Mungu Haangalii Sura, Anaangalia Moyo Wako! episode artwork

EPISODE · Sep 1, 2026 · 30 MIN

Mungu Haangalii Sura, Anaangalia Moyo Wako!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 16:7 tunaanza mwezi mpya na hatua mpya katika simulizi ya 1 Samweli. Agosti tuliimaliza na Sauli, mtu aliyeanza vizuri lakini ambaye hatua kwa hatua alianza kuweka maamuzi yake mbele ya utiifu kwa Mungu. Sasa Samweli ametumwa nyumbani kwa Yese kumtafuta mfalme mwingine.Anapomwona Eliabu, Samweli anavutiwa na kile kinachoonekana kwa macho. Anaonekana kama mtu anayefaa kuwa mfalme. Lakini Mungu anamfundisha jambo ambalo litakuwa msingi wa safari yetu na Daudi: mwanadamu huangalia sura ya nje lakini Bwana huangalia moyo.Na hapo ndipo tunapoanzia Septemba: moyoni.Tunaishi katika dunia inayotufundisha kujenga kile watu wanaweza kuona. Muonekano, elimu, cheo, fedha, mafanikio, followers na namna tunavyoonekana mbele za wengine. Lakini Mungu anaona mahali ambapo hakuna mwanadamu anayeweza kuona kikamilifu. Anaona nia zetu, tamaa zetu, sababu zinazotusukuma kufanya tunayofanya na tabia yetu wakati hakuna anayetuangalia.Hii ndiyo tofauti tutakayoanza kuiona kati ya Sauli na Daudi. Siyo kwamba Daudi alikuwa mkamilifu. Tutakuja kuona makosa yake pia. Lakini Mungu alikuwa akitafuta moyo unaoweza kumrudia, kumsikiliza na kutengenezwa naye.Kwa hiyo tunapoanza mwezi huu, labda kabla hatujamwomba Mungu abadilishe kazi yetu, biashara yetu, mahusiano yetu au mazingira yetu, tuanze na ombi la ndani zaidi: “Bwana, tengeneza moyo wangu.”Na swali letu la kwanza la Septemba liwe hili:Mungu akiangalia moyo wangu leo, anaona nini?Kwa sababu watu wanaweza kuvutiwa na kile kilicho nje lakini Mungu huanzia ndani.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 1, 2026

Embed this episode

Ready to play

Mungu Haangalii Sura, Anaangalia Moyo Wako!

0:00 30:09

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 30 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on September 1, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!