09 JULAI 2026 episode artwork

EPISODE · Jul 9, 2026 · 9 MIN

09 JULAI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Feissal Kirwa

Hii leo jaridani tunaangazia washindi wa Tuzo ya UNFPA, harakati za kutokomeza Ebola nchini DRC, na watoto wenye ulemavu nchini Kenya. Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo  kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma za dharura za uzazi kwa wakati.Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo ukiendelea kuenea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepigwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Uwezo wa kutoa matibabu umeongezeka, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na kuwaruhusu ndugu kuwaona jamaa zao kumeongeza utayari wa wagonjwa kujitokeza.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa juzi Julai 7 imeeleza kuwa ingawa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yameboresha maisha ya mabilioni ya watu duniani, kasi ya maendeleo bado haitoshi kufikia malengo yaliyowekwa ili kufikia mwaka 2030 yawe yametimizwa. Na ingawa Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kundi la watu wenye ulemavu bado ​ linakumbana na changamoto nyingi. Kevin Keitany wa Radio washirika wetu Radio Domus ya nchini Kenya ametembelea moja ya mashirika yanayosaidia watu wenye ulemavu nchini humo ili kuangazia harakati zao za kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jul 9, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

09 JULAI 2026

0:00 9:59

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on July 9, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!