EPISODE · Sep 15, 2026 · 21 MIN
Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani!
from Neno la Leo
🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 18:14 tunakutana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kuhusu maisha ya Daudi: “Daudi akafanikiwa katika njia zake zote, naye Bwana alikuwa pamoja naye.”Ni rahisi kusimama kwenye sehemu ya kwanza, “Daudi akafanikiwa.” Lakini siri ya maisha yake ipo katika sehemu inayofuata: “Bwana alikuwa pamoja naye.”Mwezi huu tumemfuata Daudi kutoka malishoni. Tulimwona akiwa kijana asiyepewa nafasi kubwa hata ndani ya familia yake. Akaingia ikulu. Akasimama mbele ya Goliathi. Akapata ushindi na jina lake likaanza kujulikana katika Israeli. Sasa Sauli anaanza kumwonea wivu na kumwangalia kwa mashaka.Mazingira ya Daudi yanaendelea kubadilika lakini uwepo wa Mungu unabaki kuwa msingi wake.Na hapa kuna swali muhimu kwetu. Tunapotafuta maendeleo, fedha, cheo, biashara inayokua, recognition na milango mipya, je, tunatafuta pia kuhakikisha kwamba tunabaki karibu na Mungu?Kwa sababu inawezekana kupata kile tulichokuwa tunakiomba lakini njiani tukapoteza kitu cha thamani zaidi. Ndiyo maana Yesu anauliza, “Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote na kupata hasara ya nafsi yake?”Mafanikio ya kweli si kuwa na kila kitu huku moyo wako ukiwa mbali na Mungu. Mafanikio makubwa ni kufika unakokwenda bila kumpoteza Mungu njiani.Kwa hiyo leo usiombe tu, “Bwana, nifanikishe.” Omba pia, “Bwana, ninapopanda, ninapofanikiwa na ninapofunguliwa milango mipya, nisaidie nibaki karibu nawe.”Kwa sababu mwisho wa yote, jambo kubwa zaidi linaloweza kusemwa kuhusu maisha yetu si tu kwamba “alifanikiwa.”Ni kwamba:“Alifanikiwa, naye Bwana alikuwa pamoja naye.”Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Embed this episode
Ready to play
Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani!
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.
Similar Podcasts
No similar podcasts found.