PODCAST · religion
Amedeus Live Podcast
by Amedeus D. Raphael
Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo.Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,
Episodes
-
Tumetokana na Mungu
Mungu ni chanzo chetu, tumezaliwa neno lake, tumetokana na yeye. Ametuzaa kwa mapenzi yak, sisi na kazi ya mikono yake, limbuko la kwanza la viumbe wake. Tuna uzima wa aina yake, tuna asili yake na tumejazwa kwa Roho wake.
-
Msingi wa Imani ya Kikristo
Kristo ndani yako nfio maana halisi na mjumuisho mzima wa Imani ya Kristo. ukristo sio dini, ni uhalisia uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Ni maisha halisi ya Mungu ndani ya mwanadamu. Ni Uungu katika mwili.
-
Usijitahidi Kushinda Tena
Usijitahidi kuwa kile ambacho tayari upo, tambua wewe ni mshindi, na umezaliwa kwenye mshindi na upaswa kudhihirisha ushindi kila siku. Ni jadi yako, Mila Yako, asili Yako kuishi na kutembea katika ushindi.
-
Hakuna Baraka zilizosalia Kuomba
Umebarikiwa kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa Roho ndani yake Kristo Yesu. Hakuna baraka hata Moja ambayo bado haujapewa. Tembea kwenye uhalisi huu, tembea kwenye kweli hii! Tembea kwenye Nuru hii!
-
Huburi Maisha ya Ushindi
Duniani Mnayo dhiki lakini Jipeni Moyo, mimi Nimeushinda ulimwengu. Yesu ameushinda ulimwengu kwa ajili yako, changamka, kuwa imara. Tembea na ishi maisha ya Ushindi. Ni jadi yako na haki Yako.
-
Mfunuaji wa Siri za Mungu
Mfahamu Roho Mtakatifu kwa undani kabisa kupitia nakala hii! Roho Mtakatifu ni nafsi hai ya Mungu, yeye ni mfariji wetu, rafiki anaye ambatana nasi kwa ukaribu kuliko yoyote yule katika ulimwengu huu! Mjue binafsi na tembea katika ushirika nae kwa viwango vya kipekee.
-
Uhusiano wa Kiungu
Wewe umeungwa na Bwana Yesu, wewe ni kitu kimoja na yeye! Yeye yupo ndani Yako na wewe upo ndani yake. Uzima wake upo ndani Yako leo, wewe umeletwa kwenye daraja la Mungu! Una uzima na asili ya Mungu ndani Yako Leo hii.
-
Yesu Ndiye Kristo
Elewa Kweli hii na tembea katika uhalisi wake, kwamba Yesu ndiye Kristo, ndiye masihi, Mwokozi wa ulimwengu, Neno la Mungu lililofanyika mwili!
-
Hema Yake Iliyotakaswa
Wewe ni makao ya Mungu, maskani yake. Wewe ni mwakilishi wa Mungu katika ulimwengu wako. Dhihirisha ubora na ukuu wake leo, mtangaze Bwana Yesu kila Mahali ulipo au uendapo. Acha ulimwengu umwone Kristo ndani Yako na kupitia wewe kuanzia leo.
-
Kutembea Ndani Yake
Elewa upo ndani ya Kristo kama wewe umezaliwa mara pili. Elewa Kristo ni eneo, ni maskani na upaswa kuenenda ndani yake kupitia neno lake. Neno lake ni Nuru, taa na uhalisi wa maisha yetu ya kila siku.
-
Haki - Kipawa kwa Wasio Watauwa
Je, unajua ni Kipawa na zawadi kutoka kwa Mungu kwa ulimwengu na sio kwa Wakristo! Kipawa hiki kinakuwa asili yako na uhalisi wako pindi tu unapozaliwa mara ya pili. Kipawa hiki kinakufanya mtawala na hodari katika maisha pale kitambua na kutembea katika Nuru yake. Jifunze zaidi kuhusu Kipawa hiki.
-
Mwenye Furaha kila siku
Mara ngapi umejishangaa kwamba unafuraha na haujui kwanini!? Furaha ni tunda la Roho ya mwanadamu iliyoumbwa upya na hivyo unapaswa kudhirisha furaha siku zote. Dhihirisha furaha kila siku! Furaha ni kitu cha Muhimu Sana katika Ufalme wa Mbinguni. Jifunze zaidi kupitia episodi hii.
