Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako! episode artwork

EPISODE · Sep 14, 2026 · 35 MIN

Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 18:7–9 tunaona mabadiliko ya kusikitisha yakianza ndani ya moyo wa Sauli. Baada ya ushindi, wanawake wanaimba wakisema Sauli amewaua maelfu yake na Daudi makumi ya maelfu yake. Sauli anasikia comparison hiyo na kuanzia hapo anaanza kumwangalia Daudi kwa jicho tofauti.Lakini Daudi hajamkosea Sauli. Tatizo ni kwamba mafanikio ya Daudi yameanza kumfanya Sauli ajisikie mdogo.Na hapo ndipo wivu huanzia mara nyingi. Mtu mwingine anapata promotion na badala ya kufurahi tunaanza kujiuliza, “Kwa nini si mimi?” Biashara yake inakua. Anaolewa au anaoa. Anapata mtoto. Ananunua nyumba. Anapata nafasi tuliyoitamani au anatambuliwa na watu. Ghafla, kitu kizuri kinachotokea katika maisha yake kinaanza kutuumiza sisi.Lakini kumbuka hili: baraka ya mtu mwingine si ushahidi kwamba Mungu amekusahau.Safari yake si kipimo cha safari yako. Mungu kufanya jambo zuri katika maisha ya mtu mwingine hakupunguzi kile anachoweza kufanya katika maisha yako.Sauli alianza kwa kusikia wimbo. Kisha akaanza kumwangalia Daudi kwa mashaka. Na baadaye wivu huo utakua na kuathiri maamuzi yake. Hapo tunajifunza kwamba wivu usiposhughulikiwa mapema unaweza kubadilisha namna tunavyomwona mtu ambaye hajatutendea chochote.Kwa hiyo linda moyo wako mapema. Unapoona mwingine akibarikiwa, jifunze kufurahi pamoja naye. Mwambie Mungu kwa moyo wa kweli, “Asante Bwana kwa kile unachofanya katika maisha yake. Na mimi nitaendelea kuwa mwaminifu katika safari uliyonipa.”Huhitaji kuzima mwanga wa mtu mwingine ili wako uangaze. Mungu hajakusahau kwa sababu tu leo ni zamu ya mwingine kusherehekea.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Sep 14, 2026

Embed this episode

Ready to play

Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako!

0:00 35:01

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 35 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on September 14, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!