SBS Swahili - SBS Swahili podcast artwork

PODCAST · news

SBS Swahili - SBS Swahili

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

Publisher-supplied feed metadata · PodParley refreshed Sep 25, 2026 · Source feed

  1. 1000

    What are Indigenous Protected Areas in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Maeneo Yaliyolindwa yawatu wa Asili nchini Australia ni yapi?

    National parks, nature reserves, marine sanctuaries and Indigenous Protected Areas protect different environments and operate under different rules. What makes an Indigenous Protected Area different, and how can you find out whether you are welcome to visit? - Hifadhi za taifa, hifadhi za asili, hifadhi za baharini na Maeneo Yaliyohifadhiwa ya Wenyeji hulinda mazingira tofauti na hufanya kazi chini ya sheria tofauti. Ni nini kinachofanya Eneo Lililohifadhiwa la Wenyeji kuwa tofauti, na unawezaje kujua kama unakaribishwa kupatembelea?

  2. 999

    Taarifa ya Habari:Mageuzi ya sheria kuwasilishwa bungeni,kuweka mipaka ya kisheria kwa silaha za Australia na kuweka vikwazo kwa pesa za umma

    Kifurushi cha mageuzi ya sheria kitawasilishwa katika Bunge la Shirikisho leo, ili kuweka mipaka ya kisheria kwa silaha za Australia na kuweka vikwazo kwa pesa za umma, uwekezaji na biashara zinazotumika kuunga mkono mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uvamizi haramu.

  3. 998

    Yaliyojiri Afrika:Kamati itakayo fanyia kazi mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar yazinduliwa

    Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amezindua Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kati ya vyama vya CCM na ACT-Wazalendo, uteuzi huo wa wajumbe 10 unaashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar.

  4. 997

    Prostate cancer in Australia: Testing, treatment and support - Australia Yafafanuliwa:Saratani ya tezi dume nchini Australia: Upimaji, matibabu na usaidizi

    About one in five Australian men will be diagnosed with prostate cancer in their lifetime. Understanding the prostate, your risk and the options for testing can help with early detection and treatment. In this episode of Australia Explained, learn about prostate cancer, PSA testing, treatment and support. - Karibu mwanaume mmoja kati ya watano wa Australia atagunduliwa ana saratani ya tezi dume katika maisha yake. Kuelewa tezi dume, hatari yako na chaguzi za kupima kunaweza kusaidia katika kugundua na kutibu mapema. Katika makala haya ya Australia Yafafanuliwa, jifunze kuhusu saratani ya tezi dume, upimaji wa PSA, matibabu na usaidizi.

  5. 996

    Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yaendelea kukabiliana na shinikizo lakutangaza msimamo wayo kwa viwango vya uhamiaji nchini

    Serikali ya shirikisho imekuwa chini ya shinikizo la kufafanua malengo yake kuhusu mipaka ya visa, Waziri wa Mambo ya Ndani Tony Burke akiahirisha hotuba ya Klabu ya Kitaifa ya Waandishi wa Habari mwezi Agosti ambako alitarajiwa kutangaza kupunguzwa kwa uhamiaji.

  6. 995

    Makala Leo:Tunachojua kuhusu usalama wakimataifa miaka 25 baada ya tukio la 9/11

    Ni miaka 25 tangu karibu watu 3,000 waliuawa katika mashambulizi ya Septemba 11, ambayo yalisababisha Vita dhidi ya Ugaidi vilivyoongozwa na Marekani na kuiingiza Australia katika vita nchini Afghanistan na Iraq.

  7. 994

    Mumbi afunguka kuhusu mapokezi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia

    Wanachama wa Jumuiya zawa Afrika wanao ishi mjini Sydney, walijumuika katika ukumbi wa maarufu wa Opera House na Events Cinema kushiriki katika tamasha ya kila mwaka ya filamu zaki Afrika kuanzia 3-6 Septemba.

  8. 993

    Taarifa ya Habari:Upinzani wa mseto waomba maelezo zaidi kabla ya kura ya mageuzi ya sheria za mitandao ya kijamii zilizo imarishwa

    Makampuni ya mitandao ya kijamii yanaweza kuwapa watumiaji chaguo la kuzima algoriti yao, chini ya rasimu za sheria zilizopangwa kufichuliwa na serikali wiki hii.