-
Jua kile Ulichonacho ndani Yako
Kuza tabia ya Mungu iliyo ndani ya roho yako kwa kupitia ufahamu na utambuzi wa sifa na tabia za Kiungu na asili yake iliyoko ndani yako. Soma waraka wa Filemoni 1:6 katika matoleo mbalimbali ya biblia upate kuelewa jinsi utambuzi wa vile ulivyonavyo ndani yako katika Kristo Yesu vinavyoweza…
more -
Wewe Sema Ndiyo Tu
Usijaribu kuwa vile ulivyo tayari.... Usijitahidi kupata kile ulichonacho tayari... sema tu, Ndiyo. Mfuate Bwana Yesu na atakufanya kuwa mvuvi wa watu. Jifunze namna ya kufuata kupitia somo na ona badiliko la kipekee katika huduma yako ndani ufalme wa Mungu.
-
Wajibu wako wa Kiungu
Elewa wajibu wako ndani ya Mungu. Umeitwa kuzitangaza fadhili za Mungu kila mahali. Umeitwa kumwakilisha yeye kwenye ulimwengu wako. Huu ni wajibu wako kiiungu.
-
Kujenga Tabia ya Kiungu Ndani Yako
Neno la Mungu linauwezo wa kujenga tabia za kiungu ndani Yako kama utalisikia, utaliamini, Ulitafakari na kulifanya kuwa maisha Yako ya kila siku. Wekeza kwenye neno la Mungu na hakika utakuwa na maisha ya ushindi Daima.
-
Kuna Kitu cha tofauti kk kuhusu Wewe
Wewe ni taifa teule, taifa takatifu, jamii ya Mungu, uzao maalumu. Wewe ni milki ya Mungu, wewe sio ajali wala bahati mbaya. Fahamu wewe ni Nani ndani ya KRISTO na ishi katika uhalisi huu!
-
Amefanyika kuwa Sisi pale Msalabani
Alifanyika dhambi yeye asiyejua dhambi... Alichukua asili yetu na kuwa mbadala wetu ili tuchukue asili yake na kuchukua haki yake... Ametufanya kuwa Wana wa Mungu, wenye asili na uzima wa Mungu... Tafakari Kweli hii na tembea katika Nuru hii.
-
Kuzaliwa katika Ufalme wa Mwana wa Pendo Lake
Kuzaliwa mara ya pili ni kigezo dhahiri. Ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu ni Ufalme halisi uliopo na unaofanya kazi hata sasa. Fahamu namna ya kuenenda na kuishi ndani ya Ufalme huu kupitia episode hii.
-
Amekupatia Kila Kitu
Bwana Yesu ni Kila Kitu. Bwana Yesu ni uzima wa milele, yeye ni Mungu wa Kweli. Mfahamu zaidi Yesu na utembee kwenye uhalisi Kweli ya neno lake na mapenzi yake kwako. Kristo ndani Yako ni tumaini la Utukufu na ushindi mkuu! Jiandae kushiriki mkutano mkubwa wa uponyaji unaitwa "Mito ya Uponyaji".
-
Haki yake kwa ajili ya asili yako ya dhambi.
Haki ni zaidi ya kitendo chema kinacholandana na maadili ya Mungu. Haki ni asili ya Mungu. Haki ni namna ya Mungu anavyoona mambo, anavyosikia, anavyofikiri, anavyoitikia na anahukumu! Kupitia Imani ndani ya Kristo Yesu tumehesabiwa haki mbele za Mungu, tumefutiwa hatia na ile hati ya mashitaka...
-
Neno lake ni Uthibitisho Unaouhitaji.
Neno la Mungu li hai, limevuviwa kwa uweza na nguvu ya Roho Mtakatifu! Linaweza kusabibisha mabadiliko na uhalisia wa kile linachosema. Litafakari na kulitegemea neno kila siku! Neno la Mungu ndio Uthibitisho Pekee unaohitaji!
-
Nyimbo za Rohoni
Jifunze kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli! Panda juu zaidi, katika viwango vikubwa zaidi vya ushirika wako na Bwana Yesu kupitia ibada zako binafsi kusifu na kuabudu. Imba wa Roho, imba kwa akili pia. Sifu kwa Roho, sifu kwa akili pia.
-
Omba Kwa ajili ya wengine
Simama katika nafasi iliyowazi kwa ajili ya familia yako, shule, mji na taifa lako. Unaweza kusabibisha mabadiliko makubwa Sana kupitia Dua, Sala, maombezi na Shukrani kwa ajili ya jamii Yako. Bariki ulimwengu leo kwa kupitia Sala na maombezi.
-
Umezaliwa kwa ajili ya maisha Mazuri.
Wewe haukuumbwa kwa ajili ya shida na tabu, Bali ubora, afya njema na utukufu. Fahamu haki, Stahiki na wajibu wako ndani ya Kristo na Tembea katika halisia za Kweli hizi za ufalme!
