Episodes
-
Uzalendo
Nini hasa ni maana ya neno uzalendo. Tunatumia vigezo vipi kusema mtu fulani ni mzalendo. Falsafa inasemaje juu ya uzalendo
-
Ukimya wa Hofu katikat Siasa za Tanzania
Nguvu na mbinu zinazotumiwa na serikali ya Tanzania kutengeneza Hofu ili kukabiliana na wale wanaoikosoa. Falsafa inatuambia nini juu ya diplomasia za mabavu zinazotumiwa na serikali ya tanzania
-
Mtego wa maridhiano ya kitapeli
Jinsi gani maridhiano yanatumika kama mtaji kwa wachache na silaha ya ukandamizaji
-
Nani hasa anamiliki chama chako
Umewahi kujiuliza jinsi gani muundo halisi wa chama kilicho tawala kwa muda mrefu ubadilika na kuwa genge la wafanyabiashara. Sheria ya chuma ya Oligarchy inasema nini
-
Mkate na Sarakasi
:Mkate na sarakasi ni dhana inayotumika katika jamii yetu kimkakati, Je falsafa ina lipi la kusema juu ya hilo
-
Ubaguzi wa Kifamilia
Ubaguzi wa kifamilia au nepotism una madhara gani katika jamii na kwanini lazima kuukemea kwa nguvu zote
-
Ugonjwa wa Kiburi
Falsafa inasemaje juu ya kiburi kinachowakuta viongozi
-
Nguvu na Mabavu
Kuna tofauti gani kati ya nguvu na mabavu, je ni kweli taasisi inapopoteza nguvu inaweza kutumia mabavu kuendesha shughuli zake, Falsafa inasemaje juu ya haya
-
Uovu wa Kimfumo
Jinsi gani watu wa kawaida wenye sura nzuri na muonekano wa kawaida, hujikuta wakafanya uovu wa kushitua kwa kisingizio cha kufuata taratibu za kazi.
-
Amani Hasi na Amani Chanya
Hapa tunachimba tofauti kati ya amani hasi inayotangazwa sana na serikali na Amani chanya inayotegema haki.
-
Utilitarianism
Falsafa ya utilitarianism inavyofanya kazi katika serikali na jamii kiujumla
-
Mkataba wa Kijamii
Tunachimba namna mkataba wa kijamii unavyotokea na jinsi inavyoweza kulindwa na raia
About this show
Katika Falsafa za Jamii, tunajadiri kwa kina jinsi falsafa mbali mbali zanavyotumika katika maisha ya kila siku ndani ya jamii zetu
Hosted by
Eudaimonia Ethos
Categories