Ruhusu Mungu Akutengeneze. episode artwork

EPISODE · Sep 3, 2026 · 18 MIN

Ruhusu Mungu Akutengeneze.

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 16:13 tunaendelea na simulizi ya Daudi. Jana tulimwacha malishoni, mahali ambapo watu hawakumfikiria lakini Mungu alikuwa amemwona. Leo anaitwa nyumbani na Mungu anamwambia Samweli, “Ondoka, umtie mafuta, maana huyu ndiye.” Daudi anapakwa mafuta katikati ya ndugu zake na Roho wa Bwana anakuja juu yake.Lakini jambo la kushangaza ni hili: Daudi alipakwa mafuta kuwa mfalme lakini hakwenda moja kwa moja kukalia kiti cha enzi.Alikuwa amechaguliwa lakini bado alikuwa na safari. Kulikuwa na tofauti kati ya kusudi alilopewa na utayari wa kulibeba.Nasi tunaweza kufanya kosa la kutaka kila kitu kitokee mara tu tunapoanza kuona kusudi la Mungu katika maisha yetu. Tunapata ndoto, maono, kipawa au nafasi fulani na tunataka jukwaa mara moja. Lakini Mungu anaweza kukuita leo na bado akatumia muda kukufundisha, kukukomaza na kuandaa tabia yako kwa kile anachotaka kukukabidhi kesho.Usikimbilie jukwaa kwa sababu tu umeona kusudi. Ruhusu Mungu akutengeneze.Daudi alipakwa mafuta kabla taifa halijamtambua. Mungu alikuwa ameona ndani yake kile ambacho wengine bado hawajakiona. Kwa hiyo kama watu bado hawaoni kile Mungu anaweka ndani yako, usiwe na haraka ya kujithibitisha. Endelea kuwa mwaminifu katika hatua uliyo nayo sasa.Swali si tu, “Je, Mungu amenichagua?” Swali jingine muhimu ni, “Je, ninamruhusu Mungu aniandae kwa kile alichonichagulia?”Kwa sababu wakati wako utakapofika, hutahitaji tu nafasi. Utahitaji uwezo na tabia ya kubeba kile ambacho Mungu amekukabidhi.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 3, 2026

Embed this episode

Ready to play

Ruhusu Mungu Akutengeneze.

0:00 18:59

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 18 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on September 3, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!