Usiifiche Karama Ambayo Mungu Ameweka Ndani Yako! episode artwork

EPISODE · Aug 24, 2026 · 19 MIN

Usiifiche Karama Ambayo Mungu Ameweka Ndani Yako!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 10:22 tunakutana na picha ya kushangaza. Wakati umefika wa Sauli kutangazwa mbele ya watu kama mfalme lakini Sauli haonekani. Wanapomtafuta, Mungu anawaonyesha kwamba amejificha miongoni mwa mizigo. Jana tuliona Roho wa Bwana akimjia Sauli na Mungu akimwezesha kwa ajili ya jukumu lililokuwa mbele yake. Leo mtu yule yule ambaye Mungu amemwandaa anajificha.Neno la leo linatufanya tujiulize: Kwa nini wakati mwingine tunakimbia kile ambacho Mungu mwenyewe ameweka ndani yetu? Mungu anaweza kutupa karama, uwezo, nafasi au jukumu lakini hofu, kujiona hatutoshi au kuogopa maoni ya watu kukatufanya tujifiche. Kuna tofauti kati ya unyenyekevu na kujidharau. Wakati mwingine tunasema, “Mimi siwezi, mimi sifai, kuna wengine bora kuliko mimi,” tukidhani ni unyenyekevu wakati kumbe hofu imevaa mavazi ya unyenyekevu.Lakini kuna tahadhari nyingine muhimu katika simulizi ya Sauli. Kupewa uwezo na Mungu hakumaanishi kwamba kila uchaguzi wetu wa baadaye utakuwa sahihi. Sauli atalazimika kuendelea kuchagua utii. Hivyo ujasiri wa kutoka mafichoni lazima uambatane na utegemezi kwa Mungu.Je, kuna kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako lakini umekuwa ukikificha kwa sababu ya hofu? Huenda tatizo si kwamba Mungu hajakupa uwezo. Huenda ni kwamba bado hujawa tayari kutoka miongoni mwa “mizigo” yako na kutumia kile alichokupa.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Aug 24, 2026

Embed this episode

Ready to play

Usiifiche Karama Ambayo Mungu Ameweka Ndani Yako!

0:00 19:10

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 19 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on August 24, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!