Furaha ni pale ninapoweza kuhudumia familia yangu episode artwork

EPISODE · Mar 23, 2026 · 2 MIN

Furaha ni pale ninapoweza kuhudumia familia yangu

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi/Rashid Malekela

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Furaha ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Machi, wakazi wa kata ya Luchelele, jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania, wameeleza maana ya furaha katika maisha yao ya kila siku, ambapo kwa wengi, furaha haitokani na anasa, bali inajengwa na afya njema, upendo wa familia, na uwezo wa kuitunza familia hiyo kwa mahitaji ya msingi. Wakizungumza na Rashid Malekela wa Idhaa hii, wanawake wa eneo hilo wameeleza kuwa furaha kwao ni chanzo kikuu cha amani ya moyo. Rehema James amesema kuwa furaha yake kubwa ni kuamka salama, wakati Regina Emmanuel amegusia uhusiano wa mzazi na mtoto kama nguzo ya furaha yake, "Furaha yangu kuu inatokana na mama yangu kuwa hai na mwenye afya."Faida Anthony, mmoja wa wakazi wa eneo hilo, amefafanua kuwa kwake furaha ni matokeo ya jitihada za kutafuta riziki akisema,"Furaha ni kutafuta fedha, mboga, na kuijali familia yangu."Mitandao ya kijamii na changamoto za furahaLicha ya umuhimu wa afya na familia, matumizi ya teknolojia yameanza kuathiri jinsi watu wanavyopata au kupoteza furaha katika ulimwengu wa sasa. Duch Sababu, ambaye ni Afisa Usafirishaji maarufu ‘bodaboda’, amebainisha kuwa mitandao ya kijamii ina sura mbili; inaweza kuleta kicheko kupitia maudhui ya ucheshi au kuleta huzuni kulingana na kile mtu anachokiona, huku akitoa angalizo kwa watumiaji wa mitandao,"Furaha ni afya njema, lakini pia mitandao inaweza kuleta furaha kupitia vichekesho au huzuni kulingana na kile unachokiona."Wito wa Umoja wa MataifaMwaka huu, Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa furaha ya kweli kwa binadamu wote itafikiwa endapo kutakuwa na usawa, haki, na ulinzi wa mazingira kulingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Ili kufikia malengo hayo duniani, kuna uhitaji wa kuendelea kuimarisha huduma za kijamii zinazogusa maisha ya watu wa hali ya chini moja kwa moja.Kwa vijana, wameshauriwa kutumia muda wao kwenye mitandao ya kijamii kutafuta mambo yatakayowajenga kifikra na kuwapa furaha badala ya mambo yanayoweza kuwaharibia amani yao ya moyo.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Mar 23, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

Furaha ni pale ninapoweza kuhudumia familia yangu

0:00 2:27

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 2 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on March 23, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!