08 MEI 2026 episode artwork

EPISODE · May 8, 2026 · 10 MIN

08 MEI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Flora Nducha

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bado watu wana kumbukumbu mbichi za ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema wanaendelea kuratibu na kufuatilia kwa karibu mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea kwenye meli ya kifahari ya kitalii na kwamba  “Hatari ni ndogo kabisa, hii si COVID mpya.”Matthew Hollingworth ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) amerejea hii leo kutoka Somalia na kuwaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi yale aliyojionea akiwa ziarani nchini humo kwa wiki moja kuwa “ Nimeona familia ambazo zimeshuhudia madhara mengi  kwa wakati mmoja ikiwemo athari za hali mbaya ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi, athari zote hizo zimekuwa zikisukuma njaa hadi katika viwango vya hatari .”Na, Wanawake na wasichana nchini Lebanon wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kukimbia makazi yao licha ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa Aprili 17 mwaka huu, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published May 8, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

08 MEI 2026

0:00 10:55

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 10 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on May 8, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!