EPISODE · Sep 9, 2026 · 40 MIN
Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine!
from Neno la Leo
🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 17:38–40 tunaendelea na simulizi ya Daudi kuelekea kwa Goliathi. Baada ya Sauli kukubali Daudi aende kupigana, anamvika mavazi yake ya vita, kofia ya shaba, deraya na kumpa upanga. Ni vifaa vizuri kabisa vya vita, lakini Daudi anapojaribu kutembea navyo anatambua jambo muhimu: hajavizoea.Anavivua.Badala yake anachukua fimbo yake, mawe matano laini na kombeo lake, vitu ambavyo alikuwa amejifunza kuvitumia muda mrefu akiwa malishoni.Neno la leo linatukumbusha kwamba si kila kitu kinachomfaa mtu mwingine kitakufaa wewe. Tunaweza kujifunza kutoka kwa watu, kupokea ushauri, mentorship na maarifa yao lakini hatuhitaji kuwa nakala zao.Mara nyingi tunapokaribia nafasi kubwa tunaanza kuangalia waliofanikiwa kabla yetu na kufikiri lazima tuzungumze kama wao, tuongoze kama wao, tufanye kazi kama wao au tutumie kile walichotumia. Na bila kujua, tunaweza kuanza kudharau kile ambacho Mungu ameweka ndani yetu kwa sababu hakifanani na cha mwingine.Lakini Daudi asingemshinda Goliathi kwa kujaribu kuwa Sauli.Silaha za Sauli zilionekana kubwa kuliko kombeo la Daudi lakini Daudi alikuwa amejifunza kutumia kombeo lake muda mrefu kabla hajafika kwenye bonde hili. Kile kilichoonekana kidogo mbele za watu kilikuwa kitu ambacho tayari alikuwa amekiendeleza kwa uaminifu.Na hilo linatuuliza: Ni kitu gani Mungu ameweka mikononi mwako ambacho unakidharau kwa sababu unalinganisha na kile alichompa mwingine?Jifunze kutoka kwa wengine lakini usipoteze kile Mungu ameweka ndani yako. Tambua karama zako. Zikuze. Jifunze kuzitumia vizuri. Mungu hakukuitia kuwa version dhaifu ya mtu mwingine.Na kama tutakavyoona kesho, ushindi wa Daudi haukuwa katika kombeo lenyewe. Nguvu yake ilikuwa mahali pengine kabisa. Lakini kwa leo, kumbuka hili: usiache kombeo lako kwa sababu tu silaha ya Sauli inaonekana kubwa zaidi.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Embed this episode
Ready to play
Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine!
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.
Similar Podcasts
No similar podcasts found.