  9. 992

    Yaliyojiri Afrika:Agizo la Rais Ruto lazua hofu miongoni mwa wahamiaji wenye asili ya Burundi

    Nchini Kenya, ukosoaji umekuwa ukiongezeka tangu tangazo la Rais William Ruto Jumatano iliyopita. Alisema kwamba biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wageni nchini Kenya lazima zifunge kuanzia Jumatatu, Septemba 7.

  10. 991

    Makala Leo: Unachohitaji kujua kuhusu magonjwa ya msimu huu wa masika

    Australia inapo ingia katika majira ya kuchipua, wataalamu wanawasihi watu wasiache kujilinda dhidi ya magonjwa ya msimu.

  11. 990

    Taarifa ya Habari:Sera ya malipo ya uzeeni ya One Nation yakosolewa vikali

    Chama cha One Nation kina kana kwamba sera yake mpya ya malipo ya uzeeni itasababisha uondoaji mkubwa wa malipo ya uzeeni, au kuongezeka kwa mfumuko wa bei.

  12. 989

    Mumbi afunguka kuhusu maandalizi ya tamasha ya filamu zaki Afrika nchini Australia

    Wanachama wa Jumuiya za Afrika wanao ishi jijini Sydney, New South Wales wana jiandaa kuhudhuria tamasha maalum.

  13. 988

    Makala Leo: Dunia yamkumbuka gwiji wa muziki Dolly Parton

    Gwiji wa muziki wa Country, Dolly Parton, amefariki akiwa na umri wa miaka 80.

  14. 987

    Yaliyojiri Afrika: CCM yamtimua Dkt Emmanuel Nchimbi

    Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM umemvua uanachama Emmanuel Nchimbi na kumpitisha Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kujaza nafasi ya Makamu wa Rais.

  15. 986

    Taarifa ya Habari:Australia yatoa kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal

    Serikali ya Australia inaanzisha kifurushi cha usaidizi cha dola milioni 5 kwa jamii zilizoathiriwa nchini Nepal, huku idadi ya Waaustralia waliopotea ikiongezeka hadi 39.

  16. 985

    Makala Leo:Kwa nini baraza lamawaziri wakitaifa haliku gusa vituo vya mbadala vya data

    Mkutano wa viongozi wa shirikisho, majimbo na wilaya ulimuacha Waziri Mkuu Anthony Albanese akikubali agizo la vituo vya data vinavyoweza kutumika tena.

  17. 984

    Makala Leo:Wa Australia 34 miongoni mwa watu ambao wamepotea katika mafuriko Nepal

    Takriban watu 160 wameuawa, na mamia wakiwemo watalii na Waaustralia 34 hawajulikani walipo, kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea kwenye mpaka wa Nepal na Tibet.

  18. 983

    Taarifa ya Habari:Makumi yawa Australia hawajulikani waliko katika mafuriko nchini Nepal

    Waziri Mkuu Anthony Albanese amethibitisha kuwa Waaustralia 34, hawajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa ya ghafla kwenye mpaka wa Nepal-Tibet.

  19. 982

    Yaliyojiri Afrika:Ujumbe maalum wafuatilia usitishaji mapigano DRC

    Ujumbe wa kwanza wa aina yake umetumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda.

  20. 981

    Taarifa ya Habari:Hospitali za New South Wales kupewa nafasi zaidi za matibabu

    Hospitali za New South Wales zitapata nafasi zaidi za matibabu za muda mfupi ili kupunguza shinikizo kwa idara za dharura.

  21. 980

    Makala Leo: Mrundikano wa visa za wenza unao waacha waaustralia katika sintofahamu

    Mchakato mpya wa kipaumbele ambao unaweza fanya baadhi ya raia wa Australia, wasubiri kwa muda mrefu zaidi kwa wenzi wao kupokea visa umesababisha ukosoaji.

  22. 979

    Makala Leo:'Usibofye kitu chochote':Jinsi barua pepe moja inavyoweza haribu biashara

    Waaustralia wanapoteza mamia ya mamilioni ya dola kutokana na matapeli, huku matapeli wakizidi kutumia akili mnemba kuwadanganya waathiriwa wao.

