Ep. 7 - Salama Na Fid Q | NGOSHA WA MBASA episode artwork

EPISODE · Mar 12, 2020 · 1H 23M

Ep. 7 - Salama Na Fid Q | NGOSHA WA MBASA

from Salama Na · host Salama Na

Nakumbuka kipindi ambacho Fidi alikua anaamini kabisa kama kuweka ‘uso wa mbuzi’ ndo kulikua kunakufanya uwe ‘hard core’, sina uhakika lini aliachana na dhana hiyo ila kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi tabasamu na bashasha vimekua havibanduki kwenye uso wake, jambo ambalo mimi kama rafiki nalifurahia sana. Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu wa kike ambao ni wapenzi haswa wa mziki wake walikua wakiniambia eh, sema rafiki yako mgumu jamani, Kha! Mi hucheka tu na baadae wakishazoeana basi sidhani kama kuna hata mmoja anaweza kusema kitu kibaya kuhusu yeye. Nilikua nacheka kwasababu mimi naamini namfahamu rafiki yangu huyu, yeye hupenda sana matani, na kucheka na marafiki wa karibu wanaweza wakathibitisha hilo maana katika watu ambao unaweza ukawatania weeee mpaka asubuhi, na utani mpaka wa vitu vyengine ambavyo wewe wa karibu unaweza kusema hey, hiyo sasa imepitiliza, yeye waala... Atacheka tu! Mwenye kipaji chake cha kujifunza mwenyewe, nasema hivyo kwasababu nadhani kufahamiana kwetu na kuelewana kwetu pia kunatokana na kuwa na vitu vinavyofanana ndani yetu. Kajifunza jinsi ya kupenda kusoma vitabu mwenyewe, kujifunza jinsi ya kuandika na kurap mwenyewe, kajiendeleza mwenyewe (bila ya shaka kuna watu walomsaidia kwa tafu za hapa na pale ila walitokea baada ya kuona jitihada zake). Alihakikisha anasafiri kwenda nje ya nchi na Africa kwa jitihada zake mwenyewe na mpaka leo, kukiitwa watu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha Hip Hop ya nyumbani hapa ilipo basi jina lake litakua ni miungoni ya yale yatakayopata heshima ya juu kabisa. Pia anachekesha sana. Uelewa wake wa baadhi ya vitu unaweza ukakuacha mdomo wazi wakati mwengine. Kwenye uwepo wake? Vicheko lazima vitawale. Hii siku nilitia nae story haikua kama kazi, bali kama mtu na rafikiye tu wakitia story juu ya njia za maisha ambazo tumepitia mpaka sasa. Fidi amekuzwa na Mama yake ambae alikua ni mfanyakazi wa serikalini (ameshastaafu), alikulia mkoani kama wengi wetu, alifika Dar akakaa kwa ndugu kama wengi wetu, alianzia sehemu na kutoka hapo mdogomdogo akajijenga kufikia hapa alipo. Humu tumeongelea hayo, watoto, muziki, ndoa, maisha ya wasanii na maendeleo kwa ujumla. Yangu matumaini uta enjoy na kuelewa baadhi ya vitu zaidi na zaidi. Here’s to Ngosha wa Mbasa. Love, Salama. Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Mar 12, 2020

Embed this episode

NOW PLAYING

Ep. 7 - Salama Na Fid Q | NGOSHA WA MBASA

0:00 1:23:14

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 23 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on March 12, 2020.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!