EPISODE · Sep 10, 2026 · 13 MIN
Kwa Jina la Bwana!
from Neno la Leo
🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 17:45 tunafika katika moja ya kauli zenye nguvu zaidi katika simulizi ya Daudi na Goliathi. Goliathi anasimama mbele ya Daudi akiwa na upanga, fumo, mkuki, uzoefu wa vita na mwonekano wa kutisha. Daudi ana fimbo, kombeo na mawe.Kwa macho ya kibinadamu, hakuna ushindani.Lakini Daudi anasema: “Wewe unanijia kwa upanga na fumo na mkuki, bali mimi ninakujia kwa jina la Bwana wa majeshi.”Na hapo ndipo tunagundua siri ya ujasiri wa Daudi.Haikuwa kombeo. Haikuwa jiwe. Wala haikuwa confidence kubwa ndani yake mwenyewe. Daudi alikuwa anajua Mungu anayesimama nyuma yake.Hili ni muhimu sana kwa sababu tunaweza kuisoma simulizi ya Daudi na Goliathi kama motivational story inayosema, “Jiamini na unaweza kushinda giant yoyote.” Lakini Daudi mwenyewe hasemi hivyo. Hasemi, “Goliathi, ninakuja kwa sababu ninajiamini.” Anasema, “Ninakujia kwa jina la Bwana.”Hii ndiyo confidence ya Mkristo. Tunajiandaa. Tunajifunza. Tunakuza uwezo wetu. Tunafanya kazi kwa bidii na kutumia vizuri kile Mungu alichoweka mikononi mwetu. Lakini hatufanyi silaha zetu kuwa chanzo cha tumaini letu.Huenda leo unaingia kwenye meeting muhimu, interview, assignment mpya, biashara, changamoto ya kifamilia au jambo ambalo linakutisha. Jiandae vizuri. Fanya sehemu yako kwa uaminifu. Lakini moyoni ujue: “Sitegemei uwezo wangu peke yake. Ninakwenda pamoja na Mungu.”Daudi alikuwa na kombeo mkononi lakini tumaini lake lilikuwa kwa Bwana.Na huenda hilo ndilo tunalohitaji kujikumbusha leo: tumia kile kilicho mkononi mwako lakini mtegemee Yule aliye pamoja nawe.Ninakujia kwa jina la Bwana!Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Embed this episode
Ready to play
Kwa Jina la Bwana!
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.
Similar Podcasts
No similar podcasts found.