EPISODE · Mar 23, 2026 · 3 MIN
Madhara ya vita vya Israeli/Marekani dhidi ya Iran yazidi kudhihirika
from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi/Flora Nducha
Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiingia wiki ya nne tangu uanze tarehe 28 mwezi uliopita wa Februari, Umoja wa Mataifa leo umeonya kuwa athari mbaya za kibinadamu na uchumi wa kimataifa zinaongezeka wakati mzozo huo ukivuruga kabisa njia muhimu za usambazaji wa bidhaa ndani ya Mashariki ya Kati na kwingineko duniani. Flora Nducha na taarifa zaidi.Asante Assumpta. Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati sasa umevuka mipaka ya eneo hilo, ukiathiri pia Asia na Afrika, hasa katika biashara na usafirishaji.Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Miradi na Huduma, UNOPS inaonya kuwa mamilioni ya watu wako hatarini kutokana na athari za kibinadamu na kiuchumi. Mkuu wa shirika hilo, Jorge Moreira da Silva, amesema kuvurugika kwa usafirishaji kupitia Mlango Bahari wa Hormuz kumesababisha mshtuko mkubwa wa kiuchumi duniani.Amesema “Nchi zinazoendelea barani Asia na Afrika zina uwezekano mkubwa wa kubeba gharama kubwa zaidi hali inayotishia usalama wa chakula,” na kuongeza kuwa njaa duniani inaweza kuongezeka kwa makumi ya mamilioni ya watu.Pia amesema mgogoro huu unazidisha hali mbaya iliyopo katika nchi kama Sudan, Sudan Kusini, Afghanistan, Yemen, na Somalia, ambapo mifumo ya chakula tayari ni dhaifuAmeonya pia kuwa mashambulizi dhidi ya meli na kuvunjika kwa minyororo ya usambazaji kunazuia upatikanaji wa dawa na misaada, hasa Gaza, huku vita vikienea vinaweza pia kuhatarisha fedha zinazotumwa nyumbani kwa familia, hasa Asia Kusini.Nchini Lebanon, kwa mujibu wa Sirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, zaidi ya watu 1,000 wameuawa na wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa tangu mapema Machi, wakiwemo wahudumu wa afya, wanahabari na wafanyakazi wa misaada.Watoto wanaendelea kubeba mzigo mkubwa. Naibu Mkurugenzi wa UNICEF, Ted Chaiban, anasema “Watoto wanaouawa au kujeruhiwa ni sawa na darasa moja kila siku.”UNICEF inaonya pia juu ya athari kubwa za kisaikolojia kwa watoto na wahudumu wa misaada.Katika Ukanda wa Gaza, hali inazidi kuwa mbaya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestna UNRWA, limesema mamia ya watu wamepata ulemavu wa kudumu huku huduma za afya na misaada zikizidi kuwa finyu.Wakati huo huo, hofu ya usalama wa nyuklia inaongezeka kufuatia mashambulizi karibu kweny vituo nyeti nchini Iran na Israel. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomic IAEA, Rafael Grossi, ameonya kuwa: “Hakuna hatua ya kijeshi inayopaswa kuhatarisha usalama wa vituo vya nyuklia.”Ingawa hakuna ongezeko la mionzi lililoripotiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa a Afya Duniani WHO, tayari linaanza maandalizi ya dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa bila hatua za haraka za kupunguza mzozo, dunia inaweza kukabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu na kiuchumi.
What this episode covers

NOW PLAYING
Madhara ya vita vya Israeli/Marekani dhidi ya Iran yazidi kudhihirika
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.