Kunusuru wanawake wenzangu na jamii Gaza inanipa faraja: Alya Abu Shawish episode artwork

EPISODE · Mar 9, 2026 · 2 MIN

Kunusuru wanawake wenzangu na jamii Gaza inanipa faraja: Alya Abu Shawish

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host UN News/Anold Kayanda

Alya Abu Shawish, mwanamke aliyeko mstari wa mbele kuondoa hatari ya mabomu Gaza  (OVERNIGHT)Hii leo pia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, imefanyika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo duniani kote iliadhimishwa jana Jumapili. Katika muktadha huo huo ninamualika Anold Kayanda atupeleke Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kumwangazia Alya Abu Shawish, Mwanamke anayefanya kazi katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa huduma ya kutegua mabomu, UNMASakisaidia kuwaweka salama wenzake katika mojawapo ya mazingira hatari zaidi duniani. Karibu Anold.(Taarifa ya Anold)Asante Flora,Hakika Gaza ni moja ya mazingira hatari duniani kwa sasa. Alya Abu Shawish anaposhuka kwenye gari kabla ya kuingia ofis iza UNMAS zilizoko Deir al-Balah katikatimwa Gaza, anavaa jaketi la kujikinga na risasi.Ndani ya ofisi amesimama mbele ya ramani ya kidijitali, akifuatilia mienendo ya timu za wafanyakazi walioko mitaani zilizosambazwa kote katika ukanda huo wa Gaza ili kufanya kazi za kuondoa mabaki ya vilipuzi vya vita katika eneo hilo.Baada ya mipango yote kukamilika ofisini, sasa Alya Abu anaendesha gari akiwa na wenzake kuelekea kazini nje ya ofisi. Anaeleza akisema,(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kazi yangu kama mwanamke katika eneo hili inaonyesha kwamba wanawake wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha usalama na kuleta mabadiliko yanayoonekana, hata katika mazingira hatari na yenye changamoto kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza.”Alya Abu Shawish anaonekana na wenzake mitaani wakifanya kazi. Watoto wanafuata, kwa vyovyote wakitambua kazi muhimu inayofanywa na UNMAS kufanya mazingira yawe salama dhidi ya vilipuzi.Hata hivyo, nyuma ya dhamira hii ya kitaaluma kuna hadithi binafsi inaloakisi hali halisi ya maelfu ya wanawake huko Gaza.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kama mwanamke na mama, nimepitia changamoto nyingi ambazo wanawake wa Kipalestina huko Gaza hukabiliana nazo wakati wa vita hofu, kuhama makazi, uhaba wa mahitaji muhimu, na hali ya kutokuwa na uhakika kila wakati. Kama wanawake wengi hapa, nimelazimika kuilinda familia yangu huku nikikabiliana na hali hizi ngumu.”Licha ya changamoto hizi, Alya Abu Shawish anasema uzoefu wake umeimarisha azma yake ya kuwasaidia wengine na kumhamasisha kufanya kazi katika uwanja ambao mara nyingi huonekana kutawaliwa na wanaume.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Uzoefu huu haukunidhoofisha; uliimarisha azma yangu ya kuwasaidia wengine. Ulinitia moyo kufanya kazi katika masuala ya kuondoa mabomu na usalama na UNMAS uwanja ambao mara nyingi huonekana kuwa wa wanaume. Katika jukumu hili, ninachangia kupunguza hatari zinazosababishwa na mabaki ya vilipuzi vya vita na kusaidia jamii kuishi kwa usalama zaidi.”Wanawake wengine katika timu za UNMAS pia hushiriki katika shughuli za kuhamasisha jamii kuhusu hatari za mabaki ya vilipuzi, ambayo sasa yamekuwa moja ya changamoto kubwa zaidi za kibinadamu huko Gaza kadri uharibifu unavyoendelea kuenea. Kwa Abu Shawish, juhudi hizi hubeba ujumbe unaokwenda mbali zaidi ya kazi kwani inaonesha uimara na mnepo.

NOW PLAYING

Kunusuru wanawake wenzangu na jamii Gaza inanipa faraja: Alya Abu Shawish

0:00 2:57

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

Et Merdre ! Martin Poirot Et Merdre ! Votre émission vivante consacrée aux spectacles du même genre !Découverte des coulisses de toute les formes de créations artistiques du spectacle vivant : mise en scène, scénographie, jeu, écriture, expositions... Dans chaque émission retrouvez un artiste, un spectacle, un lieu, ou un festival. Aussi disponible en vidéo sur YouTubeUne émission animée par Martin PoirotRéalisée par Zachary GuerenneurIllustrée par Carole MarietHébergé par Ausha. Visitez ausha.co/fr/politique-de-confidentialite pour plus d'informations. Zero Așteptări Paul Puscas Podcastul nostru, este un refugiu de pace și introspecție în tumultul cotidian și în mijlocul așteptărilor adesea nerealiste ale societății. Ne-am dedicat acest spațiu digital pentru a oferi o platformă celor care doresc să exploreze diverse perspective și să participe la discuții deschise, autentice, fără prejudecăți sau anticipații predeterminate. Fiecare episod pe care îl lansăm este o invitație la reflecție și explorare personală, acoperind o gamă largă de subiecte, de la dezvoltare personală și spiritualitate, la cultură, artă și știință, prezentate întotdeauna într-o manieră acc Temps de Dol Temps de Dol Soy 1 de 4. Lo he sido dos veces. Aquí te traigo mi tiempo de duelo para que, si también estás transitando un proceso de duelo gestacional sepas que no estás sola. Hablemos. Escuchemos. Visibilicemos. Y, sobretodo, acompañemos. Podcast de Leyendo Ciencia Ficción Leyendo Ciencia Ficción Un podcast sobre literatura de ciencia ficción de cualquier época.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 2 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on March 9, 2026.

What is this episode about?

Alya Abu Shawish, mwanamke aliyeko mstari wa mbele kuondoa hatari ya mabomu Gaza  (OVERNIGHT)Hii leo pia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, imefanyika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo...

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes, you can download this episode by clicking the download button on the episode player, or subscribe to the podcast in your preferred podcast app for automatic downloads.
URL copied to clipboard!