Nafsi Yangu Ina Amani episode artwork

EPISODE · Aug 6, 2024 · 1H 48M

Nafsi Yangu Ina Amani

from Men The Podcast · host Michael Baruti

Nafsi Yangu Ina Amani Katika dunia ambayo inashangalia ukamilifu wa mwanaume, dunia ambayo bado haiko tayari kuzungumzia kwa kina juu ya afya ya akili ya mwanaume, dunia ambayo mwanaume anayepitia changamoto za afya ya akili bado anatengwa na kuonekana mtu asiyefaa kushirikishwa na jamii yake, Sunday Kapesi anapambana kubadilisha hayo. Toka safari yake ya kuondokewa na baba yake mzazi, kuanza kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kupata urahibu, kuweza kumuangalia mama yake na ndugu zake usoni na kukiri kwamba anahitaji msaada, na kuamua kwenda “rehab” ili aweze kupambana na urahibu huo, Sunday haachi simulizi yeyote kwenye mazungumzo haya. Kama baba, kama mtoto, kama kaka, na kama mtu ambaye ana ndoto za kuisaidia na kuiokoa jamii yake, Sunday anaongea na sisi ni namna gani ni rahisi mno kwa mtu yeyote, hususani mwanaume kuingia kwenye urahibu, lakini pia anatutia moyo kwamba kila tatizo bado linauwezo wa kutatuliwa. Ilimchukua muda kiasi gani kwa Sunday kupambania afya yake ya akili mpaka kufikia hatua ya kuweza kupata “amani kwenye nafsi yake”?  Sikiliza kiundani mazungumzo haya ili na wewe uweze kufahamu kwamba haijalishi unapitia magumu kiasi gani, siku zote kuna suluhisho la unayopitia, na linaweza kuwa suluhisho bora ambalo litajenga zaidi afya yako ya akili na kukufanya uwe bora zaidi ya jana. Pambana kuipa nafsi yako amani

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Aug 6, 2024

Embed this episode

NOW PLAYING

Nafsi Yangu Ina Amani

0:00 1:48:12

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Men The Podcast?

This episode is 1 hour and 48 minutes long.

When was this Men The Podcast episode published?

This episode was published on August 6, 2024.

Can I download this Men The Podcast episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!