Ep. 32 - Salama Na Riyama | UTAKWENDA UTARUDI episode artwork

EPISODE · Sep 3, 2020 · 1H 15M

Ep. 32 - Salama Na Riyama | UTAKWENDA UTARUDI

from Salama Na · host Salama Na

Riyama Seleman Ally, malkia wa kazi aifanyayo na kila alitilialo msisitizo hulifanya kwa asilimia 100, hata kama akichelewa kama pengine alivyochelewa kupata heshima yake na malipo yake anayostahili, kama ambavyo anapata sasa au ambayo anapata maana safari bado ni ndefu. Na kwa mazungumzo haya nilofanya naye huo ndo muelekeo na ndo nia na madhumuni. Sote tunajua PENYE NIA PANA NJIA, so kazi ni kwetu. Mzaliwa wa Unguja Tanzania, kakua katika familia ya kidini na malezi bora ila kwa mujibu wa maongezi yetu haya yeye alipenda zaidi kuwa muimbaji, kitu ambacho Mwenyezi Mungu mtoa vipaji hakumjaalia kipaji hicho na uzuri ni kwamba aligundua mapema na akafanya ustaarabu wa kutafuta kitu chengine cha kusogeza maisha yake. Ule usemi wa Mungu anakupa unachostahili na sio unachotaka hapa umetulia mahala pake. Imagine kutoka kutaka kulazimisha kuwa Khadija Kopa (ndo muimbaji anayempenda zaidi) na kuwa mmoja wa wasanii wa filamu hodaaari kabisa hapa kwetu na kama SI NDIO MUIGIJAZI BORA WA KIKE WA FILAMU hapa Tanzania. Heshima zangu za dhati zinaenda kwake kwa kukubali kuja kuongea nami na kunielezea kinaga ubaga juu ya ukuaji wake, maamuzi fulani fulani ambayo ashawahi kufanya maishani mwake. Elimu yake, alisoma? Shule ipi? Alikua mwanafunzi wa aina gani? Kuhusu familia? Ana mtoto? Na pia tulizungumzia filamu na maisha yake kama kioo cha jamii. Majibu yalikua mazuri na marefu na kwa hilo namshkuru sana yeye kwa kuweza kuja na kuongea nami huku mume wake mpendwa akiwa anamgojea kwenye parking lot. Yangu matumaini uta enjoy maongezi haya kama nami nilivyo enjoy kuongea naye. Love, Salama.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 3, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 32 - Salama Na Riyama | UTAKWENDA UTARUDI

0:00 1:15:02

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 15 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on September 3, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!