Kuanza Vizuri Haitoshi, Linda Imani Yako Mpaka Mwisho! episode artwork

EPISODE · Aug 31, 2026 · 24 MIN

Kuanza Vizuri Haitoshi, Linda Imani Yako Mpaka Mwisho!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 15:35 tunafunga safari yetu ya mwezi wa Agosti katika sehemu yenye huzuni. Samweli anamwombolezea Sauli na tunaona huzuni iliyotokana na mwelekeo ambao maisha ya Sauli yalikuwa yamechukua. Ni mwisho mzito lakini wenye somo muhimu sana: si muhimu tu kuanza vizuri, ni muhimu kuendelea kutembea na Mungu.Tulianza mwezi huu na Hana, mwanamke aliyefika mbele za Mungu akiwa na maumivu, akamimina moyo wake kwake na kujifunza kusubiri. Tukaona Mungu akimjibu na kupitia Samweli tukajifunza kusikiliza sauti ya Mungu, kumtii, kukumbuka Ebenezeri zetu na kuendelea kuwa waaminifu.Kisha tukamwona Sauli. Alianza akiwa mtu aliyepewa nafasi kubwa na Mungu. Lakini hatua kwa hatua presha, hofu ya watu na utiifu wa masharti vikaanza kuathiri safari yake. Na tunapofika mwisho wa sura ya 15, tunakutana na matokeo ya mwelekeo huo.Hili linaweza kuwa somo kubwa tunalobeba tunapofunga Agosti: ushindi wa jana hauondoi hitaji la utiifu wa leo. Hatutosheki kusema tulianza vizuri, tuliwahi kuwa karibu na Mungu au Mungu aliwahi kututumia. Kila siku tunahitaji kuendelea kumruhusu Mungu atengeneze mioyo yetu.Paulo alipofika mwisho wa safari yake alisema, “Mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda.” Hilo liwe ombi letu pia. Si kwamba hatutakosea njiani bali tunapoanguka tunamrudia Mungu na kuendelea kutembea naye.Tunapofunga mwezi huu, swali letu liwe: Si tu nilianzaje, bali ninaendeleaje? Je, moyo wangu bado unamsikiliza Mungu? Je, bado niko tayari kumtii?Tusiombe tu Mungu atusaidie kuanza vizuri. Tumwombe atupe neema ya kubaki waaminifu na kumaliza vizuri.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Aug 31, 2026

Embed this episode

Ready to play

Kuanza Vizuri Haitoshi, Linda Imani Yako Mpaka Mwisho!

0:00 24:45

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 24 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on August 31, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!