-
Mafanikio yenye kuongezeka Daima
Umeitwa katika umilele. Mungu aweka umilele ndani Yako. Wewe ni kama mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji. Umeunganishwa na mfumo wa Ugavi wa Mungu.... Mafanikio Yako ni dhahiri, halisi na ya kudumu...
-
Mungu amepangilia maisha Yako kwa Umakini mkuu.
Wewe ni kazi ya mikono ya Mungu, Mungu alikundalia maisha Bora kwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwepo. Anataka utembee katika ubora, utukufu na ukuu kila siku. Mafanikio, ushindi, afya njema, ustawi na tija ni mpango wake kwa ajili yako.
-
Mungu anazungumza Kupitia Neno Lake.
Mungu na Neno lake ni wamoja. Fikra yake, sauti yake, mawazo yake yanawakilishwa katika neno lake! Huwezi kutambua sauti yake kama hautambui neno lake. Jifunze neno lake kila siku.
-
Ishi kwa ajili ya Kristo
Maisha kwako yana maana Gani!? Shauku Yako kuu ni nini katika maisha!? Kwanini unaishi!? Mustakhabali wa maisha Yako ni nini au ni upi!? Sikiliza rhapsodi hii na chagua kuishi kwa ajili ya Kristo.
-
Kuzaliwa mara ya Pili - TeeVo
Isipokuwa umezaliwa mara ya pili hauwezi kuona wala kuingia katika Ufalme wa Mbinguni... Maisha ni jambo la Kiroho, kilichozaliwa kwa Roho ni Roho na kilichozaliwa kwa mwili ni mwili. Fanya sala ya wokovu mara tuu ya Episode hii na uzaliwe mara ya pili leo hii.
-
Shahidi wa Kizazi Chako
Wewe ni shahidi wa Kristo kwa kizazi Chako.... Wewe balozi wa Kristo, shuhuda wa ufalme na Kweli yake... Usikae kimya, usinyamaze, usione haya kwa ajili ya Kristo au injili yake!
-
Tabia ya Kitauwa
Kama mtoto wa Mungu unapaswa kuwa na tabia zinamwakilisha Mungu na kumtukuza Mungu wakati wote. Uaminifu, uadili, upole, ukarimu, kiasi, adabu njema, utauwa, ni tabia unazopaswa kuzionyesha wakati wote. Sikiliza podcast hii kila Siku ili ikujenge vema katika tabia za Kitauwa!
-
Iishi Kweli na Ishi katika Kweli
Kweli ni neno la Mungu Neno la Mungu ni fikra ya Mungu, hekima yake, haki yake, mawazo yake, makusudi yake, mipango yake iliyowasilishwa kwenye maandishi. Ukiijua Kweli, Kweli itakuweka huru.
-
Msifu Bwana Hata Iweje
Mpe Bwana sifa na Shukrani, kwa ukuu wake na ubora, kwa fadhili zake na rehema! Yeye ni Mungu mkuu, muumba wa mbingu na nchi! Anastahili sifa, heshima, utukufu na adhama. Mungu wetu ni Bwana na hakuna kama yeye.
-
Mtoaji mwenye Furaha
Toa kwa moyo wa ukunjufu, bila kulazamishwa, malalamiko au kushurutishwa. Ni heri na baraka zaidi kutoa kuliko kupokea.
-
Fanya Kazi na Roho Mtakatifu
Huduma yako na utumishi wako ufanye kwa kupitia uvuvio wa Roho Mtakatifu! Yeye ndio anaweza kutakasa kazi yako na kuifanya ikubalike mbele za Mungu. Fauta maelekezo yake naye atakuongoza katika safari ya ushindi na ukuu.
-
Alikuja kwetu katika Roho Mtakatifu
Elewa muunganiko wa Bwana wetu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, ni muunganiko wa Ajabu na kipekee. Bwana Yesu ni mfariji aina ile ile kama Roho Mtakatifu, hao wawili ni kitu kimoja. Roho Mtakatifu ni Baba aliyekuwa ndani ya Bwana Yesu, yeye ndiye Bwana Yesu alikuwa akishuhudia kwamba nayatenda yale...
-
Ukiri wangu, Afya yangu
Uzima, afya njema, amani tele, ustawi na ushindi endelevu ni haki Yako ndani ya Kristo. Tumia Kinywa chako kuthibitisha haki hii kila siku katika kila eneo la Maisha Yako. Jiandikishe leo kushiriki ibada mubashara za uponyaji pamoja na mtumishi wetu wa Mungu Mchungaji Chris Oyakhilome, tarehe 15,...
-
Kuna Nguvu ndani ya Neno
Kama mtoto wa Mungu, wekeza muda wako wa kutosha kusoma na kutafakari neno la Mungu. Hakika litakupa ushindi na ubora kwenye eneo la Maisha Yako.
