Je, Utiifu Wako Utastahimili Mafanikio? episode artwork

EPISODE · Aug 26, 2026 · 8 MIN

Je, Utiifu Wako Utastahimili Mafanikio?

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 12:14–15 tunakutana na Israeli katika hatua mpya. Wamepata kile walichosisitiza kukitaka, sasa wana mfalme. Lakini Samweli anawakumbusha kwamba mazingira yao mapya hayajabadilisha jambo la msingi: bado wanapaswa kumcha Bwana, kumtumikia na kuitii sauti yake.Neno la leo linatufanya tujiulize swali ambalo mara nyingi hatujiulizi: Je, utiifu wetu kwa Mungu unaweza kustahimili mafanikio? Ni rahisi kumtafuta Mungu tunapohitaji kazi, tunapotafuta mwenza, tunapoanzisha biashara au tunaposubiri mlango fulani ufunguke. Lakini nini kinatokea baada ya kupata kile tulichokuwa tunakiombea? Je, bado tunaomba? Bado tunasikiliza? Bado tunamtii Mungu?Israeli walikuwa wameingia katika msimu mpya lakini Mungu hakubadilika. Vivyo hivyo hakuna mafanikio, cheo, fedha, ndoa au hatua mpya inayotufikisha mahali ambapo hatuhitaji tena kumtii Mungu. Kwa kweli kadiri tunavyopewa zaidi ndivyo tunavyohitaji kuwa makini zaidi tusije tukaanza kutegemea tulichopewa kuliko Yule aliyetupa.Kwa hiyo leo tujiulize: Je, tunamtaka Mungu mpaka tupate tunachotaka au tutabaki waaminifu kwake hata baada ya kupata tulichokuwa tunakiomba? Mwanzo mzuri ni muhimu lakini Mungu anatuita kwenye utiifu unaodumu katika kila majira, wakati wa uhitaji na wakati wa mafanikio.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Aug 26, 2026

Embed this episode

Ready to play

Je, Utiifu Wako Utastahimili Mafanikio?

0:00 8:25

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 8 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on August 26, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!