19 MACHI 2026 episode artwork

EPISODE · Mar 19, 2026 · 10 MIN

19 MACHI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Leah Mushi

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo baada ya takribani wiki mbili mkutano wa 70 wa CSW70 unakunja jamvi.  Maudhui yalikuwa kuendeleza Haki, Sheria na Kuchagiza Hatua kwa ajili ya wanawake na wasichana, na sasa washiriki wanaeleza Idhaa hii wanachoondoka nacho.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo akizungumza na waandishi wa habari Mjini Brussels Ubelgiji kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati akiwa a na Rais wa Baraza la Muungano wa Ulaya António Costa, ametoa ujumbe mahsusi kwa wahusika wakuu wa mzozo huo. Amesema “Kwanza kwa Marekani na Israel, ni wakati muafaka kumaliza vita hivi ambavyo viko hatarini kutodhibitiwa kabisa, vikisababisha mateso makubwa kwa raia, na athari zake zinaenea katika uchumi wa dunia kwa kiwango cha kutisha, zikiwa na uwezekano wa kusababisha madhara makubwa zaidi hasa kwa nchi zenye maendeleo duni”Kisha ujumbe wake wa pili ni “Kwa Iran, acheni kushambulia majirani zenu. Hawakuwa sehemu ya mgogoro huu. Baraza la Usalama limelaani mashambulizi haya na kuamuru yasitishwe, pamoja na kuagiza kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz.”Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Furaha hapo Kesho Machi 20 raia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo lililoghubikwa na mizozo ya silaha wanaeleza furaha kwao inamaanisha nini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Mar 19, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

19 MACHI 2026

0:00 10:57

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 10 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on March 19, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!