  23. 978

    Taarifa ya Habari:Ripoti mpya yaitaka Australia iboreshe usalama wa dawa na itoe wakalimani kwa jamii za tamaduni mbalimbali

    Ripoti mpya imeangazia changamoto kubwa za usalama wa dawa zinazowakabili Waaustralia wenye tamaduni mbalimbali, na inatoa wito wa upatikanaji mkubwa wa taarifa na wakalimani wa dawa zinazotumia lugha nyingi.

  24. 977

    Yaliyojiri Afrika:7 wafariki katika ajali ya helikopta Kenya

    Watu saba, wakiwemo raia watano wa Marekani na mkuu wa ujasusi wa Ecuador, wamefariki baada ya helikopta ya watalii kuanguka karibu na Mlima Ololokwe, katika kaunti ya Samburu nchini Kenya.

  25. 976

    Makala Leo:Mabadiliko ya NDIS yatakuathiri vipi?

    Mamia ya maelfu ya watu watapoteza msaada kutoka NDIS, baada ya mabadiliko yanayolenga kupunguza ukuaji katika mpango huo kupitishwa ndani ya Seneti kwa uungwaji mkono wa Upinzani wa Mseto usiku wakuamkia.

  26. 975

    Yaliyojiri Afrika:Askari pori watuhumiwa kwa mauaji ya raia Tanzania

    Kituo cha sheria cha haki za binadamu Tanzania, kime eleza wasiwasi kuhusu madai ya watu kuuawa, kujeruhiwa au kupotea katika maeneo ya hifadhi nchini humo.

  27. 974

    Taarifa ya Habari:Upinzani wa Mseto watishia kuzuia mabadiliko ya NDIS isipokuwa mwanya wa kodi ya mjane utakapofungwa

    Upinzani wa Mseto unatishia kuzuia mabadiliko ya serikali kwa NDIS, isipokuwa serikali ya Labor iharakishe sheria ya kufunga kile kinachoitwa kodi ya mjane.

  28. 973

    Makala Leo:Mageuzi ya NDIS yanatarajiwa kuwa sheria ila, wanaharakati wadai makato yata sababisha madhara

    Mageuzi ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Watu Wenye Ulemavu yamejadiliwa katika Seneti, huku sheria ikitarajiwa kupitishwa wiki hii kwa msaada wa Upinzani wa Mseto.

  29. 972

    Can you pick fruit from someone's garden? - Australia Yafafanuliwa:Je, unaweza chuma matunda kutoka bustani ya mtu?

    Walking through an Australian suburb, you might spot everything from curry leaves and lemons to tomatoes and herbs growing in front gardens or on verges. But is it legal to pick it? This guide explains when it's legal to pick produce, why permission matters, and how community gardens offer another way to grow your own food. - Ukitembea katika kitongoji cha Australia, unaweza ona kila kitu kuanzia majani ya kari na limau hadi nyanya na mimea inayokua katika bustani za mbele au kwenye ukingo. Lakini je, ni halali kuvivuna? Mwongozo huu unaelezea wakati ni halali kuvuna mazao, kwa nini ruhusa ni muhimu, na jinsi bustani za jamii zinavyotoa njia nyingine ya kukuza chakula chako mwenyewe.

  30. 971

    Taarifa ya Habari:Wafanyakazi wa kusambaza vyakula kuongezewa mshahara kuanzia leo

    Takriban idadi yawa Australia 250,000 wanaosafirisha vyakula kutoka hotelini na dukani kwa ajili ya kujikimu, wanatarajiwa kupokea mshahara wa chini kisheria kwa mara ya kwanza.

  31. 970

    Makala Leo:Serikali kuwekeza mamilioni katika nyumba za waathiriwa wa unyanyasaji wa majumbani; lakini je, inatosha?

    Mgogoro wa makazi ukiendelea, vurugu za kifamilia na majumbani (DFSV) ndio sababu kuu ya wanawake na watoto kuondoka nyumbani kwao na kukosa makazi.

  32. 969

    SBS Learn Eng Ep 117 Jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabu

    Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kukopa vitabu katika maktaba?

