EPISODE · Mar 9, 2026 · 2 MIN
Mpango wa MEMKWA Tanzania wampa fursa ya elimu mtoto Sanita
from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu · host Un News/Assumpta Massoi
UNICEF: Mradi wa Elimu Kwa Waliokosa warejesha matumaini kwa mtoto wa kikeNchini Tanzania Mpango wa Elimu Kwa Waliokosa au MEMKWA umemwezesha msichana mmoja kuweza kupata haki yake ya msingi ya elimu na kisha kuwa na matumiani ya kutimiza ndoto yake ya kuwa nesi au muuguzi. Simulizi ya Assumpta Massoi inafafanua kisa hicho kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Nats.. 00’00 – 00’14” (Kwa majina naitwa…. Wanaenda shule)Tupo wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania Sanita huyo alishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule.(Sauti ya Sanita)Amerejea shuleni kupitia mradi wa MEMKWA uliotambua kuwa zaidi ya watoto milioni 2 wenye umri wa kuwa shule ya msingi nchini Tanzania hawako shuleni hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau UNICEF na serikali ya Qatar wakafanikisha MEMKWA.Tangu mwaka 2022 zaidi ya watoto elfu 98 katika mikoa 3 ya Tanzania ikiwemo Kigoma, wamenufaika na MEMKWA.Nats…(Darasani) 0’30-0’36” (Shikamoo mwalimu…….la mstatili)Sasa tumo darasani na Sanita ni miongoni mwa wanafunzi. Rashid, mwalimu wa Sanita anaelezea.(Sauti ya Rashid- Mwalimu wa Sanita)Sanita anakwenda ubaoni kujibu swali. Mwalimu anauliza..Nats.. 1’00” – 1’03” (Ameweza, haya tumpigie makofi….fx makofi)Sanita anafunguka..(Sauti ya Sanita)Kitendo cha Sanita kupata haki ya elimu kinamwezesha hata Rhoedesia ambaye ni mama mzazi wa Sanita kuwaza mustakabali wa binti yake.(Sauti ya Rhoedesia) 1’11” -1’20” (NInavyomuona mwanangu anaenda…. ili apate kazi)Mwalimu Rashid anatamatisha na tathmini ya mradi wa MEMKWA na ombi mahsusi.(Sauti ya Mwalimu Rashid)
Embed this episode
NOW PLAYING
Mpango wa MEMKWA Tanzania wampa fursa ya elimu mtoto Sanita
No transcript for this episode yet
Similar Episodes
No similar episodes found.
Similar Podcasts
No similar podcasts found.