Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo! episode artwork

EPISODE · Sep 16, 2026 · 36 MIN

Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 19:4–5 tunamwona Yonathani akifanya jambo linalotuonyesha maana nyingine ya urafiki wa kweli.Sauli sasa anataka Daudi auawe. Daudi hayupo kwenye mazungumzo haya lakini Yonathani yupo. Na badala ya kukaa kimya, anamkumbusha baba yake ukweli: Daudi hajamkosea. Anamkumbusha jinsi Daudi alivyohatarisha maisha yake kupigana na Goliathi na jinsi Mungu alivyotumia ushindi wake kuleta furaha kwa Israeli.Lakini kuna jambo kubwa zaidi hapa. Yonathani angeweza kufaidika Daudi akiondolewa. Kama mwana wa Sauli, alikuwa na maslahi yake mwenyewe katika kiti cha enzi. Hata hivyo, Yonathani anachagua kilicho sahihi kuliko kile kinachoweza kumnufaisha yeye.Huo ndio urafiki wa kweli.Ni rahisi sana kumwambia mtu, “Wewe ni rafiki yangu,” akiwa mbele yetu. Lakini kipimo kingine cha urafiki kinakuja pale jina lake linapotajwa akiwa hayupo.Watu wakianza kumsema vibaya, tunafanya nini? Tunajiunga nao? Tunakaa kimya ili tusiharibu nafasi yetu kwenye kundi? Au tunakuwa na ujasiri wa kusema, “Hapana, hicho mnachosema si sahihi”?Kutetea rafiki hakumaanishi kuficha makosa yake. Rafiki wa kweli anaweza kukuambia ukweli unapokosea. Lakini pia hataruhusu uongo usemwe juu yako wakati anajua ukweli.Na huenda leo swali si tu, “Nina rafiki kama Yonathani?” Swali kubwa zaidi linaweza kuwa:“Mimi ni Yonathani kwa nani?”Je, watu ninaowaita marafiki wanaweza kuwa na uhakika kwamba hata wakiwa hawapo, sitatumia udhaifu wao kujinufaisha, sitajiunga na wanaowasema vibaya na nitasimamia ukweli?Kwa sababu rafiki wa kweli si yule anayesema mazuri kuhusu wewe ukiwepo tu. Ni yule anayesimamia ukweli hata ukiwa haupo.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 16, 2026

Embed this episode

Ready to play

Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo!

0:00 36:07

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 36 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on September 16, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!