Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako! episode artwork

EPISODE · Sep 12, 2026 · 44 MIN

Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 17:49–50 tunafika katika wakati ambao tumekuwa tukiuelekea kwa siku kadhaa. Daudi anaweka mkono katika mfuko wake, anachukua jiwe, analitia katika kombeo na kumpiga Goliathi kwenye paji la uso. Yule mtu aliyekuwa amelitia hofu jeshi zima la Israeli anaanguka.Goliathi alikuwa na upanga, mkuki, deraya na uzoefu mkubwa wa vita. Daudi alikuwa na kombeo na jiwe.Lakini tayari tumejifunza kwamba nguvu ya Daudi haikuwa katika jiwe. Tumaini lake lilikuwa kwa Bwana. Hata hivyo, Mungu hakumwambia Daudi atupe kombeo lake. Daudi alimtegemea Mungu huku akitumia kile ambacho tayari alikuwa nacho mikononi mwake.Na hapo ndipo Neno la leo linapotufikia.Mara nyingi tunasubiri kitu kikubwa ndipo tuanze. Tunajiambia, “Nikipata fedha zaidi nitaanza. Nikipata connections zaidi nitafanya. Nikipata watu zaidi, elimu zaidi au mazingira mazuri zaidi ndipo nitaweza.” Na wakati mwingine kweli tunahitaji maandalizi na rasilimali zaidi. Lakini kuna wakati swali muhimu si, “Ninakosa nini?” bali “Ninafanya nini na kile ambacho tayari Mungu amenipa?”Huenda kombeo lako leo ni ujuzi fulani. Huenda ni wazo, nafasi ndogo, muda, kipaji, elimu au hata mtu mmoja anayekuamini. Usikidharau kwa sababu hakionekani kikubwa kama silaha za Goliathi.Kumbuka pia, Daudi hakuliona kombeo kwa mara ya kwanza siku ya vita. Alikuwa amejifunza kulitumia malishoni. Kwa hiyo usiwe mwaminifu tu kutumia ulicho nacho, endelea pia kukikuza na kukitumia vizuri.Huenda tunamwomba Mungu atupe zaidi wakati yeye anatuita kwanza kuwa waaminifu kwa kile ambacho tayari ametuwekea mikononi.Fanya sehemu yako. Tumia ulicho nacho. Kikuze kwa uaminifu. Mtegemee Mungu. Kisha mwachie yeye ukubwa wa matokeo.Kwa sababu wakati mwingine Mungu hahitaji kuanza na kile ambacho bado huna. Anaweza kuanza na kile kilicho mikononi mwako.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 12, 2026

Embed this episode

Ready to play

Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako!

0:00 44:11

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 44 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on September 12, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!