SE7EP15 - SALAMA NA MCHUNGAJI RICH BILIONEA | SERMON episode artwork

EPISODE · Sep 22, 2022 · 1H 5M

SE7EP15 - SALAMA NA MCHUNGAJI RICH BILIONEA | SERMON

from Salama Na · host Salama Na

Kipindi cha nyuma kidogo nilifanya lile ambalo huwa nafanya la kuwashirikisha rafiki zangu na team kuhusu list ya watu ambao wangependa kuwaona kwenye kiti chetu chakavu na sababu za kwanini hasa waje kwenye meza ile yenye kigae kwa juu maana tukisema tutaje majina tu bila ya sababu thabit za wao kuja pale tunaweza tukaondoa maana yenyewe ya kuwa na watu wenye story za kuvutia na kutufunza kama ambavyo tumekua tukifanya. Jina la mgeni wetu huyu lililetwa kwangu na Michael (Mx) Mlingwa na Ndugu yangu Elbogast Myaluko ndo alinipatia mawasiliano naye na kuanzia hapo mengine yamebaki kukhadithiwa kama hivi. Sikua namfahamu Mchungaji Richard Hananja mpaka Michael alipo niambia nami nikachukua muda wangu wa kwenda kufanya ka research kangu kabla hajaja mezani, ambacho nilijifunza ni kwamba Mchungaji alikua ni mtu mashuhuri sana ambaye ana watu wengi sana pia wanao mskiliza. Ilinichukua takriban miezi miwili kuweza kumpata maana kila weekend (mara nyingi rekodi za kipindi huwa zinafanyika weekend) yeye huwa yuko safarini. Huitwa sana sehemu mbali mbali, na sasa Serikali nayo imekua ikimuita pia katika matamasha na mikutano mbalimbali. Kwahiyo mara utamsikia yuko Dodoma, mara Moshi, mara Iringa ilimradi yuko busy. Na wakati mwengine Jumapili yake inakua ya yeye kualikwa kwenye Makanisa mbalimbali ili akatoe neno, siku hizi yeye ameshastaafu kuhubiri kanisani na sasa zilizobaki ni hizo za mialiko maalum. Kama kawaida mimi na wenzangu tulitaka kuanza kwa kumfahamu mgeni wetu maana kama nilivyokuambia hapo awali mimi sikua namfahamu zaidi tu ya kumuona kwenye mitandao akimwaga cheche, tulianzia kwenye kuzaliwa kwake na kukua kwake, mitihani mbalimbali ya ujana, bishara na kazi ambazo ashawahi fanya, na wakati naandika hii nimejifunza pia kuwa Mchungaji hana ambalo anaongeza chumvi maana baada ya sisi kufanya nae maongezi haya, nimeona ameenda sehemu tofauti tofauti na story yake haijawahi kubadilika. Ujasiri wa ziada huhitajika ili tuweze kufanikiwa kwenye maisha yetu na pia kuwa kwenye mstari ili usiingie kwenye matatizo na vyombo vya sheria. Mchungaji ananiambia jinsi ambavyo alikua ana hustle kila kona, kusafiri bila ya kibali cha kuvuka mipaka ya nchi na boxing ambayo aliifanya kwenye kipindi flani kwenye maisha yake. Boxing imemuachia kovu ambalo kila siku linamkubusha mapambano ambayo ameshawahi kuyafanya kwenye maisha yake. Boxing pia ndo ambayo imemfanya awe na discipline ya hali ya juu. Kwenye maisha yake ya sasa Mchungaji Hananja anatoa nafasi kwa kila aliye kata tamaa au ambae watu wamemkatia tamaa, yeye ndo huwachukua hao na kuwapa nafasi nyengine kwenye maisha yao, na amini usiamini wengi wao hunyooka na kuanza upya. Kwenye nyumba yake huko Madale Mchungaji anafanya mambo mengi ikiwa pamoja na kilimo na ufugaji. Swali langu lilianza kwa kutaka kujua hizo pesa za yeye kuweza kufanya mambo yote hayo, huwa zinatoka wapi? Mchungaji Hananja ni MUME, na kwa mujibu wa maelezo yake, alichelewa saana kuoa na mkewe ni Rafiki yake wa kwanza. Yangu matumaini moja mbili tulizopiga humu zitakupeleka sehemu. Tafadhali enjoy. Love, Salama.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 22, 2022

Embed this episode

NOW PLAYING

SE7EP15 - SALAMA NA MCHUNGAJI RICH BILIONEA | SERMON

0:00 1:05:02

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Salama Na?

This episode is 1 hour and 5 minutes long.

When was this Salama Na episode published?

This episode was published on September 22, 2022.

Can I download this Salama Na episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!