Ep. 21 - Salama Na Baraka | FAHARI TOKA ITETE episode artwork

EPISODE · Jun 18, 2020 · 1H 29M

Ep. 21 - Salama Na Baraka | FAHARI TOKA ITETE

from Salama Na · host Salama Na

Mimi ni kama wewe tu juu ya ufahamu wa huyu mtu ambaye ameibeba Itete iliyopo kata ya Isuto tarafa ya Isangati, wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla, jina ni Baraka Adson Mpenja. Wengi humuita sauti ya radi, utamshi wake wa maneno na majina ya wachezaji na viongozi ni wa namna ya kipekee haswa, na bila ya shaka hiyo ndo tofauti kuuubwa kabisa kati yake yeye na watangazaji wengine wa kabumbu ikiwa pamoja na mimi hapa Tanzania. Ni kijana na ni maridadi na pia hajasahau wapi ametoka na ndoto zake ndo hizi ananoziishi sasa kwa mujibu wa maongezi yetu haya. Umaarufu wake si wa kulazimisha wala si wa skendo, kazi yake maridadi aifanyayo kwa ustadi wa hali ya juu ndo imemtambulisha kwetu hapa nyumbani na kanda nyengine za Afrika ambapo king’amuzi cha Azam kinafika. Burudani ambayo anaitoa huku akipeperusha umaarufu wa ligi kuu ya Tanzania bara na mashindano ya kimataifa ni ya mfano wa kuufuata hasa. Yangu hakika katika sajili bora ambazo AzamTV walishawahi kufanya basi ya Baraka Adson Mpenja inaweza ikawa ya kuokota dodo chini ya Mvinje. Basi umaridadi wake huo ndo ulotusukuma haswa sisi kumuita kwenye meza yetu, na akaja bila ya kusita. Tuliongea kuhusu chimbuko lake, ndoto zake jinsi anavyojifunza kila siku kutoka kwa wazoefu walomzunguka, masomo, ndoa, maisha kwa ujumla na mapenzi yake kwa mpira wa miguu. Ilikua matani na ung’amuzi mwingi wakati naongea naye na yangu matumaini uta enjoy. Love, Salama. Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jun 18, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 21 - Salama Na Baraka | FAHARI TOKA ITETE

0:00 1:29:08

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 29 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on June 18, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!