Lazima tujenge uhusiano mpya na bahari- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa episode artwork

EPISODE · Jun 8, 2026 · 2 MIN

Lazima tujenge uhusiano mpya na bahari- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Assumpta Massoi

Bahari duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazotishia afya ya mazingira na ustawi wa binadamu, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kutoa wito wa hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na hali hiyo. Akizungumza kwa njia ya video katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya Bahari inayoadhimishwa kila mwaka Juni 8, Bwana Guterres amesema bahari ni msingi wa maisha na maendeleo duniani, lakini zimekuwa zikikabiliwa na shinikizo linalozidi uwezo wake wa kustahimili."Bahari inaongoza tabianchi yetu, inalinda mifumo ya ikolojia na uchumi, na inalisha mabilioni ya watu duniani," anasema Guterres na kuongeza kuwa, "bahari ipo kwenye zahma kubwa na tunaishinikiza kupita uwezo wake."Guterres amerejelea Ripoti ya Tatu ya Tathmini ya Bahari Duniani iliyozinduliwa leo, ambayo imebainisha kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, uvuvi uliokithiri, kupotea kwa bionuwai na uchafuzi wa bahari.Katibu Mkuu Guterres amesisitiza akisema, "hatuwezi kuendelea kuichukulia bahari kama kitu kisicho na ukomo," akihimiza kujengwa kwa uhusiano mpya na bahari unaozingatia sayansi, unaoongozwa na sheria za kimataifa na unaojengwa juu ya wajibu wa pamoja wa mataifa, sekta mbalimbali na vizazi vyote.Ametaja mafanikio ya Mkutano wa Tatu wa Bahari wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwaka jana pamoja na kuanza kutekelezwa kwa Makubaliano ya Baiyonuai ya Bahari katika maeneo yaliyo nje ya mamlaka ya kitaifa mwaka huu kama ushahidi kwamba ushirikiano wa kimataifa unaweza kuleta matokeo.Anasema, "hatua za pamoja za kimataifa zinawezekana na ni za lazima."Katika hitimisho la ujumbe wake wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa dunia, sekta binafsi na wananchi kuchukua hatua kwa haraka ili kulinda bahari kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.Anasema, "katika Siku hii ya Kimataifa ya Bahari, hebu tuchukue hatua kwa nia thabiti na kutatua mahitaji ya wakati huu."Hakika yanayosemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yanaendana na aliyoyasema Mwenyekiti aliyechaguliwa wa ya Tume ya Kiserikali ya Bahari ya UNESCO (IOC) kwa Afrika na Nchi za Visiwa vinavyokaribia bara la Afrika (IOCAFRICA) Hellen Gichuhi alipozungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa.

Episode metadata supplied by the publisher feed · Published Jun 8, 2026

Embed this episode

NOW PLAYING

Lazima tujenge uhusiano mpya na bahari- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

0:00 2:50

No transcript for this episode yet

We transcribe on demand. Request one and we'll notify you when it's ready — usually under 10 minutes.

No similar episodes found.

No similar podcasts found.

Frequently Asked Questions

How long is this episode of Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu?

This episode is 2 minutes long.

When was this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode published?

This episode was published on June 8, 2026.

Can I download this Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episode?

Yes. Use the download control on the episode player to save the publisher-provided media file.
URL copied to clipboard!