  33. 968

    Taarifa ya Habari:Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni

    Ripoti ya mwisho kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa na Serikali kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu itawasilishwa Bungeni leo. Uchunguzi huo ulizinduliwa katika mwezi Mei ili kuchunguza mapendekezo ya Serikali, ya kuokoa karibu dola bilioni 38 kwa kipindi cha miaka minne.

  34. 967

    Yaliyojiri Afrika: Uganda na Tanzania za zindua ushirikiano wa nishati

    Bandari ya Tanga itakuwa kitovu muhimu cha nishati katika jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya ushirikiano mpya wa nishati uliozinduliwa kati ya serikali ya Uganda na Tanzania.

  35. 966

    Makala Leo:Sensa imekwisha ila, bado hauja chelewa kama hauja jaza fomu yako

    Sensa ya 2026 imekwisha na idadi kubwa ya Waaustralia walikamilisha utafiti huo mtandaoni.

  36. 965

    Taarifa ya Habari:Serikali yawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama

    Serikali inawahakikishia watu kwamba Sensa itakuwa salama, kufuatia visa vya hivi karibuni vya roboti za AI kufanya ujambazi na uvunjaji wa data katika mashirika makubwa.

  37. 964

    Yaliyojiri Afrika:Wanariadha wa Uganda watoweka Scotland

    Mabondia wanne wa timu ya Uganda, wametoweka baada yakufeli kujitokeza kwa safari zao za ndege zakurejea nyumbani, baada ya kushiriki katika michezo ya jumuiya yamadola mjini Glasgow.

  38. 963

    Makala Leo: Watetezi wa ulemavu waomba mlinzi nakuonya kuhusu 'athari kubwa' mageuzi yanapokaribia

    Watetezi wa ulemavu wanaihimiza serikali kufikiria upya mabadiliko ya Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Ulemavu unao julikana kama NDIS, kabla ya kura ya bunge inayokaribia kuhusu mageuzi yaliyopendekezwa.

  39. 962

    Taarifa ya Habari:Wafanya biashara waomba ushirikiano na serikali kabla ifanye mabadiliko katika uhamiaji

    Vikundi vya wafanyabiashara vinaihimiza serikali ya shirikisho kushirikiana nao, katika mashauriano kabla ya mabadiliko yoyote makubwa kutangazwa kuhusu sera ya uhamiaji.

  40. 961

    Taarifa ya Habari:Ofisi ya takwimu ya Australia yahimiza wanao ishi katika nyumba zenye watu wengi wasiwe na hofu kushiriki katika sensa

    Usiku wa sensa ukikaribia, maafisa wa Ofisi ya Takwimu ya Australia wanawahimiza watu wanao ishi katika makaazi yenye watu wengi sana, wasiwe na hofu yakushiriki kwa sababu hapatakuwa athari yoyote ya kisheria.

  41. 960

    What are my rights if stopped by police in Australia? - Australia Yafafanuliwa:Haki zangu ni zipi kama nitasimamishwa na polisi nchini Australia?

    Police officers have a range of operational powers they can exercise under legislation, including to ask questions, give ‘move on’ directions and conduct searches. Here’s what you need to know about your basic rights and obligations in a police interaction. - Maafisa wa jeshi la polisi wana mamlaka mbalimbali ya kiutendaji ambayo wanaweza kuyatumia chini ya sheria, ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali, kutoa maelekezo ya 'kutoka ulipo' na kufanya upekuzi. Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu haki na wajibu wako wa msingi katika mwingiliano wa polisi.

  42. 959

    SBS Learn Eng Ep 116 Jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyama

    Je, unajua jinsi yakuzungumza kuhusu kumtembelea daktari wa wanyama?

  43. 958

    Taarifa ya Habari:Mfanyabiashara afariki mjini Melbourne baada ya tukio linalo shukiwa kutekelezwa na wezi

    Mfanyabiashara mmoja wa duka mjini Melbourne amefariki baada ya kushambuliwa alipokuwa akijaribu kuzuia kundi la vijana walio kuwa waki iba dukani.

