Ep. 4 - Salama Na Barnaba | FUNDI episode artwork

EPISODE · Feb 23, 2020 · 1H 3M

Ep. 4 - Salama Na Barnaba | FUNDI

from Salama Na · host Salama Na

Barnaba ni mfupi (siko hapa kumtoa kasoro) ila wazungu wana usemi wao ambao nitausema kwa kiswahili, ya kwamba vitu vizuuuri huja kwenye pakeji ndogo. Ukitaka kuelewa maana yake kama hujang’amua basi kamuulize Bibi. Umbo lake na uwezo havifanani , na kama ingekua ubora na kipaji ndo ukubwa wa mwili basi mwenzetu angekua kama HERCULES, pia siko hapa kwaajili ya kumtukuza bali kusema vile nimunavyo katika macho yangu. Ni kijana ambaye anajifunza kila siku iendayo kwa Mungu, hajawahi kujikweza, mwenye roho ya Imani, mwenye kumuogopa Mungu na pia asiyesahau alipotoka na pia alotoka nao huko alipotoka. Mtanashati pia, na ukiniuliza mimi naamini kabisa hiki ni kitu ambacho kimekua kikistawi kwa siku zinavyokwenda, na huo ndo ukuaji, maana kukua si nywele na kucha tu, hata kujielewa na kufahamu kwamba nyanya pia ni tunda lakini juisi yake mpemba hauzi pia ni ukuaji. Muziki ndo mpenzi wake wa kwanza, ambao umemuepusha na mengi na kumpa vingi pia na kumkutanisha na watu ambao pengine alikua anawaona kwenye picha tu, kuufahamu kwake mziki kwa kujifunza kupiga gitaa na kuutengeneza kama muandaaji na pia kuweza kuuandika ni kipaji ambacho Jalali kampatia, na jinsi ambavyo si mchoyo wa kuwapa na wenzie wakang’ara (kitu ambacho alijifunza) ndo ambacho pia kinampa utofauti kati yake na wengine wengi. Kwenye kikao hiki mimi naye tulianzia nyuma kiasi, enzi za kuokota vyuma chakavu ili mambo yaende, kupigiwa kelele ya mwizi na kuponea chupuchupu kuchezea kibiriti, THT, uandishi, heshima, Marehemu Ruge, maisha ya ndoa, social media na mengine ya kutosha. Ilikua siku ya kujifunza mengi kutoka kwake na kwa hilo namshkuru Mungu kwa kunikutanisha nae. Tafadhali Enjoy. Love, Salama

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Feb 23, 2020

Embed this episode

Ready to play

Ep. 4 - Salama Na Barnaba | FUNDI

0:00 1:03:54

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 3 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on February 23, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!