04 AGOSTI 2026 episode artwork

EPISODE · Aug 4, 2026 · 9 MIN

04 AGOSTI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host ASSUMPTA MASSOI

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama pamoja na afya.Muhtasari wa habari:Utapiamlo mkali nchini Afghanistan umefikia viwango vya kutisha, huku majimbo 12 yakirekodi kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa cha utapiamlo miongoni mwa watoto wakati huu watu milioni 14 wakikabiliwa na njaa kali, imesema WFP.Mjumbe Maalum wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) kwa ajili ya Sudan, Derk Segaar, leo amewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kwamba wiki iliyopita alisafiri kwa njia ya Barabara nchini Sudan na kwamba ingawa macho ya dunia yameelekezwa zaidi katika maeneo ya Darfur na Kordofan, athari za vita zinaendelea kote nchini Sudan ambayo ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani, lakini pia ni miongoni mwa migogoro inayopuuzwa zaidi.Na Umoja wa Mataifa na wadau wake wanaendelea kuisaidia Rwanda kujiandaa dhidi ya Ebola. Hatua hizo zinajumuisha ufuatiliaji katika vituo vya afya, jamii na mipakani, huku zaidi ya wahudumu 100 wakipelekwa kwenye vituo vya kuingilia nchini. Pia, wahudumu karibu 400 wanapatiwa mafunzo ya utambuzi wa mapema.Mada kwa kina:Na sasa ni wasaa wa mada kwa kina inayotupeleka nchini Afrika Kusini, ambako dawa mpya ya kujikinga na Virusi Vya Ukimwi, VVU, iitwayo Lenacapavir, imeanza kutolewa kama sehemu ya jitihada dhidi ya maambukizi mapya, hasa miongoni mwa vijana walio katika hatari kubwa zaidi.Kwa mara ya kwanza, mtu anaweza kujikinga na VVU, kwa kudungwa sindano moja tu kila baada ya miezi sita, bila kumeza kidonge kila siku. Lenacapavir imeonesha ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi, na sasa imeanza kutolewa katika nchi tisa barani Afrika, ikiwemo Afrika Kusini, nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na VVU. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na  Ukimwi, UNAIDS, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anakusimulia. Kwako Feissal. 

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Aug 4, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

04 AGOSTI 2026

0:00 9:56

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on August 4, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!