Ep. 33 - Salama Na SPESHOZ | BOBBIN episode artwork

EPISODE · Sep 10, 2020 · 1H 23M

Ep. 33 - Salama Na SPESHOZ | BOBBIN

from Salama Na · host Salama Na

Jeffrey Jessey Mmbungu ni kijana wa ki Tanzania ambaye aliangaliaaa wapi pa kupata rizki ili mambo yake yamuendee kama anavyopenda na akafanikiwa kwa asilimia nyingi sana huku akipata pointi nyingi za kujiamini na kuthubutu kutoka kwangu. Ni rafiki yangu kwa miaka zaidi ya minne sasa, tunagombana tunapatana, kisha tunagombana tena alafu tunapatana, kisha tunagombana kwasababu ya Manchester United alafu tunapatana tena kabla hatujagombana tena kwasababu ya suit yangu kutotobolewa mashimo ya vifungo vya pembeni ya suruali yangu, au pengine kwasababu nlikua nataka kumpiga kirungu akachomoa, au pengine simu yake haipatikani kiiiila wakati wakati yeye ni mtu ambaye hatakiwi simu yake iwe na mizinguo hiyo, ilimradi ni vita tu kati yetu. Najua hili lakini, kwamba wagombanao ndo wapendanao, kiasi cha heshima na kumuamini na kumu admire ni cha hali ya juu sana. Kuna habari zilienea kipindi flani kuhusu maamuzi yake ya kuacha kazi benki ya dunia na kuamua kujiajiri, na kwamba ni mtoto wa kishua ila anajitia umaskini ili apate huruma kutoka kwa watu na yake yamuendee. Shutuma nzito haswa kwa upande wake. Kwenye kipindi hiki nadhani hatukuacha kitu, yote yalipewa ufafanuzi na pia tukapewa elimu ya yale tusoyajua ambayo ki ukweli tulikua tunajifanya tunayajua sana. Kuanzia hilo suala la kazi mpaka alivyokutana na Cecilia Mosha aka Ceci kama ambayo Jeff humuita. Wana watoto wawili wa kiume ambao wote wamepewa majina ya wachezaji wa zamani wa Manchester United, na ndoto yake ni kuwa vijana wake hao waje kuwa wachezaji wa mpira, niko hapa kuzidisha maombi hayo ili dua za Baba zitimie nami kama shangazi niweze kwenda kukaa kwenye ‘private box’ za Wembley au OT kuangalia vijana wetu wakilisakata gozi So biashara wake aliingiaje huko? Na kweli alijiona akitoa ajira kwa watu zaidi ya hamsini ambao wako chini yake? Mitihani gani haswa hupata? Yeye kama yeye ana thamani ya kiasi gani? Pesa ngapi huwa anatengeneza kwenye kazi yake hii? Kuna changamoto? Nani mteja wake mkuu? Mahusiano yake na Diamond Platnumz? Walikutana wapi? Huwa Platnumz analipia nguo zake zinazotoka kwa Jeff? Ana biashara nyengine anazofanya? Na elimu yake je? Wapi alienda skuli? Alisomea nini? Kusema za ukweli maswali ni mengi ila tuli pata wa kumuuliza maana alinyoosha vizuri na nilicheka sana na ku enjoy haswa. Yangu matumaini nawe pia utafanya hivyo. Kuna ya kujifunza mengi hapa, ya kukupa muangazo pia yanapatikana humu kwa wingi. Tafadhali enjoy. Love, Salama.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 10, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 33 - Salama Na SPESHOZ | BOBBIN

0:00 1:23:36

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 23 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on September 10, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!