Search ambao ulifanyika Much More pale juu, alinifuata akaniambia juu ya mapenzi yake ya kipindi changu cha Planet Bongo enzi hizo na baada ya hapo ikawa ni urafiki ulodumu mpaka leo. Kipindi changu cha Mkasi kilizaliwa kwenye kibaraza cha studio kwa Marco Chali pale MJ RECORDS ambako ilikua ni maskani yetu kubwa mimi na AY. Marco anajua KILA KITU, kuanzia kuendesha baskeli, kutengeneza mabiti, kuandika, kuimba, kuogelea,kucheza basketball kupambana na maisha na ni mwingi wa Imani pia. Amekua akijinyima karibu kila siku ilimradi watu anaowapenda wapate chochote, zaidi kwa familia yake. Katika watu ambao naweza kuwapigia simu nikawaambia sina kitu Marco ni mmoja wapo na anaweza akawa nae ni vivo hiyo ila akanipa mimi na yeye akaenda kutafuta nyengine. Mwaka jana rafiki yangu Mwenyezi Mungu alimbariki mtoto wake wa kwanza, binti, anaitwa Yoy, tabasamu ambalo rafiki yangu analo sikuwahi kuliona likiwa endelevu kama ambavyo toka Yoy amekuja duniani… Mwenyezi Mungu amlindie na amkuzie kwenye misingi iliyo bora na afya njema. Kwenye kikao chetu hiki ingekua inawezekana tungeweza kuongea hata masaa 24, yeah, story zetu zinaweza kufika huko, na siku nyengine tunaweza hata tusiongee kabisa, ikawa mikausho mikali tu ila humu tulipata wasaa wa kumuongelea Yoy, muziki, career yake, Mwenyezi Mungu, Godzilla, mawazo na discipline. Yangu matumaini utapata kadhaa ya kujifunza na kukusogeza. Love, Salama.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Feb 9, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 2 - Salama Na Marco Chali | DOKTA

0:00 1:03:54

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 3 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on February 9, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!