PODCAST · news
Habari RFI-Ki
by RFI Kiswahili
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
-
24
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuhamasisha kuzuia visa vya watu kujiuwa.
Shirika la afya duniani WHO linasema watu laki 7 na elfu 20 hujitoa uhai kila mwaka. Kujiua ni kati ya sababu tatu kuu ya vifo miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15–29.
-
23
Matumizi ya AI, UN yataka makampuni ya yanayotengeneza teknolojia hiyo kupunguza hatari yake
Mkuu wa ofisi ya tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Volker Turk, hapo jana ameonya kuwa akili unde inaweza kuwa tishio kwa binadam.
-
22
Kauli ya Rais wa Kenya William Ruto kuhusu wafanyabiashara wadogowadogo wa kigeni
Rais akisema wafanyabiashara wa ndani wanahitaji kulindwa. Agizo lake limeibua mjadala kuhusu nafasi ya wageni katika biashara ndogo nchini Kenya.
-
21
-
20
-
19
-
18
-
17
Maoni kuhusu matangazo yetu juma hili
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuzungumzia kila ulichoskia kwenye matangazo yetu au yale yanayoendelea hapo ulipo. Skiza makala haya.
-
16
Uganda: Muhoozi Kainerugaba kuwania urais mwaka 2031
Mkuu wa Majeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwana wa rais Yoweri Museveni, ametangaza kuwania urais ifikapo mwaka 2031. Tunakuuliza msikilizaji ,Uganda inaelekea kwenye kizazi kipya cha uongozi au mwendelezo wa utawala wa familia? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
15
Kigali : Vijana ni viongozi wa leo
Jukwaa la kubadili mtazamo wa Afrika jijini Kigali limewataka vijana wa Afrika kujitokeza na kubadili mustakabali wa maisha yao badala ya kutegemea viongozi wa sasa. Tunakuuliza msikilizaji , vijana wana nafasi gani kuleta mabadiliko ya siasa na uchumi? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
14
EAC : Wiziri wa fedha kupitia simu wazidi
Nchini Kenya, serikali imesema wizi wa fedha kupitia njia ya simu umeongezeka zaidi mwaka huu ikilinganishwa na miaka ya awali. Kuimarika kwa teknolojia ukitajwa kuwa kichocheo. Je nani anapaswa kuwajibikia pesa za mwananchi zinapoibwa kupitia simu ? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
13
DRC : Serikali na waasi wa M23 wakubaliana
Serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23 wamebaliana kuhusu mpango wa mazungumzo ya amani, hatua inayotoa nafasi ya kutekelezwa kwa mkataba wa amani wa Doha na Washington, ili kumaliza vita mashariki mwa nchi hiyo. Skiza maoni ya mskilizaji.
-
12
Uchaguzi nchini Zambia, upinzani yalalamikia matokeo ya uchaguzi
Nchini Zambia, Rais Hakainde Hichilema, amechaguliwa kwa muhula wa pili, akimshinda mpinzani wake wa Karibu Brian Mundubile. Hata hivyo kumeshuhudiwa malalamiko ya dosari kadhaa ikiwemo udanganyifu, wizi wa kura na vitisho, mambo yanayoripotiwa wakati wa chaguzi nyingi barani Afrika.s
-
11
Kuna uwezekano wa asilimia 81 Afrika kukumbwa na hali ya hewa ya Elnino
Ripoti ya wataalam wa hali ya hewa imeonya kuwa Afrika inakabiliwa na uwezekano wa aslimia 81 wa kukumbwa na hali ya hewa ya El Nino. Katika ripoti hiyo, eneo la Kusini mwa Afrika linatarajiwa kukumbwa na
-
10
Vuguvugu la upinzani nchini DRC C64 kutangaza kufanya maandamano Septemba 15
Mwishoni mwa juma lililopita, upinzani nchini DRC kupitia vuguvugu la C64 ulitangaza kuwa utafanya maandamano Septemba 15 kupinga mchakato wa marekebisho ya katiba. Tangazo lao walilitoa baada ya muda waliokuwa wameutoa kwa Rais Felix Tshisekedi kuitisha mazungumzo ya kitaifa kupita.
-
9
Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya, yatoa kanuni mpya za ufadhili wa kampeni
Mwaka mmoja kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imetoa kanuni mpya za ufadhili wa kampeni za wagombea mbalimbali.Mgombea urais atatakiwa kutumia kiasi cha shilingi za Kenya zisizozidi Bilioni 6 huku vyama vya siasa vikitakiwa kutokuvuka matumizi ya bilioni 25 za Kenya.Tumemuuliza mskilizaji ,anazungumzia vipi kanuni hii ?na nchini mwake , kuna utaratibu kama huu?
-
8
Maoni ya mskilizaji Wiki hii kutokana na matangazo yetu
Na Hannah Nalianya Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote kuhusiana na matangazo yetu. Skiza maoni ya Juma hili
-
7
Argentina kuvaana na Uhuspania kwenye fainali
Fainali ya kombe la dunia katika mchezo wa soka, itawakutanisha mabingwa watetezi Argentina na Hispania waliowahi kushinda taji hili mwaka 2010. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumapili nchini Marekani. Unatarajia nani ataibuka mshindi katika mechi hiyo na kwanini. Skiza ya mskilizaji
-
6
Ufaransa yaondolewa kwenye kombe la dunia
Na Hannah Naliaka Safari ya Ufaransa kutinga fainali za kombe la dunia imefikia tamati baada ya kushindwa mabao 2-0 na Uhispania katika nusu fainali ya kwanza. Unazungumziaje mechi hiyo ? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
5
Bara Ulaya linatathimini kudhibiti mitandao kwa watoto
Umoja wa Ulaya unatathmini kuweka marufuku ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto kutokana na athari za mitandao hiyo kwa watoto. Unazungumziaje pendekezo hili? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
4
Nani atabeba kombe la dunia mwaka huu
Fainali za kombe la dunia zimefikia hatua ya nusu fainali, huku timu nne zikisalia kwenye mbio za kutwaa ubingwa. Uhispania itacheza na Ufaransa, wakati Uingereza itapambana na mabingwa watetezi Argentina. Unatathmini vipi hatua iliyofikia? Skiza maoni ya mskilizaji.
-
3
-
2
DRC: Muungano wa upinzani wa C64 kutangaza kuendelea na maandamano yake ya amani Julai 22
Tangazo hilo limetolewa licha ya kushiriki kwenye mazungumzo ya kisiasa na rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
-
1
Siku ya Kiswahili duniani Juni 07 2026
Dunia hivi leo inaadhimisha siku ya Kiswahili Duniani, kutambua mchango wa lugha ya Kiswahili katika kuunganisha watu, tamaduni na mataifa mbalimbali, kauli mbiu ikiwa Kiswahili Lugha ya kimataifa ya amani, mshikamano na diplomasia ya kiuchumi.” Siku hii inafanyika wakati pia RFI Kiswahili tunatimiza miaka 16 tangu tulipoanza kurusha matangazo yetu, una ujumbe gani kwetu?
-
0
Je, serikali ya Afrika Kusini ilichukua hatua za kutosha kulinda usalama wa raia wa kigeni?
Wiki iliyopita, maelfu ya raia wa mataifa mbalimbali ya Afrika waliondoka Afrika Kusini kutokana na hofu ya usalama baada ya maandamano yaliyolenga wageni. Baadhi ya nchi zimeikosoa serikali ya Afrika Kusini kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
-
-1
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
TOPICS IN THIS SHOW
Loading reviews...
Loading similar podcasts...