Ep. 20 - Salama Na Lord Eyes | HAWATUWEZI episode artwork

EPISODE · Jun 11, 2020 · 53 MIN

Ep. 20 - Salama Na Lord Eyes | HAWATUWEZI

from Salama Na · host Salama Na

Isaac ndo jinsi jina lake linavyoandikwa, kipaji adhimu kabisa kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Allah kamjaalia kila ambalo msanii anaomba abarikiwe nalo wakati anapewa kipaji. Mrefu, muonekano mzuri, mashairi ya kibabe na kujiamini kulikokaa sehemu yake haswa. Walipoanza kama kundi hapo ndo attention yangu waliipata wana Nako 2 Nako Soldiers kutoka Ara, kila kitu kilikua tofauti juu yao, mavazi, style, matamshi na hata muonekano. Hii ilikua chachu ya kuwafikisha popote ambapo walikua wamepalenga. Mashabiki kila kona ya Tanzania na Afrika na dunia kwa ujumla, hakuna radio utakayoskilizia ambayo walikua hawapati nafasi. Walikua marafiki wa kila kituo na kazi yao waliifanya vizuri haswa. Nia ya mazungumzo haya ilikua ni ku catch up na rafiki yangu Isaac aka Lord Eyes aka Lodii. Kiasi cha heshima nilichokua nacho juu yake ni cha hali ya juu, uwezo wake wa kufanya kazi aliyopewa kipaji na Jalali ni wa kipekee. So nini kilienda kombo haswa kwa baadhi ya wanachama katika kundi lake na kwake yeye binafsi? Niamini haikua kazi rahisi kuweza kupata ujasiri wa kutaka kuyajua yote. Ni ngumu wakati mwingi kumuuliza mtu kuhusu struggle zake ambazo bado anapigana nazo na hii haijalishi hata kama mmezoeana kiasi gani. Lodii alikua hana cha kujificha, hana kinyongo wala hana kisasi na mtu yoyote, kubwa analolifanya ni kuwa bora one day at a time na kuelekea kwenye sehemu salama anayotaka kufika. So nini haswa kilitokea kwa Wanako? Na yeye alijikutaje kazama kwenye dimwi na madawa na maisha ambayo alikua hayataki? Siku ya kwanza kuonja ilikua lini? Na je ni lini alikua ana tatizo na akaanza kulifanyia kazi? Wazazi wake? Ana mtoto au watoto? Ni mapenzi yakimfikisha huko? Au marafiki? Au maisha? Na pia aliwezaje kutoka huko? Lini aliona haswa kama imetosha na basi aanze kujikomboa? Kusema za ukweli story ni ndefu ila tulipata wa kutusimulia na yangu matumaini kuna mambo mawili matatu utajifunza juu ya maisha, umaarufu, marafiki na maamuzi ambayo unaweza ukafanya. Tafadhali enjoy. Love, Salama Follow:  Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jun 11, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 20 - Salama Na Lord Eyes | HAWATUWEZI

0:00 53:46

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 53 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on June 11, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!