EPISODE · Sep 7, 2026 · 16 MIN
Usingoje Kila Mtu Aamini Ndipo Wewe Uamini!
from Neno la Leo
🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 17:32 tunafunga wiki yetu ya kwanza ya Septemba tukiwa tumemfuata Daudi kutoka malishoni mpaka sasa amesimama mbele ya mfalme.Kwa siku nyingi jeshi la Israeli limekuwa likimsikiliza Goliathi akitoa vitisho. Kila anapotokea, hofu inaenea. Wanaume waliofunzwa vita wanaona ukubwa wa tatizo na mioyo yao inakata tamaa. Lakini Daudi, kijana ambaye hata hakuwa mwanajeshi, anafika mbele ya Sauli na kusema, “Moyo wa mtu yeyote usizimie kwa ajili yake. Mtumishi wako atakwenda kupigana na huyu Mfilisti.”Mazingira hayajabadilika. Goliathi bado yupo. Jeshi la Wafilisti bado lipo. Kilichobadilika ni kwamba sasa kuna mtu mmoja ambaye amekataa kuiona hali kupitia hofu ya kila mtu mwingine.Neno la leo linatufundisha kwamba tunapaswa kuwa makini tusije tukabeba hofu ya mazingira yetu. Wakati mwingine utajikuta mahali ambapo kila mtu anaona sababu za kukata tamaa. Watu watasema haiwezekani, hakuna njia, tumeshajaribu au hali ni kubwa kuliko uwezo wetu. Hilo halimaanishi tujifanye tuna majibu yote. Lakini pia hofu ya wengi isiwe ndiyo inayoamua kile tunachoamini kuhusu Mungu.Daudi anatufundisha kwamba huhitaji kusubiri kila mtu awe na imani ndipo wewe uamini.Na ujasiri wake haukuwa kujiamini kipofu. Kesho tutaona kwamba Daudi alikuwa na historia na Mungu. Alikuwa amemwona Mungu akimsaidia huko nyuma na historia hiyo ndiyo iliyompa ujasiri wa kukabiliana na kile kilichokuwa mbele yake.Kwa hiyo tunapofunga wiki hii, jiulize: Je, kuna hofu ambayo nimeianza kuamini kwa sababu tu kila mtu anaiamini?Wakati mwingine Mungu huanza kubadilisha mazingira kupitia mtu mmoja anayekataa kuruhusu hofu iwe na sauti kubwa kuliko imani.Usingoje kila mtu aamini ndipo wewe uamini.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Embed this episode
Ready to play
Usingoje Kila Mtu Aamini Ndipo Wewe Uamini!
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.
Similar Podcasts
No similar podcasts found.