24 JULAI 2026 episode artwork

EPISODE · Jul 24, 2026 · 9 MIN

24 JULAI 2026

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani kwa Maendeleo Endelevu awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Ofisi ya Rais inayohusika na Maendeleo ya Vijana, limeendelea kutumia mafunzo ya ufundi stadi kama njia ya kudumisha amani na kuwajengea uwezo vijana kiuchumi. Hii ni katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiwemo namba moja la kuondokana na umaskini na namba 16 linalolenga pamoja na mambo mengine kujenga amani kwenye jamii.Rashid Malekela, balozi kijana wa UNDP Tanzania alihudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina.Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake, UN Women, limeonya kuwa wanawake na wasichana katika mji wa El Obeid nchini Sudan sasa wanakabiliwa na hatari mbili wanapokwenda kuchota maji ambayo ni mashambulizi ya droni mchana yanawalazimu kusubiri hadi usiku, ambako hukumbana na ubakaji na ukatili mwingine wa kingono.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 130,000 nchini Burundi, wengi wao wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRc unaweza kusitishwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu endapo halitapata ufadhili wa haraka.Na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO, umefanikiwa kurejesha utulivu katika eneo la Nyakunde jimboni Ituri, hatua iliyowezesha kurejea kwa harakati dhidi ya ugonjwa wa Ebola.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jul 24, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

24 JULAI 2026

0:00 9:59

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 9 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on July 24, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!