-
Yafumbue Macho Yao
Injili ndio Nuru ya kufungua macho Yao. Wanavyozidi kuisikia injili ndivyo watakavyozidi kutembea kwenye Nuru na kumfahamu zaidi Mungu na mwanawe Yesu Kristo. Endeleza kampeni ya kusambaza injili kila Mahali, fumbua macho ya teenagers wote Tanzania. Jipatie nakala yako ya Teenagers Devotional…
more -
Fanya Imani Yako iwe Hai
Pasipo Imani haiwezakani kumpendeza Mungu... Imani ni kanuni ya msingi katika Ufalme wa Mungu. Pasipo Imani haiwezakani kunyakuwaliwa.... Chochea Imani Yako leo na Hakikisha ipo hai muda wote....
-
Wewe ni Makao Makuu ya Mungu
Mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu. Mwili wako ni maskani yake... Moyo wako ni makao yake, dhihirisha tabia yake, ubora wake na hekima yake kila siku.
-
Kinywa chako - Sheria yako
Kinywa chako ndio kiunganishi kati ya uhalisia wa maisha yako na yale yote aliyokukirimia Mungu katika maisha maisha Yako. Jifunze namna ya kutumia kiunganishi hichi vizuri kwa ajili ya maisha ya ubora, utukufu na ukuu mwingi.
-
Ufalme Unaoendeshwa kwa Maneno
Maneno ni Vitu.... Maneno ni malighafi Muhimu na ya msingi Sana katika Ufalme wa Mbinguni... Maneno yanaweza kuamua hatma yako iwe nzuri au mbaya.... Maneno yanaweza kubadili mustakhabali wa maisha yako kabisa.... Elewa umuhimu wa maneno leo na uyatumie ipasavyo katika Ufalme wa Mbinguni ambamo…
more -
Kuwa na fikra ya Ufalme
Elewa kwamba Kanisa la Yesu Kristo hapa duniani ni sehemu ya Ufalme wa Mungu na hivyo linapaswa kufanya kazi zake kama Ufalme zaidi kuliko taasisi. Fahamu kanuni za Ufalme ambao wewe umezaliwa humo na tembea katika ubora na utukufu wa ufalme huu! Fikra na ufahamu wa ufalme ni dhana halisi...
-
Zingatia maisha Yajayo
Kuna maisha zaidi ya haya! Hapo Dunia tunapita, kuna zama za Muda mrefu zaidi ya hizi za wakati na ziko mbioni kuanza. Fahamu Kweli hii na Anza kujipanga kwa ajili ya zama hizi kwa maana halisi na dhahiri! Usiishi kama hapa ndio mwisho, Hakika hapa sio mwisho wa maisha! Tunatarajia kusambaza…
more -
Utambuzi na Werevu wa Juu
Je Unataka kuwa mwerevu, mwenye utambuzi wa hali ya juu wa mambo yote ya kiroho na kimweli!? Basi unahitaji kulitafakari neno la Mungu usiku na mchana. Neno la Mungu linauwezo wa kukupa maarifa, Werevu, mtazamo, fikra na uwezo wa ufahamu wa juu sana kuliko malighafi nyingine yoyote duniani.…
more -
Fuata Ushauri Wake
Roho Mtakatifu anajua kilichobora kwa ajili yako na kwa ajili ya kila mtu ulimwenguni. Anajua kila kitu, anaweza kukuongoza kwenye kila nyanja ya maisha! Yeye ni Bwana wa mikakati, mshauri wa Ajabu. Maarifa na enzi yote ni Yake...
-
Hekima ya Mungu
Hekima ya Mungu ni neno, neno lake limesheni maarifa yake, fikra zake, mtazamo wake, makusudi na mapenzi yake. Tafakari Kweli Yale leo na utembee kwenye hekima ya Kiungu.
-
Neno katika Mwili
Vipi siku ukikutana na maneno Yako, utayapenda na kuyafurahia au utayachukia na kuyakimbia! Maneno ni vitu, maneno kielelezo chako, cha mawazo, matarajio na mtazamo wako. Maneno Yako ni wewe mwenyewe! Maneno yako yanabeba utu wako!
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
No topics indexed yet for this podcast.
Loading reviews...
ABOUT THIS SHOW
Kufikia wasiofikiwa na kugusa wasio guswa kwa Injili ya Kiumbe Kipya ya Bwana wetu Yesu Kristo.Maudhui ya Podcast hii:Mapitio ya Rhapsodi ya Uhakika, Maungamo ya Afya ya Kiungu, Ukiri wa Imani,Mtazamo wa Mkristo,Mapitio ya Vitabu,
HOSTED BY
Amedeus D. Raphael
CATEGORIES
Loading similar podcasts...