Waisraeli Walipotamani Kile Wasichokihitaji! episode artwork

EPISODE · Aug 19, 2026 · 12 MIN

Waisraeli Walipotamani Kile Wasichokihitaji!

from Neno la Leo

🎙️ Leo kwenye Neno la LeoLeo kupitia 1 Samweli 8:6–7 tunafika katika hatua muhimu katika historia ya Israeli. Waisraeli wanamtaka mfalme ili wawe “kama mataifa mengine.” Samweli anahuzunika lakini Mungu anamfunulia tatizo kubwa zaidi: “Si wewe waliyekukataa bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.” Walikuwa na Mungu akiwaongoza lakini wakaanza kutamani mfumo waliouona kwa wengine. Neno la leo linatufanya tujiulize kama nasi wakati mwingine tunatamani vitu si kwa sababu tunavihitaji au ni mapenzi ya Mungu bali kwa sababu tunaona wengine wanavyo. Tunaweza kutamani kazi, fedha, mahusiano, nafasi au maisha ya mtu mwingine mpaka tukashindwa kuona kile ambacho Mungu tayari ametupa. Si kila tunachotamani ndicho tunachohitaji na si kila kitu kizuri kwa mwingine ni kizuri kwa kusudi la Mungu juu yetu. Je, tunaweza kumwamini Mungu hata pale mapenzi yake yanapotofautiana na yale tunayotamani? Wakati mwingine baraka si Mungu kutupa tunachotaka bali kutuzuia tusipate kile ambacho tunadhani tunahitaji.Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Aug 19, 2026

Embed this episode

Ready to play

Waisraeli Walipotamani Kile Wasichokihitaji!

0:00 12:45

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Neno la Leo?

This episode is 12 minutes long.

When was this Neno la Leo episode published?

This episode was published on August 19, 2026.

Can I download this Neno la Leo episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!