EPISODE · Sep 6, 2026 · 16 MIN
Usiruhusu Maneno ya Watu Yazuie Kufikia Malengo Yako!
from Neno la Leo
🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 17:28–29 tunaendelea na simulizi ya Daudi na Goliathi. Jana tuliona Daudi akiitazama changamoto kwa macho tofauti. Lakini kabla hajafika hata mbele ya Goliathi, anakutana na vita nyingine ambayo huenda hakuitarajia: maneno ya ndugu yake mwenyewe, Eliabu.Eliabu anamsikia Daudi akiuliza kuhusu Goliathi, anakasirika na kuanza kumshutumu. Anahoji sababu ya Daudi kuja vitani na hata kutafsiri vibaya nia ya moyo wake.Fikiria hilo: Daudi hajapigana na Goliathi lakini tayari kuna mtu anayemwambia, kwa namna fulani, “Wewe unafanya nini hapa?”Na maisha yanaweza kuwa hivyo pia. Kabla hujafika kwenye changamoto yenyewe unaweza kukutana na sauti zinazokuambia huwezi, hujui, huna uzoefu, hufai au hata kwamba nia yako si nzuri. Na wakati mwingine sauti hizo zinaweza kutoka kwa watu ambao tulitarajia wangetuelewa zaidi.Lakini Daudi anatufundisha jambo muhimu. Hakutumia nguvu zake zote kumshawishi Eliabu amwelewe. Alijibu kisha akaendelea mbele.Nasi tunahitaji hekima hiyo. Haimaanishi kwamba kila ushauri unaopingana nasi ni mbaya. Kuna wakati Mungu anaweza kutumia watu kutusahihisha. Lakini pia si kila sauti inapaswa kupewa mamlaka ya kuamua mwelekeo wa maisha yetu.Ukisimama kujitetea mbele ya kila mtu anayekuelewa vibaya, unaweza kutumia nguvu zako kwenye vita ambavyo hukupewa kupigana na kuchelewa kufika kwenye kile kilicho mbele yako.Huenda si kila mtu ataelewa kile unachofanya. Si kila mtu ataamini unaweza. Na si kila mtu atatafsiri nia yako kwa usahihi. Lakini si lazima kila mtu akuelewe ndipo uendelee kufanya kile unachojua ni sahihi mbele za Mungu.Daudi alikuwa na Goliathi mbele yake. Hakuwa na muda wa kuifanya Eliabu kuwa vita yake kuu.Usipoteze muda kujitetea kwa kila mtu. Sikiliza kwa hekima, baki mnyenyekevu na endelea mbele.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Embed this episode
Ready to play
Usiruhusu Maneno ya Watu Yazuie Kufikia Malengo Yako!
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.
Similar Podcasts
No similar podcasts found.