Ep. 5 - Salama Na Shilole | MAMA episode artwork

EPISODE · Mar 1, 2020 · 1H 11M

Ep. 5 - Salama Na Shilole | MAMA

from Salama Na · host Salama Na

Zuwena Yusuf Mohammed ndo jina alopewa na wazazi wake na siko hapa kuwakosoa kwa chaguo lao hilo ila mi nadhani Shilole ndo limekaa mahala pake zaidi. Anaongea kama Shilole, anacheka kama Shilole, ni shujaa kama Shilole, REAL kama Shilole, anapenda kama Shilole na sisi tunampenda kama Shilole. Ally Rehmtullah alikua anaadhimisha miaka kumi ya kazi yake. So alifanya auditions kwa ajili ya kuchagua models kuelekea kwenye adhimisho lenyewe, Shilole aka Shishi alikua mmoja wa ma judge wa skuihiyo, picha likaanza hakuwepo popote pa kuweza kuonekana, shuguli ambayo ilichelewa kuanza kutokana na mambo mengine ilibidi pia iendelee bila yeye. Akatokea wakati tunakaribia kabisa kumaliza ila alipofika kila mtu alijua kama Shishi KAWASILI. Vicheko na matani vilitawala na kila mtu akasahau kama hata Shishi alichelewa kufika. Shishi ni ‘special’. Kuanzia muonekano mpaka tabia, jinsi anavyoishi maisha yake na jinsi anavyotafuta na kujiongeza kila siku ni mfano tosha kwetu sote ya kwamba ‘mwenda bure si mkaa bure’ Anaweza pia akawa kafanya yote ili kuweza kutumiza ndoto yake au zake. Kaigiza, kaimba, kaishi kwenye mahusiano ambayo hajivunii kama alishawahi kuishi hivyo, kafanya biashara, kapigana na mengine mengi kapitia ambayo yanaweza kumaliza kurasa, yote kwa yote... Ni mfano wa kuigwa kwa watafutaji na wanaoanza wengi. Kwenye meza yetu pia alikuja kachelewa, huku akiwa kavurugwa na baadhi ya watu lakini tulipokaa tu kwenye viti yote yalisahaulika na tukajikita zaidi kwenye mazunguzo yetu ambayo yalijaa vicheko, masikitiko, simulizi za kuacha midomo wazi na faraja tele. Tafadhali enjoy, na chukua mawili matatu ambayo yatakufunza jambo katika safari yako na kukufanya uwe bora zaidi. Love, Salama.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Mar 1, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 5 - Salama Na Shilole | MAMA

0:00 1:11:02

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 11 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on March 1, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!