SE7EP04 - SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO | شيخ  episode artwork

EPISODE · Jul 7, 2022 · 58 MIN

SE7EP04 - SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO | شيخ

from Salama Na · host Salama Na

Sheikh Hilali Shaweji Makarani au Sheikh Kipozeo ni mtu wa watu, au niseme kama ambavyo tunasema kwetu Uswazi, Sheikh ni mwana wa wana, anaweza kuwapa wana darsa kwa lugha yao na wakawa huru na wao kusema maoni yao au uelewa wao kwa raha na bashasha nyingi na naamini hii imemfanya yeye awe ni mmoja ya Ma Sheikh wanao tambulika zaidi kwenye mitandao ya kijamii nje na ndani ya Tanzania. Lugha hiyo ya wana ambayo anaitumia inasaidia sana kufikisha ujumbe ambao ameukusudia kwa wakati huo na ikapata mpaka majadilioano, majadiliano hayo ndo huzaa majibu ya maswali mengi ambayo wengi hujiuliza. Kwetu au kwangu ilikua ni kaji task ambako nilikua najua inabidi nikakamilishe, na jina lake kurejea kutajwa mara kwa mara na watazamaji wa kipindi hiki pia ilichochea dhamira hiyo kwa kiasi kikubwa. Nilikua sijawahi kukutana nae kwahiyo hii nami ilikua ni mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho, shabiki yake? Oh yes, mkubwa tu. Nimekua nikimskiliza na kumuangalia kila nipatapo nafasi ya kukutana na mafunzo yake, kwahiyo hamu ya kutaka kuongea nae ilikua inaongezeka kila siku zinavyozidi kwenda. Wakati ambao Mwenyezi Mungu ameupanga ndo wakati sahihi kabisa. Na naamini huu ndo ulikua muda ambao tulikua tumepangiwa haya mazungumzo kutokea na haikua huko nyuma ambako pengine tulidhani tungemtafuta na kuweza kuongea nae. Alikua mkarimu kwangu, humchukua muda pia kuongea kama yule wa kwenye video maana kama Mwalimu nadhani huwa anaangalia spidi ambayo uko nayo na kujua anaenda na wewe vipi ili iwe imekaa mahala pake. Na naam, tuliweza kwenda vizuri, alinifanya nami niwe huru na muwazi kwa yale ambayo tulikua tumepanga na wenzangu kumuuliza. Akiwa Baba na mume mpedwa kwa familia yake, Sheikh Kipozeo amekua akipata mialiko sehemu mbali mbali ili aweze kuwapa watu ‘dawa’. Humu zaidi sisi tulitaka kujua jina lilipo anzia na jitihada zake za kufikisha neno la Mwenyezi Mungu kwa wanaohusika. Alituambia pia kuhusu asili yake na ‘urithi’ wa dini ulipotokea. Lini hasa alijua kwamba ambacho anakifanya sasa ndo ambacho alikua anatakiwa kufanya kwenye maisha yake yote? Yangu matumaini dawa itaingia na uta enjoy kuangalia au kuskiliza episode hii yetu ya nne. Love, Salama.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jul 7, 2022

Embed this episode

NOW PLAYING

SE7EP04 - SALAMA NA SHEIKH KIPOZEO | شيخ

0:00 58:42

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 58 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on July 7, 2022.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!