17 JULAI 2026 episode artwork

EPISODE · Jul 17, 2026 · 10 MIN

17 JULAI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Anold Kayanda

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu António Guterres aliyeko ziarani nchini China amehutubia mdahalo kuhusu Tahadhari za Mapema kwa Wote katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika kwenye jukwaa la kimataifa la Akili Mnemba na Tabianchi jijini Shanghai na kutoa wito wa kuharakisha maendeleo ya mifumo ya tahadhari za mapema inayotumia akili mnemba ili kuzuia majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo amesema "tahadhari lazima zifikie kila mtu aliyeko hatarini kwa lugha wanazoelewa na mifumo ya mawasiliano wanayoweza kuiamini."Kesho Julai 18 ikiwa ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, huko Geneva, Uswisi hii leo mashindano ya 18 ya Nelson Mandela ya Mahakama ya Kimataifa ya Kuigiza yamefikia kilele kwa timu ya Chuo Kikuu cha Midlands State kutoka Zimbabwe kuibuka mshindi ilihali Chuo Kikuu cha Strathmore kutoka Kenya kimeshika nafasi ya pili.Hii leo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na marafiki wa mpira wa miguu au kabumbu, wamezindua kampeni ya mwaka mmoja ya  Dunia Moja, Mchezo Mmoja, Lengo Moja kwa lengo la kutumia mpira wa miguu kama kichochea cha kuimarisha afya ya akili kwa vijana, tukio linalofanyika siku mbili kabla ya fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanaume. Akizungumza mapema kabla ya tukio hilo Sahira Al Nahari, ambaye ni Kiongozi kijana mchechemuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs amesema, "kwa hiyo, mpira wa miguu una mengi ya kutufundisha. Tunapokabiliwa na janga la kimataifa, hebu tuzielekeze fikra zetu kwenye viwanja vya mpira wa miguu. Tunapotazama kinachotokea viwanjani, tunajifunza nidhamu, ustahimilivu, na jinsi ya kuinuka tena baada ya kupoteza jambo muhimu sana."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jul 17, 2026

PodParley-generated summary based on available episode metadata and transcript content.

NOW PLAYING

17 JULAI 2026

0:00 10:55

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Et Merdre ! Martin Poirot Et Merdre ! Votre émission vivante consacrée aux spectacles du même genre !Découverte des coulisses de toute les formes de créations artistiques du spectacle vivant : mise en scène, scénographie, jeu, écriture, expositions... Dans chaque émission retrouvez un artiste, un spectacle, un lieu, ou un festival. Aussi disponible en vidéo sur YouTubeUne émission animée par Martin PoirotRéalisée par Zachary GuerenneurIllustrée par Carole MarietHébergé par Ausha. Visitez ausha.co/fr/politique-de-confidentialite pour plus d'informations. Zero Așteptări Paul Puscas Podcastul nostru, este un refugiu de pace și introspecție în tumultul cotidian și în mijlocul așteptărilor adesea nerealiste ale societății. Ne-am dedicat acest spațiu digital pentru a oferi o platformă celor care doresc să exploreze diverse perspective și să participe la discuții deschise, autentice, fără prejudecăți sau anticipații predeterminate. Fiecare episod pe care îl lansăm este o invitație la reflecție și explorare personală, acoperind o gamă largă de subiecte, de la dezvoltare personală și spiritualitate, la cultură, artă și știință, prezentate întotdeauna într-o manieră acc Temps de Dol Temps de Dol Soy 1 de 4. Lo he sido dos veces. Aquí te traigo mi tiempo de duelo para que, si también estás transitando un proceso de duelo gestacional sepas que no estás sola. Hablemos. Escuchemos. Visibilicemos. Y, sobretodo, acompañemos. Podcast de Leyendo Ciencia Ficción Leyendo Ciencia Ficción Un podcast sobre literatura de ciencia ficción de cualquier época.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 10 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on July 17, 2026.

What is this episode about?

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia...

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes, you can download this episode by clicking the download button on the episode player, or subscribe to the podcast in your preferred podcast app for automatic downloads.
URL copied to clipboard!