13 MEI 2026 episode artwork

EPISODE · May 13, 2026 · 9 MIN

13 MEI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host ANOLD KAYANDA

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar.Huu ndio mkutano wangu wa mwisho kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema António Guterres, baada ya mkutano wa 10 wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa hii leo huko Addis Ababa, Ethiopia, huku akijinasibu kuwa ushirikiano kati ya vyombo hivyo  wakati wa kipindi chake cha miaka 10 umekuwa moja ya mifano imara ya ushirikiano thabiti wa kimataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, limetoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa kutatua migogoro kwa njia mbadala (ADR), wasaidizi wa kisheria 126 kutoka kisiwani Pemba, Zanzibar ili kusogeza huduma za kisheria karibu na jamii na kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani.Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM. Akizungumza na Flora Nducha Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 uliomalizika mwezi uliopita hapa Umoja wa Mataifa, Farina Gorma afisa mkuu wa shirika hilo la kimataifa katika ofisi ya Stuttgart amesema wanawake wengi wanaowasili Ulaya hukumbana na mtihani hasa wa kupata huduma za afya, msaada wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia..Mwenyeji wako ni Anold Kayandai, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published May 13, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

13 MEI 2026

0:00 9:59

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on May 13, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!