  44. 957

    Yaliyojiri Afrika: DRC yaadhimisha GENOCOST

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, ameongoza kumbukumbuku ya mauaji ya GENOCOST jijini Kinshasa, inayofanyika kila tarehe 2 mwezi Agosti.

  45. 956

    Taarifa ya Habari:Mamia ya watu wakimbia mapigano Tigray na kuingia Sudan

    Mamia yawa Ethiopia kutoka eneo la kaskazini mwa Tigray, wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Sudan katika siku mbili zilizopita, wakikimbia mapigano karibu na mpaka.

  46. 955

    Makala Leo:Australia inakabiliwa na 'tsunami ya uharibifu' mkubwa kutokana na mlipuko wa virusi vya homa ya ndege H5

    Jimbo la Kusini Australia huenda linakabiliwa na tukio la kwanza la vifo vingi vya wanyamapori nchini Australia linalohusishwa na homa ya ndege ya H5N1.

  47. 954

    Makala Leo:Benki ya Hifadhi yasema wa Australia wengi hawa elewi jinsi viwango vya riba vinavyofanya kazi

    Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Australia kimepungua, lakini shinikizo la bei la msingi linabaki kuwa juu sana.

  48. 953

    Taarifa ya Habari

    Mdhibiti wa ushindani [[ACCC]] ameombwa na serikali ya shirikisho kufuatilia vituo vya mafuta kwa matukio yoyote ya kupunguzwa kwa bei - sasa kwa kuwa punguzo la muda la ushuru wa mafuta limeisha.Visa 74 vya aina ya H-5 ya homa ya ndege vimethibitishwa nchini Australia.Hiyo inajumuisha uthibitisho wa tukio la kwanza la vifo vingi humu nchini kutokana na virusi hivyo Kusini mwa Australia.Mji wa Ceuta mwishoni mwa juma haukuonekana tena kama jiji lililokuwa na wasiwasi, lakini wakazi bado walikuwa wameshtushwa na matukio ya wiki. Wengi wa wahamiaji 60,000 walioingia Ceuta wamerudi Morocco.Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.

  49. 952

    Taarifa ya Habari:Kiongozi wa Victoria, ajiuzulu baada ya siku kadhaa za shinikizo dhidi ya uongozi wake

    Jacinta Allan amejiuzulu kama Kiongozi wa Victoria, akisema ni uamuzi sahihi kwa Wa-Victoria. Tangazo hilo limekuja nusu saa tu baada ya changamoto inayotarajiwa ya uongozi katika mkutano uliopangwa wa chama cha wabunge, kuashiria kurudi kwa bunge la jimbo.

  50. 951

    Australia Yafafanuliwa:Tamasha ya Garma ni nini, na kwa nini ni muhimu?

    Kila mwaka, maelfu ya watu husafiri kwenda katika jamii ya kijijini kaskazini mashariki mwa Arnhem Land katika Eneo la Kaskazini.

Type above to search every episode's transcript for a word or phrase. Matches are scoped to this podcast.

Searching…

We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.

No matches for "" in this podcast's transcripts.

Showing of matches

No topics indexed yet for this podcast.

Loading reviews...

ABOUT THIS SHOW

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

HOSTED BY

SBS

Produced by SBS Audio

CATEGORIES

Frequently Asked Questions

How many episodes does SBS Swahili - SBS Swahili have?

SBS Swahili - SBS Swahili currently has 50 episodes available on PodParley. New episodes are automatically indexed when they're published to the podcast feed.

What is SBS Swahili - SBS Swahili about?

Independent news and stories from SBS Audio, connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians. - Taarifa huru na hadithi zinazo kuunganisha na maisha nchini Australia nawa Australia wanao zungumza Kiswahili

How often does SBS Swahili - SBS Swahili release new episodes?

SBS Swahili - SBS Swahili has 50 episodes. Check the episode list to see recent publication dates and frequency.

Where can I listen to SBS Swahili - SBS Swahili?

You can listen to SBS Swahili - SBS Swahili on PodParley by clicking any episode. We provide an embedded audio player for direct listening, and you can also subscribe via your preferred podcast app using the RSS feed.

Who hosts SBS Swahili - SBS Swahili?

SBS Swahili - SBS Swahili is created and hosted by SBS.
URL copied to clipboard!